top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 75 “Usitafute Wapenzi Wengi, Ee Israeli!”

Updated: Apr 13, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 17 Februari, 2020


Maandiko Husika


Hagai 2:6-7

6 Kwa maana YEHOVAH wa majeshi Asema hivi, “Kwa mara nyingine (kitambo kidogo tu) NItazitikisa mbingu, na dunia, na bahari, na nchi kavu;

7 Nami NItatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; Nami NItaijaza nyumba hii utukufu,” Asema YEHOVAH wa majeshi.


Yeremia 4:30

Na wewe, utakapotekwa, utafanyaje? Ujapojivika mavazi mekundu, ujapojipamba mapambo ya dhahabu, ujapojitia wanja machoni, unajifanya kuwa mzuri bure tu; wapenzi wako wanakudharau; wanakutafuta uhai wako.


Yohana 15:1-2

1 MIMI NDIMI MZABIBU wa kweli, na BABA YANGU ndiYE MKULIMA.

2 Kila tawi ndani YANGU lisilozaa Huliondoa; na kila tawi lizaalo Hulisafisha, ili lizidi kuzaa.


Ujumbe wa Kinabii


Ee Israeli, ee Israeli NIsikize siku hii! MIMI, BABA yako YEHOVAH, Nakuita kwa usikivu. Rekebisha njia zako na upate furaha yako ndani YANGU. Pata furaha yako ndani ya YESHUA HAMASHIAKH TAMANIO la mataifa (Hagai 2:6-7). Tulia na ujue kwamba MIMI ni MUNGU. Tulia na usijue woga wowote.


Msihofie majitu yanayotembea nchi. Msihofie kisichojulikana lakini wekeni tumaini lenu ndani YANGU. Jijazeni na Neno LANGU na hamtapotoka. Msitafute usikivu wa mataifa, kwa maana yatawageuka (Yeremia 4:30). Je, hamjajifunza somo vizuri? Wapenzi wenu wote, wako wapi? Katika nyakati zilizopita, je, hawakuwasaliti walivyosaliti wenzao (Ezekieli 16)?

Msiweke tumaini lenu katika mwanadamu na wala msiweke matumaini yenu katika wana wafalme (Zaburi 146:3). Lakini NItumainie MIMI, YEHOVAH, kuwaokoa kupitia MWANANGU YESHUA MASHIAKH AnaYEdumu milele. Katika JINA LAKE mnawekwa huru (Warumi 10:13). Katika JINA LAKE mateka wanaachiliwa. NIsikizeni MIMI na msijue woga wowote. Woga ni jela, utumwa ambao SIjawaweka ndani.


Je, siNIliwapa Torah ili kuwajulisha Njia ya Uzima? Na JINA LAKE ni YESHUA HAMASHIAKH (Yohana 14:6). Kwa hivyo msisikize woga wowote isipokuwa kicho cha YEHOVAH ambacho ni safi, kinadumu milele (Zaburi 19:9).


Patikaneni ndani YANGU, watoto WANGU. Pateni maisha yenu katika chaka la mapenziYANGU [Mapenzi ya MUNGU]. Msiruhusu shughuli za huu ulimwengu kuwasonga roho (Marko 4:19). Potezeni maisha yenu kwa ajili YANGU ili mweze kuyapata milele (Mathayo 10:38-39). NIko nanyi watoto WANGU. Msishangae hili. Msishangae kuwa “NDIMI NILIYE” MKUU Anajua haswa mawazo yenu. Mipango NInayo kwa ajili yenu, watoto WANGU, ni kwa ajili ya uzuri na sio kwa ajili ya uovu.


Kwa hivyo msijue woga wowote. Je, mnaNIelewa? Nawapenda watoto WANGU na upendo WANGU kamili hufukuza woga (1 Yohana 4:17-19). Msiwewasiotii, lakini NIfuateni katika njia zenu zote. MIMI sio tu jambo la kufikiria baadaye, watoto WANGU. MIMI ni BWANA MUNGU MWENYEZI; kuwa mwanzo katika maisha na upendo wenu (Kutoka 20:1-2). Kwa hivyo kuweni dhahiri katika njia zenu KWANGU, watoto WANGU, sio wenye nia mbili. Kuweni imara katika njia zenu zote. Fanyweni imara. Toeni matunda mazuri. Fuateni YESHUA MFANO wenu na mtakaa katika mzabibu (Yohana 15:1-8).


Shikeni mbweha na mtasitawi (Wimbo 2:15). Msiruhusu wanyama waharibifu kuenea kote. Washike na mtasitawi. Msiruhusu bidii yenu ipotee bure. Msiruhusu mharibifu kuharibu. NItumainie MIMI (Mithali 3:5-6). NIfuate. Kuweni katika amani na mjue kwamba MIMI ni MUNGU. Watoto, NIsikie MIMI. NIsikie MIMI na muishi.


Mwisho wa Neno.

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page