Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 10 Desemba, 2019
Maandiko Husika
Kutoka 19:4
‘Nyinyi wenyewe mmeona NIlivyowatenda Wamisri na jinsi NIlivyowabeba kwenye mbawa za tai na kuwaleta KWANGU.
Isaya 52:1-2
1 Amka, amka! Jivike nguvu, ee Sayuni;
Vaa mavazi yako ya fahari, ee Yerusalemu, mji mtakatifu!
Asiyetahiriwa na aliye najisi hataingia kwako tena.
2 Jikungʼute mavumbi yako, inuka, uketi, ee Yerusalemu.
Jifungue minyororo iliyo shingoni mwako,
Ee Binti Sayuni uliye mateka
Yohana 8:34-36
34 YESHUA Akawajibu, “Amin, amin Nawaambia,
kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana
hukaa nyumbani daima.
36 Hivyo MWANA Akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
Ujumbe wa Kinabii
Zungumza, mwanaNGU, zungumza. Tangaza sifa za juu za MUNGU wako, ELOHIM wako, maana YEYE ni mkuu kuokoa, mkuu kuokoa. Akiwabeba watu kwa nguvu ZAKE; mkuu kuokoa (Kutoka 19:4).
Hamjui kwamba ELOHIM, YEYE ni BWANA wenu? Sujudu na mtangaze sifa za juu za MUNGU (Zaburi 149:6). YEHOVAH ndilo JINA LAKE (Kutoka 3:14-15).
Jikingine katikati mwa uwepo WAKE. Usilipe maovu kwa maovu (Warumi 12:17). Bariki na usilaani. Usilaani watu wako, ee Yakobo, ee Israeli. Usilaani lakini wabariki na ukweli. Usifiche jambo. Msipige marufuku fundisho [la MASHIAKH ni nani]. Tangaza YESHUA MASIA katikati mwenu.
Ndipo mtaNIpendeza. Ndipo mtakuwa mnaNIpendeza MIMI BABA yenu, YEHOVAH. MsiNIjifiche. Msijivishe uwongo. Tupeni mbali nira ya mzigo mzito wa dhambi. Msishindane na MUUMBA wenu lakini salimisheni yote KWANGU. MIMI ni ALFA na OMEGA, mwanzo na mwisho. MIMI NDIMI NILIYE. Hakuna mwingine ila MIMI – MKUU KUOKOA (Isaya 63:1).
Ee Israeli, NInawatikisa muamke (Isaya 52:1-2). Ee Israeli, Nawatikisa kutoka kwa usingizi. Wengi wataangamia katika siku zijazo, kwa maana walisinzia, wakiangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6). Pateni maarifa ya kuokoa, maarifa pekee yanayopatikana katika MASIA. Mgeukieni, ee watu WANGU. Mgeukieni na muMwamini na uwezo, nafsi na nguvu zenu zote. Mgeukieni na mtumainie kabisa katika DAMU YAKE, kwa maana YEYE ndiYE upatanisho wenu. YESHUA ndilo JINA LAKE (Luka 1:30-33).
Siku za giza zinakaribia, mwanaNGU. Watu lazima wafunzwe. Lazima wafunzwe jinsi ya kukimbia na kujificha wakati ghadhabu YANGU na hasira YANGU kali inapita (Isaya 26:20-21). Lazima wafunzwe jinsi ya kukimbia na kujificha ndani YANGU. Lazima wafunzwe jinsi ya kushika amri. Lazima wafunzwe dhambi ni nini, kwa maana mstari wa maadili umefifia (Marko 7:20-23, 1 Yohana 3:4).
Endelea kutaipu mwanaNGU, maana hili linaNIpa UTUKUFU wakati unaandika kile Nasema, kile Nasema ili watu wasikie. Watakusikiza. Watasikiza kile wale saba WANGU wako nacho kusema. Watatambua ukweli na ukweli utawaweka huru kwa wale wote watapokea na kuamini (Yohana 8:31-36).
Kwa hivyo Nawatia moyo siku hii kuendelea kutabiri. Endelea kuhubiri ukweli. Endelea kutangaza lile makanisa hayatahubiri, lile wachungaji waovu wanene hawataki lisikike. Hawahubiri kuishi takatifu. Hawajali wanapowatapeli kondoo Jumapili moja baada ya nyingine (1 Timotheo 6:3-12). Yote wanayojali kuhusu ni wao wenyewe na jinsi ya kutajirika haraka. Wanalainisha mifuko yao na dhahabu na fedha ilhali kondoo na wanakondoo WANGU wana njaa. Kuna siku ya kulipa karibu, yaja haraka na upesi.
Hukumu yao hailali na wala si legevu (2 Petro 2:1-3). Wanahesabu huruma YANGU kwa ajili ya kuruhusu dhambi yao. Wamekosea kabisa. Natabiri maangamizo! Natabiri hukumu juu ya hawa wachungaji waliopotea, juu ya hawa mbwa mwitu katika mavazi ya kondoo! NItakuwa na siku YANGU mahakamani (Yeremia 2:35)! NItajaribu waovu! Wale wote ambao hawatatubu... ingekuwa ni heri kwao wasingekuwa wamezaliwa. Hivyo Asema MIMI, YEHOVAH!
Hili ndilo Nataka kusema. Hili ndilo Nataka kuwaambia watu. Kwa hivyo waambie mwanaNGU na usipie marufuku neno moja. Kwanza Nakuambia yanene. Kisha NItakutuma kwao kutangaza katika usikivu wao. Haitakuwa rahisi kama vile haikuwa rahisi kwa Yeremia lakini alitii nawe pia [utatii].