top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 70 “Yote Itakuwa Edeni Tena!”

Updated: Apr 13, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 13 Januari, 2020


Maandiko Husika


Ufunuo 21:5

NaYE Aliyeketi juu ya kile Kiti cha Enzi Akasema, “Tazama, Nayafanya mambo yote kuwa mapya!” Kisha Akaniambia, “Andika, maana maneno haya ni ya kuaminika na kweli.”


Yohana 11:25-26

25 YESHUA Akamwambia, “MIMI NDIMI huo Ufufuo, na Uzima.

Yeye aNIaminiye MIMI, hata akifa, atakuwa anaishi.

26 Naye kila aishiye na kuNIamini hatakufa kabisa hata milele. Je! Unayasadiki haya?”


Tito 2:11-14

11 Maana neema ya MUNGU iwaokoao wanadamu wote imefunuliwa; 12 nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13 tukilitazamia tumaini lenye baraka na kufunuliwa kwa utukufu wa YESHUA HAMASHIAKH, MUNGU mkuu na MWOKOZI wetu; 14 ambaYE AliJItoa nafsi YAKE kwa ajili yetu, ili Atukomboe na maasi yote, na kuJIsafishia watu WAKE MWENYEWE walio na bidii katika matendo mema.


Ujumbe wa Kinabii


Yote itakuwa Edeni tena mwanaNGU (Ufunuo 21:5). Naam yote itakuwa Edeni tena mwanaNGU. Na macho yako utaona. Na macho yako utaona UTUKUFU WANGU, UTUKUFU WANGU, UTUKUFU WANGU (Yohana 17:24). Mtabadilishwa mnapoona UTUKUFU WANGU na yote itakuwa Edeni tena.


Ona jinsi maua YANGU yanasitawi katika mng’aro ung'aao wa mwangaza WANGU! Natoa uzima na Napokea uzima KWANGU mwenyewe (Yohana 11:25-26). MIMI, YESHUA, ni MUUMBA wa UZIMA na MWENYE ENZI KUU wa Israeli. Tembea naMI, ee Israeli, na acha NIkukumbushe (Mwanzo 13:17). Acha NIwakumbushezile mipaka mizuri iliyowaangukia mababu zenu katika siku za kale (Mwanzo 15:18-21; Zaburi 16:6).


Ng’oa magugu. Tupa nje kinyesi. Tayarisheni enyi Njia ya BWANA (Isaya 40:3-5). Msiwe wakaidi, wenye shingo ngumu. Lakini mfungiwe nira pamoja naMI, “NDIMI NILIYE” MKUU, katika njia iliyo sawa sawa. Tembea naMI katika ROHO na UKWELI. Tembeeni katika njia za kale za Abrahamu baba yenu (Yeremia 6:16). Jinsi mlivyo kwa urahisi sahau njia za haki, densi za Daudi mfalme wenu. Hiyo ndiyo maana tebanakulo limeanguka, limepuuzwa, limehudhurishwa vibaya.

Naita KWANGU watu walio na moyo safi, wale walio radhi kujinyenyekeza, wale wasioogopa kujilaza katika vumbi – hawajichukulii zaidi ya walivyo (Zaburi 24:3-5). Unyenyekevu. Tembea naMI, Bi-Arusi WANGU, mkono katika mkono. Kwa maana Nakuita KWANGU MWENYEWE, mfupa wa mifupa YANGU, mwili wa mwili WANGU. Tembea naMI katika wakati wa jua kupunga, ukikomboa kile Adamu wa kwanza alifeli kufanya, kile Hawa wa kwanza alipuuza kufanya (Mwanzo 3:8).


Kuwa mnyenyekevu, wa roho nyoofu, ee Bi-Arusi WANGU, na usijionezaidi ya kile unachofaa (Warumi 12:3). Kwa maana kiburi kwa wakati wowote hakijafaidi mwanadamu kabisa. Msiogope bali mNItafute na moyo mcheshi uliojawa na neema na rehema. Acha NIone akisi ya BABA YANGU ndani yenu. Acha NIone akisi ya MAMA WANGU wa MBINGUNI ndani yenu. Acha NIone Mbingu yenyewe, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u ndani yenu, sivyo (Luka 17:20-21)?


Ndiyo, na wingu lote la mashahidi litasema, “amina” na “hatahivyo,wachaiwe.” Kwa maana Naamuru jeshi kuu la Mbinguni na wingu lote la mashahidi. Makumi ya elfu ya malaika na kumi ya maelfu ya kumi ya maelfu wanazunguka Kiti cha Enzi cha MWENYEZI yakiMpa shukrani bila kukoma (Ufunuo 5:11-12). Bila kukoma wanatoa sifa, mnafanya [hivyo] watoto WANGU?


Je, watoto WANGU, mnafanya kila mwezalo kuabudu katika ROHO na katika UKWELI? Mnafanya hivyo? Je, mnajishikilia KWANGU na moyo wote? Je, mnafanya kadri mwezavyo kushika amri? Zinafaa kuwa zaidi ya kuangaliwa tu kama mchongo kwenye jiwe au mchoro kwenye bamba. Tangu lini Neno LANGU likawa tu kipande cha mapambo? Mnajua kwa kiasi gani hili linaNIchukiza, watoto WANGU?!


Wanasonga karibu naMI na midomo yao na kuonekana kuwa watakatifu sana katika mapambo ya madoido ya majengo yao lakini hili haliNIpendezi ila limefanywa na roho nyofu, moyo nyofu. Je, ROHO WANGU Anakuongoza? Au moyo wako uko mbali na MIMI? Wanafiki (Mathayo 15:7-9).


Mna mengi ya kuwa na shukrani kwa ajili yake, watoto WANGU. DAMU YANGU iliyomwagwa NIlipeana kwa ajili yenu pale Kalivari (Wakolosai 1:19-20). Pumzi NInayoweka katika mapafu yenu kila asubuhi. NIshukuru MIMI, watoto WANGU – MIMI, YESHUA. Mengi sana mnayo kuwa na shukrani kwa ajili yake. Hata shida za muda NInazoruhusu kuja njia yenu, kwa maana kuzipitia NInawafinyanga na kuwaumba mnapojisalimisha kwa “NDIMI NILIYE” MKUU. Naam, watoto WANGU, NIko nanyi sikuzote. Tu msiNItelekeze MIMI au amri ZANGU. Tumsikatie tamaa Tumaini lenu (Tito 2:11-14). NDIMI NILIYE ndiYE TUMAINI lenu LILILOBARIKIWA kupitia heri na kupitia shari. Msaada wenu uonekanao daima wakati wa hitaji na mnaNIhitaji MIMI watoto WANGU. Msiruhusu shetani au hii dunia iwaambie vinginevyo. Msijiruhusu kufurishwa sana na kiburi kufikiri hamNIhitaji au kuhitaji kuNIkiri katika njia zenu zote.


NIko hapo watoto WANGU kupitia heri na kupitia shari. Msiwahi tupa imani yenu ndani YANGU, kwa maana bila imani haiwezekani kuNIpendeza MIMI, “NDIMI NILIYE” MKUU (Waebrania 11:6). Selah.


Mwisho wa Neno.

12 views

Recent Posts

See All
bottom of page