top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 72 “Israeli, MIMI, YEHOVAH, NIlichora Mpaka Wenu”

Updated: Apr 13, 2024


Umepewa Nabii Shimshon kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 24 Februari, 2020


Maandiko Husika


Ufunuo 1:20

Kuhusu siri ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono WANGU wa kuume na vile vinara saba vya taa vya dhahabu ni hii: Zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, navyo vile vinara saba ni hayo makanisa saba.


Ujumbe wa Kinabii


Israeli, je, SIkuchora mipaka yenu?! Mbona NIliwaacha Misri kwa miaka 400? NIlitayarisha ardhi YANGU pana ikitiririka na maziwa na asali, MIMI, YEHOVAH. Na wakati watenda dhambi walikuwa wameiva kwa mvuno wa uangamizaji, NIliwatoa na mkono wa nguvu, wenye uwezo na ukuu kuteketeza Misri na kuteketeza dunia, wale walioishi katika nchi yenu ya ahadi. Huzuni wa MIMI, YEHOVAH, wakati mkipita lile jangwa. Ni kwa sababu ya Moshe WANGU SIkuwaangamiza wakati huo na kuanza upya naye!


Kwa damu, jasho na machozi mlisakini hii nchi. NIlichora mipaka yenu! NIligawanya nchi! Na nyinyi ni nani kuipeana? Kwa maana haijaandikwa hautapeana ardhi?! Kwa maana ni YANGU, MIMI, YEHOVAH! HUKUMU! HUKUMU! HUKUMU! Itatembelea na kushika maisha yenu, familia zenu, mazao yenu, anga zenu. HUKUMU, HUKUMU, HUKUMU itatembelea marabii wanaokana YULE wanaYEjua ndiYE MASIA wao mmoja na PEKEE!


Mnafuata yule kahaba,Marekani na umalaya wake wote! Kama tu katika siku za Samueli, mlisema, “hatuKUtaki WEWE YEHOVAH, tupe mfalme! Tunaka tuwe kama yale mataifa mengine!” Na NIliwapa Saulo ambaye alichukua wana wenu na mabinti wenu na kuua Makuhani wenu na kukaribisha uchawi katika nchi yenu. Hivyo ilivyo tena! Mnataka juu yenu yule anayewakilisha yote ambayo NINACHUKIA! MkiNItupa MIMI, YEHOVAH, YULE ambaYE Aliwazaa, kwa hivyo damu itatiririka katika barabara zenu. Mmepofushwa sana na kiburi cha maisha, na ustawi, mavazi, nguo za kisasa kabisa, na NItakitia doa na damu yenu!


Kila wakati Naangalia ardhi yenu, Naona damu ya MWANANGU iliyomwagika. Na Naona tena na tena na tena na tena kuteseka KWAKE kwenye huo msalaba! Na Nakumbuka jinsi Alivyoteseka na wakati ambapo NIliwaepusha kwa sababu ya damu ya MWANANGU, NItawaponda maana damu inahitaji hukumu! Ilikuwa mara 2 Israeli! Damu inayookoa, damu inayolia, kwenye MCHANGA WENU! Malaika WANGU anza kuua, Natafuta kuwaamsha! Natafuta kuwaamsha kidogo kwa kidogo. Hukumu YANGU itakuja hadi ghadhabu nzima itaanguka, hadi mlie MBARIKIWA NI YEYE AJAYE KATIKA JINA LA YEHOVAH!


MIMI, YESHUA Nasema, mnawajibishwa zaidi Israeli, kwa maana mnayo Torah YANGU. NIliwaachia mfano ya jinsi ya kuishika. NIlitembea ardhi yenu! NIlisema “Tubu!” Je, SIkusema? Kwa maana Ufalme wa MUNGU, BABA YANGU u hapa. NIlisema nyoka na vipiribao vitalipa. Na basi vita[lipa]. Tubu Israeli, tubu! Tubu, Israeli, tubu! Na mgNIeuzie mtazamo wenu MIMI, YESHUA!


Natuma Moshe WANGU, METATRON WANGU! Alikuja mbeleni Misri! Na Alikuja wakati ghadhabu ya BABA YANGU, [Alikuwa] Amekasirika na Wamisri, hawakuwa na damu na Israeli, wale wenye kiburi ambao walidhani hawakuhitaji damu, na Alileta upanga WANGU na Aliua na wakati Aliona damu Alipita juu.


Tisho, tisho, tisho! Tisho, tisho, tisho! Tisho, tisho, tisho! Damu YANGU pekee inawezarudisha tisho linalokuja! DAMU YANGU PEKEE! Damu YANGU pekee! Sio damu ya kuku, sio damu ya mbuzi, au Wanakondoo. Kwa maana BABA Alitoa MWANAKONDOO kamili! AmbaYE Alikuwa ni MIMI, YESHUA! Abrahamu pia atasimama na Isaka. Maana walikuwa mfano wenu! Waliwaonyesha kile BABA Angefanya. Abrahamu ametuma wengi jahanam, akipima, viwango vya mateso. Mnasema nyinyi ni watoto wa Abrahamu?!


Maana wale wanaokataa MWANANGU YESHUA, jua nyinyi ni wa baba yenu shetani na kazi zake mnafanya. Lakini Natamani mwe WANGU! Nawapenda Israeli! Nawapenda Israeli! Nawapenda Israeli! Njoni KWANGU, kupitia MWANANGU YESHUA! Kupitia MWANANGU, KUPITIA MWANANGU PEKEE! Njoni KWANGU! Ikiwa huna MWANA huna BABA! Ingawa Nawasikia, ingawa Nawapenda, ingawa NImewalinda, lakini NImewaita, NImetuma wajumbe WANGU hata mashahidi WANGU 2, – wengi watafurahia kuona miili yao imelala wafu. Lakini mtasimama katika hofu kuu kuwaona wamefufuka tena. Mtatetemeka hadi kwa mifupa.


Marabii wengi watakufa! Wengi, wengi, wengi, wengi! Wengi wanajua ukweli, na bado wanaMkana, MWANANGU! Kwa maana wanapenda cheo cha Rabii, wanapenda hicho cheo. Mgeukieni RABII MZURI, YESHUA! YULE pekee ni MASHIAKH! Na Donald Trump, Donald Trump, NIlikuinua ulinde Israeli. Unafanya nini Donald Trump? Hata nafsi yako Natamani kuokoa! Hata wewe, ikiwa hautapokea MWANANGU YESHUA utateseka. Kwa wakati huu, bado Nakutumia. Bado Nakutumia. Muda utasema.


Watoto WANGU, jipateni zaidi na zaidi katika pumziko LANGU, zaidi na zaidi katika amani YANGU. Mkijitahidi kutii zaidi na zaidi, lakini jueni, mbinguni yote yasimama kuwapigia vita. Kwa maana huu ndio wakati. Danieli 12 na kutakuwa na vita ambavyo havijawahi kuwa katika mbingu na vitaonekana Duniani. Na katika wakati huu, naam, kutakuwa na wengi ambao wanafuata shetani, lakini wengi watageuzwa kwa uadilifu na kuangaza kama nyota milele na milele. Nyota ZANGU 7 (Ufunuo 1:20). Ng’aeni kwa wangavu kwa ajili ya zile Nyota zingine, ng’aeni kwa wangavu, kwa wangavu zaidi na wangavu zaidi. Ng’aeni kwa wangavu, kwa wangavu na kwa wangavu zaidi! Kwa maana BWANA ARUSI wenu yuaja! MIMI, YESHUA, Naja kuwanyakua nyote!


Tazameni mbele furaha iliyoko mbele yenu! Wakati unasonga karibu wa nyinyi kutukuzwa! Lakini kumbukeni, huo ndio wakati MIMI YESHUA NIlisalimisha maisha YANGU. Na hivyo Nawaambia nyinyi nyote msalimishe maisha yenu. Mtaona zawadi kuu! Kila siku ni nzuri. Kila siku Nawafunza kitu, Nawafundisha, Nawapa kitu, na Naondoa kile ambacho si cha KWANGU MIMI! Kila siku ni nzuri. Na NInazo zawadi hapa Duniani nyote mnapotembea katika miito yenu, jitahidini kila siku zaidi na zaidi na zawadi mtaona. Na MIMI, YESHUA, ndiYE zawadi yenu kuu zaidi!


Mwisho wa Neno.

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page