top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 69 “Sahau Njia Zenu, Ee Wanadamu na MNIshikilie!”

Updated: Apr 13, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 12 Januari, 2020


Maandiko Husika


Yohana 1:29

Siku iliyofuata, Yohana aliMwona YESHUA Akimjia akasema,

“Tazama, MWANA-KONDOO wa MUNGU Aichukuaye dhambi ya ulimwengu!


Isaya 1:16-20

Jiosheni na mkajitakase. Yaondoeni matendo yenu maovu

mbele zangu! Acheni kutenda mabaya, jifunzeni kutenda mema! Tafuteni haki, watieni moyo walioonewa. Teteeni shauri la yatima, wateteeni wajane. “Njooni basi tuhojiane,” Asema YEHOVAH. “Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu, zitakuwa nyeupe kama theluji; ingawa ni nyekundu sana kama damu, zitakuwa nyeupe kama sufu. Kama mkikubali na kutii, mtakula mema ya nchi, lakini kama mkikataa na kuasi, mtaangamizwa kwa upanga.” Kwa kuwa kinywa cha YEHOVAH kimenena.


Ujumbe wa Kinabii


MUNGU Amepaa kwa kelele za shangwe (Zaburi 47:5)! “Sahau njia zako ee mwanadamu na uNIshikilie, kwa maana Naua. Nafanya hai. Tilia maanani njia ZANGU na muimbe nyimbo za manufaa. Shangilia JINA LANGU TAKATIFU YESHUA na msujudu mbele ya Kiti cha Enzi cha “NDIMI NILIYE” wa KUHESHIMIKA. Ametoa uhai WANGU fidia ya wengi (Marko 10:45). Ametoa uhai WANGU, Akimwaga DAMU YANGU kwa ajili yenu, kwa ajili ya upatanisho wa nafsi yenu.


Naua. Nafanya hai (Kumbukumbu 32:39). Hakuna aliye kama MIMI katika dunia nzima. Naam, katika uumbaji wote. MIMI ni MWANA wa “NDIMI NILIYE” BWANA wa Wakati na Nafasi, MUUMBA wa ulimwengu. NaMheshimu BABA YANGU. Je, unaheshimu wako? NInaheshimu Nyumba ya BABA YANGU, lakini mnaNIfedhehesha, ee Israeli, mkisema NIna pepo wakati NImejazwa na ROHO MTAKATIFU (Yohana 10:17-21). Kile kilikuwa wakati huo ndicho kitakachokuwa. MIMI ni YESHUA na MTUNZI pekee wa WOKOVU. NIliYEtumwa na BABA YANGU NDIMI NILIYE. NIlitumwa na BABA YANGU NInapaswa kukomboa Israeli. Kutoka kwa dhambi zake NIlikuja mara ya kwanza kukomboa. NInakuja tena kuangamiza maadui WANGU (2 Wathesalonike 2:8, Ufunuo 19:15).


Wote wale walio upande WANGU ni afadhali wasimame na Moshe (Kutoka 32:26). Moshe hakuNIfedhehesha. Moshe hakuNIvunjia heshima. Alitembea katika Njia ZANGU na kwa hilo NInamtukuza. Lakini msimuabudu kama mungu, ee Israeli, kwa maana alikuwa mwili na damu kama nyinyi. Fungwa katika mwili na bado mtenda dhambi. NIlikuja katika mwili lakini SIkutenda dhambi (Warumi 8:3-4). MIMI NDIMI YESHUA, NAHODHA wenu wa WOKOVU, NIkikomboa Israeli kutoka kwa dhambi zake zote. NIiteni, ee Yakobo, na NItakuja mara moja tena. NInasikia vilio vya watu WANGU lakini je wanasikia vilio vya MUNGU? Je, wanaegemesha masikio yao KWANGU? Je, wanaweka usikivu kwa mwito?


Hakuna kile kimebadilika. Ujumbe bado ni ule ule. Tubuni, kwa maana Ufalme wa Mbinguni u karibu (Mathayo 4:17). Tubuni na muoshwe katika DAMU ya MWANAKONDOO inayookoa. MIMI ndiYE huyo MWANAKONDOO, ee Israeli. MIMI ndiYE huyo MWANAKONDOO Aondoaye dhambi za dunia (Mwanzo 22:8, Yohana 1:29-36). Amini na kutumainia tu. Amini na kutumainia tu na uhuru karibuni mtaona mwishowe. Kwa maana yule MWANA Anaweka huru yuko huru kweli (Yohana 8:36). NIlikuja ili kwamba mweze kupata uzima, ili muupate kwa wingi. NIlikuja kuweka mateka huru. Mko huru ndani YANGU mnapoita juu ya JINA LANGU YESHUA na kugeuka kutoka kwa njia zenu za uovu.


Njia zipi za uovu, mwasema? Dhambi ya kutoamini, ya kutia shaka MIMI ni nani ndani ya BABA ambaYE mnadai kuabudu. YEHOVAH ndilo JINA LAKE! MIMI NIko ndani ya BABA na YEYE yu ndani YANGU (Yohana 10:30). Miujiza NIlifanya ili mweze kuamini. Na mko wapi? DAMU NIlimwaga, na mko wapi? Kwa ajili yenu NIlifanya haya mambo, ee Israeli. Sasa acheni kugeuka mbali na kuwa yule mfarika asiye mwaminifu. Acheni njia zenu za ukaidi na muinamishe goti. Inamisheni goti na mwasilishe mioyo yenu kwa NDIMI NILIYE MKUU. Acheni NIwaoshe. Acheni NIwape kutoka kwa Kikombe ili mnywe. Je, hamjui kuwa MIMI ndiYE MAJI YA UZIMA yaliyozaliwa toka ubavu wa BABA YANGU? Je, hamjui kuwa kwa ajili yenu NIlikufa na kufufuka?


Upendo mkubwa NIlio nao kwenu, ee Israeli! Sasa rekebisheni njia zenu. Acha tuhojiane kabla kumechelewa zaidi, kabla ya mwangamizajiaje na kuharibu (Isaya 1:16-20). Kabla aje na kuharibu hazina zenu za thamani. Ee Israeli, hamtaweza kutambulika wakati NItakuwa NImemalizana nanyi. MIMI pekee Najua kile lazima mpitie ili mNIone kwa dhahiri, kukaa ndani ya kifua cha BABA kama MIMI. Mateso na maumivu makali, ole kuu na shida mtakunywa kabla mseme, “Mbarikiwa ni YEYE AjaYE katika JINA la BABA YEHOVAH” (Mathayo 23:37-39). Na NItawarudia upesi zaidi kuliko tai. NItawabeba MIMI MWENYEWE na kuwaokoa kutoka kwa kila mtego wa mwindaji. NItawafanya mpande sehemu zilizoinuka na mrithi uzuri wa Yakobo baba yenu. Amini tu na msitie shaka. Naja upesi, ee Israeli. Naja karibuni. Je, NItapata nini NItakaporudi kwa Nyumba ya BABA YANGU?


Mwisho wa Neno.

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page