top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 65 “Israeli, Wekeni Nyumba YANGU Katika Mpangilio!”

Updated: Apr 10, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 24 Desemba, 2019


Maandiko Husika


Yohana 14:6

YESHUA Akawaambia, “MIMI NDIMI njia na ukweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa BABA isipokuwa kwa kupitia KWANGU.


Hosea 5:15

NItarudi tena mahali PANGU mpaka watakapokubali kosa lao.

Nao watautafuta uso WANGU; katika taabu yao wataNItafuta kwa bidii.


Ezekieli 33:11

Waambie, ‘Hakika kama MIMI NIishivyo, Asema BWANA YEHOVAH, SIfurahii kifo cha watu waovu, bali kwamba wageuke kutoka njia zao mbaya wapate kuishi. Geukeni! Geukeni kutoka njia zenu mbaya! Kwa nini mkafe, ee nyumba ya Israeli?’


Ujumbe wa Kinabii


Ee jinsi ni nzuri kusifu MIMI, kwa maana MIMI ni tukufu kutazama, NIkifanya miujiza na ujalali katikati mwa Israeli (Zaburi 147:1-3)! Katikati mwa Israeli NInafanya wokovu, NIkitafuta yule Naweza okoa, nani ako radhi kusujudia ukweli. UKWELI. Umewekwa katika jiwe. Haijamomonyokwa na uozaji wa wakati. Milele.


MIMI NDIMI UKWELI (Yohana 14:6). MIMI NDIMI Mwangaza wa Ufalme, sura ya BABA YANGU. MIMI ni nani? YESHUA HAMASHIAKH mzaliwa wa pekee wa BABA (Yohana 3:16-21). NIrudieni MIMI, ee Israeli, na NItawarudia. Maanabado kwa muda kidogo tu Naenda pahali PANGU, lakini karibuni NItarudi (Hosea 5:15). NItaipata vipi nyumba YANGU?


Itakuwa imefagiliwa? Itakuwa katika mpangilio? NItaipata vipi? MIMI NDIMI BWANA wa nyumba (Mathayo 24:45-51). Ee Israeli mmefanya nini na shamba LANGU la mizabibu? Limehifadhiwa? Linatunzwa? Au mliliruhusu liwe jangwa, likiwa limekumbwa na miiba na mbaruti? Mahali ambapo NIlimwaga DAMU YANGU, DAMU ya milele (Yohana 19:17-28).


Ee israeli, jinsi NItakavyorudi kwako! Zungumza tu [yale] maneno (Mathayo 23:37-39). Bariki JINA LANGU. Acheni usemi utiririke kutoka kwa midomo yenu. Msizuie wokovu wenu. Msitafute mungu mwingine au njia nyingine. MIMI, YESHUA, ndiYE Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6). Mnatafuta BABA lakini mnatafuta vikasoro.


Njooni KWANGU, ee Israeli (Mathayo 11:28-30). Nawaita kwa kupunga mkono. Je mnaNIsikia? Je mnaNIhisi? Uchu WANGU unawawakia. Hata mauti hayangeweza kufisha upendo WANGU kwenu (Luka 24:1-12). Hata mapingo katili ya jahanam hayangeweza kuNIzuia. MIMI, YESHUA, ndimi MFALME! MIMI, YESHUA, ndimi MFALME MKUU!


Je, mnaNIsikia, ee Israeli? Hakuna neno la uongo lililotoka kwa midomo YANGU (Isaya 53:9, 1 Petro 2:21-25). MIMI ni MILELE. MIMI NDIMI MFALME. NIabudu MIMI, maana Napeana uhai na sio katika upungufu lakini kwa ujalifu kabisa. MIMI NDIMI uhai wenyewe. NIabudu MIMI na hamtawahi onja kifo. Huwa SIfukuzi wale ambao huja KWANGU, kwa maana Natamani kwamba wote wataokolewa (Ezekieli 33:11, 2 Petro 3:9). Lakini wote lazima wachague. SIwezi wachagulia.



Mwisho wa Neno.

9 views

Recent Posts

See All
bottom of page