Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 18 Januari, 2020
Maandiko Husika
Zaburi 29:1-2
1 Mpeni YEHOVAH, enyi mashujaa,
mpeni YEHOVAH utukufu na nguvu.
2 Mpeni YEHOVAH utukufu unaostahili JINA LAKE;
mwabuduni YEHOVAH katika uzuri wa utakatifu.
Wagalatia 6:9
Hivyo, tusichoke katika kutenda mema, kwa kuwa tutavuna kwa wakati wake tusipokata tamaa.
Ujumbe wa Kinabii
Jinsi mnavyohitaji Mto watoto WANGU! Acheni utiririke kupitia mishipa yenu. Mto wa Ukweli WANGU, Uzima WANGU – ule ule Mto unaotiririka kupitia mishipa YANGU. MnaNIhitaji watoto WANGU. MnaNIhitaji kuwahimili wakati anga zimejazwa na sumu. MnaNIhitaji kuwa hapo wakati [mko] katika mwangaza na wakati [mko] katika giza (Yohana 8:12).
Msijaribu kuNIelewa watoto WANGU, kwa maana nani anaweza jua akili ya “NDIMI NILIYE” MKUU (Warumi 11:34-36)? Tiini tu. Fuateni tu na mtii. Sikizeni tu maagizo yenu na mtii. NIko nanyi watoto WANGU. Je, mko naMI? Sikilizeni tu na mtii. NImewapa [kitabu cha] mwongozo wa maisha. Ni Torah. Msikizeni, MWANANGU YESHUA – Neno lililonenwa na Neno lililoandikwa (Yohana 1:1-5).
Fuateni mwongozo WAKE na msikose hatua, msikose agizo. YEYE ndiYE MCHUNGAJI MWEMA, MWANGALIZI wa nafsi zenu (Yohana 10:11-17). Sasa tazama Njia YAKE na uwe katika wakati WAKE. Kuweni katika mujibu WAKE na hamtawahi kosea, hamtawahi potoka. Msiwahi choka kufanya mema, maana katika hili mnaNIletea utukufu mwingi (Wagalatia 6:9). Mnapoonyesha imani yenu na hamtii shaka kwamba MIMI ni Mtuzaji wa wale wanaoNItafuta kwa jitihada, hili linaNIletea utukufu mwingi!
Njoni KWANGU, watoto WANGU, na msifanye BABA yenu Angoje. Kimbia mwendo. Maliza mashindano. Shinda tuzo (1 Wakorintho 9:24-27).
Ee NIpeni MIMI, watoto WANGU, NIpeni MIMI sifa, heshima, na utukufu (Zaburi 29:1-2). Kwa maana, je, MIMI Sistahiki? Je MIMI Si BABA mwenye upendo AnaYEsababisha watoto WAKE kukwepa mtego wa mwindaji? Je, MIMI, siYE BABA mwenye upendo ambaYE Amejinunulia Bi-Arusi asiye na doa na mkweli? NImeletea wanadamu ukombozi. NImeleta MKOMBOZI wa nafsi na JINA LAKE ni YESHUA HAMASHIAKH (Yohana 3:16-21). Kwa hivyo msitafute mwengine.
Je, mwaNIsikia, ee Wayahudi?! Msitafute mwengine, kwa maana ulaghai tu ndio mtakaopata, mtakutana uso kwa uso nao. NIruhusini kuwasafisha dhambi zenu, kwa maana NIshatengeza njia na JINA LAKE ni YESHUA HAMASHIAKH YULE MTUKUFU. NIruhusini NIweke mafuta ya kupaka macho kwenye macho yenu ili muone Navyoona. Msitumainie katika kazi za mwili. Msitumainie katika tamaduni zenu za wanadamu (Marko 7:1-13). Wokovu, ukombozi unakuja pekee kupitia YESHUA HAMASHIAKH ambaYE mnadharau.
Anakuja tena na moto machoni MWAKE (Ufunuo 19:12). Anakuja tena na mwangaza wa shauku ya macho YANGU. Anakuja kwenu, ee Israeli, na mtafanya nini? Anakuja kuangaza njia yenu, kuwajaza na mng’aro wa ADONAI.
Kuweni waangalifu msikosee MJUMBE WANGU [METATRON] (Malachi 3:1-3). Tahadharini msiguse Safina YAKE. Kuweni watakatifu kama Alivyo Mtakatifu. Anakuja kuangaza njia na kuwaonyesha njia. Anakuja kuwazingira na ulinzi WANGU. MtaMsikiza? Au mtaMuudhi? Ni heri msifanye hivyo. Ee Israeli, tafuteni katika Maandiko na msikasirishe YULE ambaYE Anaenda mbele ya BWANA, hata BWANA MUNGU wenu. Kuweni waangalifu na msiudhi, kwa maana Anakuja Akibeba TAWI. Anakuja kuangaza njia, kuwaonyesha Torah katika matendo, Torah imefanywa sahili, imefanywa wazi.
Msifanye Neno LANGU kuwa tata, kwa maana je, SIkutangaza laana juu ya yule ambaye angeongeza au kuondoa kutoka kwa Neno LANGU (Kumbukumbu 4:1-2)? Basi kijisababu ni kipi cha kusababisha hata watoto wachanga walio sahili kabisa wasielewe? NItawawajibisha kwa ajili ya hili na NInawawajibisha.
Nyakati za giza zaja na mnahitaji kuweza kusikia sauti YANGU (Sefania 1:14-18). Ee watoto WANGU, sikilizeni BABA yenu. Sikilizeni “NDIMI NILIYE” MKUU na msikosee hatua. NIko hapo kusamehe, ndiyo, lakini msifanye mazoea ya kutenda dhambi. Huruma YANGU inatolewa wale ambao wanaNIpenda, ambao hawahuzunishi ROHO MTAKATIFU, ambao wanaMheshimu “NDIMI NILIYE” MKUU, ambao wanaheshimu MWANANGU na Neno LAKE.
Ee Israeli, tilieni maanani njia ZANGU na msitie shaka. Tilieni maanani njia ZANGU na msitende dhambi. Maelfu ya miaka na mmefanya nini na Torah YANGU? MmeMfanya vipi YULE AliYEpeana Neno na kuzungumza kutoka Mlima Sinai? Je, bado mnaogopa kwa kusikia mlio wa sauti YANGU au mnasongea karibu na moyo mnyofu (Kutoka 20:18-21)?
Naifanya ijulikane kwenu siku hii kuwa Nakupenda, ee Israeli. Kama vile NImenena kupitia zama [zote], vivyo hivyo Nanena siku hii (Yeremia 31:3). Msisite kuchukua amri. KuNIheshimu MIMI na BABA YANGU. Naja kuwaosha, ee Israeli. Naja kupanda mimea YANGU katikati yenu. MtaNIruhusu? Je, mtaNIruhusu kuvunja mabonge kwenye shamba, kutunza bustani YANGU katikati [mwake]? Nazungmzia kuhusu mioyo yenu, ee Israeli (Yeremia 4:3-4). Naja kuwatosheleza, kuwaletea amani ya milele. JINA LANGU ni “NDIMI NILIYE” na hakuna aliye kama MIMI, ee Israeli. Msiwahi sahau hilo. Msiwahi sahau njia ZANGU au mtapata doa. NDIMI NILIYE yuko nanyi. Je, mko naMI? Uko wapi mtazamo wa moyo wenu? Juu ya vitu vipumbavu?
MsiNIhuzunishe tena, Israeli. Msihuzunishe BABA yenu au MWANA wa “NDIMI NILIYE” MKUU. NIsikie MIMI, ee Israeli. MIMI NIna upendo. NIna huruma lakini msihuzunishe RUAKH HAKODESH. Msijaribu subira YANGU. NDIMI NILIYE yuko nanyi.
Wakati wa ole u karibu na mnahitaji kuingia chini ya ulinzi wa Mabawa YANGU. Mnahitaji kutumainia katika MASIA wenu na YESHUA ndiyo JINA LAKE. Hakuna mwengine (Yohana 14:6). Njoni katika mikono YAKE ya kuokoa na mtafanywa wazima. Mtapata ufufuo na uzima. Nje YAKE kuna uozo pekee, kuna udanganyifu pekee. Kwa hivyo NItumainie MIMI siku hii, ee Israeli, na msiairishe Wokovu wenu siku nyingine. Kwa maana nani ajuaye kile kesho yaleta?