Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 4 Aprili, 2020
Maandiko Husika
Warumi 12:2-3
2 Wala msifuate kanuni za dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya MUNGU yaliyo mema, ya kuMpendeza, na ukamilifu.
3 Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama MUNGU Alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.
Tito 2:11-14
11 Kwa maana neema ya MUNGU ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa.
12 Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa,
13 huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa MUNGU wetu Mkuu, AliYE MWOKOZI wetu YESHUA HAMASHIAKH.
14 NdiYE AliJItoa nafsi YAKE kwa ajili yetu, ili Atukomboe kutoka uovu wote na kuJIsafishia watu kuwa mali YAKE MWENYEWE, yaani, wale walio na juhudi katika kutenda mema.
Ujumbe wa Kinabii
Tazama mbingu zinasimama wazi mbele yako, mwanaNGU wa zama. Usigeuke kulia au kushoto. Simama na mtazamo uliokaziwa juu YANGU MIMI, ABBA wako YEHOVAH. Mwaka huu utakuwa mwaka wa mateso na kazi ya taabu, lakini pia baraka kubwa. NIko nawe mwanaNGU, hadi hata mwisho wa wakati. Zama juu ya zama NImekuwa nawe na NItaendelea kuwa. Kwa maana, je, si hili ambalo baba aliye na upendo hufanya? NDIMI NILIYE ndiYE BABA wa Zama.
Kila mmoja wenu ni zama, nafasi ya anga, wakati na msimu. Tembea ndani YANGU. Tembea naMI, MIMI, YESHUA wenu. MIMI ndiYE MSAADA wenu uonekanao daima katika wakati wa hitaji na sikuzote huwa mnaNIhitaji, watoto WANGU (Zaburi 46:1). Msiache mwili uwashawishi vinginevyo. NDIMI NILIYE ndiYE lango lenu, ndiYE lango la kuingia kusikojulikana. HamNIjui kwa ukamilifu, watoto WANGU.
Njoni mtembee naMI, watoto WANGU, lakini sio tu maili moja zaidi. Enda naMI mwendo wote – nafasi, wakati, msimu na zama. Kwa maana pamoja naMI vitu vyote vitafunuliwa, kwa maana je MIMI siYE MWANGAZA wenu UONGOZAO? Kwa hivyo enda naMI mwendo wote na hamtawahipotoka.
Nasema, “NIondokeeni enyi watenda dhambi, kwa maana Sikuwahi wajua.” Kuelekea mashariki na kuelekea magharibi Nawavurumisha kutoka kwa koti LANGU. Kama vile mtu hukung’uta vumbi, vivyo Nawakung’uta kutoka kwa uwepo WANGU. Na amani YANGU inarudi KWANGU, inarudi juu ya kifua CHANGU. Msihuzunishe amani YANGU, enyi kizazi kiovu na kisichoaminifu. Hamko imara kama vile maji. Msiotegemewa kabisa. Kaidi kabisa. Nawatapika toka mdomoni MWANGU.
Hukumu ya yule kahaba mkuu itakuja, iko hapa. Kuweni tayari, ee dunia, maana Naachilia Mioto YANGU. Juu yenu Naachilia ghadhabu, hasira kali na kiruu CHANGU. Je, Sipaswi NIkasirike? Sipaswi NIsimame kuhukumu? Napuliza na upepo wa mashariki unakuja. Kuweni tayari, ee ulimwengu, kwa ajili ya mapigo yatakayokuja: mapigo ya nzige, mapigo ya moto, mapigo ya mvua ya mawe. Naachilia kiruu CHANGU kubomoa sanamu zenu, kutikisa kila kitu kinachowezatikisika. Ee ulimwengu, hamna hata habari! Hamna habari kile Naenda kuwatendea.
Mbele yenu, jahanam imefunguka wazi. Mtageuka kulia au kushoto kutoka kwa njia ya uasi, uvundo wa hii zama? Nasimama mlangoni na kubisha. Lakini nani atasikiliza? Nawaita, ee ulimwengu. Lakini mbona mnafunga masikio yenu? Mbona mnafanya mioyo yenu migumu?
Sikutuma [virusi vya] korona lakini NIliviruhusu. NIliviruhusu kujaribu mioyo ya wanadamu, kuona kile wangefanya. Unyama wa mwanadamu kwa mwanadamu. Haivumiliki KWANGU. NIliumba wanadamu kuwa katika umoja, kuNIabudu katika ROHO na katika UKWELI. Lakini mmechukua chambo cha shetani na kuanguka katika tamaa mbalimbali na tofauti tofauti.
Kwa hivyo simameni imara watoto WANGU na mtahadhari, kwa maana shetani huzurura-zurura, huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta yule anaweza mla. Je, mnampa ruhusa, watoto WANGU? Mnampatia ruhusa kupitia amali zenu, maneno yenu, matendo yenu, fikra zenu. Wakati haujakaa ndani YANGU MIMI, MCHUNGAJI wenu MWEMA, unafungulia mlango mwizi aingie ndani.
Pasaka yaja, watoto WANGU. Patikaneni ndani YANGU. Msiache DAMU ya MWANAKONDOO iondoke kutoka kwa mihimili ya milango yenu, kutoka kwa mihimili ya mlango wa moyo wenu. Kaeni ndani YANGU naMI NIkae ndani yenu. Tembeeni naMI NItembee nanyi. Malaika wa mauti, malaika wa mauti ataachiliwa katika njia mpya mwaka huu (Ufunuo 6:7-8). Nyakati zenye hatari kubwa, nyakati zenye hatari kubwa ziko karibu nanyi, watoto WANGU. Kazieni mtazamo wenu sikuzote juu YANGU, bila kugeuka kulia au kushoto.
Jioneni kwenye kamba liokazika, watoto WANGU. Msiruhusu kukosea hatua moja. Endeni sambamba naMI. MIMI ni YESHUA MKOMBOZI wenu; [NIko] hapa nanyi katika mwisho wa zama. Neno LANGU ni aminifu na kweli! Tazama! NIko hapa! Msitazame mwingine, kwa maana pamoja naMI kuna Maneno ya Uzima. Yote mengine ni kivuli tu kinachokimbia, tupu, wazi, bila ukweli, bila riziki. Mbona mjilishe kwenye upepo na kufukuzia kile ambacho hakifaidi? Endeni sambamba naMI.
NIlifanya vile BABA YANGU AliNIonyesha kile cha kufanya. Mnafanya vile baba yenu anawaambia mfanye. Fanyeni mambo yawe sahili. BABA YANGU Hakuwahi NIpa zaidi ya kile NIngewezastahimili na mzigo WANGU ulikuwa mkubwa na mzito. BABA yenu huwa hawapi zaidi ya kile mnawezastahimili na jueni tu neema YANGU abadan haiko mbali nanyi. Mshikilieni tu na mtembee katika UKWELI WANGU, kwa maana si iko hivyo kwamba yule MWANA Anaweka huru yuko huru kweli? Amini na mtapokea, neema juu ya neema, bila chochote kutia shaka. Shaka yoyote hairuhusiwi.
Je, mwili hutia shaka ikiwa umekula baada ya kulishwa? Kwa hivyo msitie shaka Neno LANGU ndani yenu. Ruhusini mizizi kuenda chini, maana karibuni mateso makubwa yatazuka. Tembeeni ndani YANGU na mtapita katikati mwa umati bila kuguswa, bila kudhuriwa. Nawaonyesha Njia. Naangaza njia yenu na kupofusha adui. Kaeni tu katika utiifu. Msiruhusu kukosea hatua. Mafunzo yanaisha. Wote watajaribiwa. Wote wanajaribiwa.
Jifunzeni njia kuu za BABA yenu, kwa maana YEYE ni Kitabu CHANGU kilicho wazi na kuonyeshwa mbele yenu nyote, hata mbele ya ulimwengu ili ulimwengu mzima uone. (Kitabu) hakijaandikwa katika lugha ya ajabu hakiwezi someka au kueleweka, lakini wazi kwa wote kuona, kusoma na kuelewa. Ni kupitia ugumu wa mioyo yenu ambapo vitu vinakosa kuwa wazi na kutatanisha.
MIMI ndiYE TIBA – MIMI, YESHUA. NImeteseka muda mrefu na hiki kizazi kiovu na kaidi ambacho njia zake sikuzote zimepinda nyuma. Kiburi huenda kabla ya mwanguko na mwanguko mkubwa uko karibu. Wanatafuta maarifa na wanatosheka na mambo ya mizungu. Ah, jinsi kizazi hiki kinavyoNIhuzunisha! Maarifa kuenda mbio huku na huko na ee jinsi mnavyowajibishwa KWANGU!
Napeana na Napeana na huu ulimwengu unatosheka na utovu wa shukrani! SItastahimili huu utovu wa heshima tena. Kuweni tayari, ee dunia, kuonja ghadhabu ya MWANAKONDOO na ALIYEKETI kwenye Kiti cha Enzi! Misingi na nguzo za mataifa zitatingishwa, zitaanguka kutowahi inuka tena. Nahuzunika kwa yale lazima NIfanye. Kuweni tayari, ee dunia, kurithi mapigo ya kutotii kwenu. NIliwaonya na NIkawaonya na NIkawaonya! Ni mifano mingapi ambayo MIMI, YESHUA MWOKOZI wenu, NIliwaachia katika Bibilia, NIliwaachia kote [katika] historia ili msiwahifuata?
Sodoma na Gomora zilichomeka katika ghadhabu ya mioto YANGU. Je, mnafikiri nyinyi ni bora kuwaliko wakati dhambi zenu ni mbaya zaidi mara kumi? La! Lakini Nasema watasimama kuwashutumu katika siku ya hukumu. Acheni dhambi! Kimbieni uovu. Natuma wajumbe WANGU kutoa ghadhabu YANGU. Kuweni tayari, ee ulimwengu, kwa maana Natuma Wawili WANGU. Na wataenda wawili kwa wawili. NIsikilizeni! Sikieni Neno LANGU, kwa maana SIzungumzi kwa wepesi. MIMI ndiYE MUUMBA wa nafsi zenu na Najua kile ni bora kabisa kwenu.
NItafuteni mapema wakati NIngali Napatikana. NItafuteni na moyo wenye toba na roho iliyotayari kupokea. Huu sio wakati wa kuoa na kuozwa, wa kula na kunywa kupita kiasi. Lakini huu ndio wakati, msimu, zama, mtu wa kiasi na hamkumtambua. Lakini Nawaita kuwawajibisha, kusimama mbele [za], kujiwasilisha mbele za MWANA (YESHUA) wa Zama. YEYE ni mwenye huruma. YEYE ni Mkweli. Tu msikufuru JINA LAKE au mbele ZANGU Atawakataa, Atawakana.
Fanyeni mambo yawe sahili watoto WANGU, vile NImewaumba kuwa. Msijue woga wowote. Msijue shaka yoyote, kwa maana nyakati za hatari zimeaanguka kote karibu nanyi. Selah.