top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 59 “Na NIliJIvisha Mwili, Ee Israeli!”

Updated: Mar 25, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 9 Novemba, 2019


Maandiko Husika


Kumbukumbu 10:12-13

12 Na sasa, Israeli, YEHOVAH MUNGU wako, Anataka nini kwako, ila umche YEHOVAH, MUNGU wako, na kwenda katika njia ZAKE zote, na kuMpenda, na kuMtumikia YEHOVAH, MUNGU wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;

13 kuzishika amri za YEHOVAH na sheria ZAKE, ninazokuamuru leo, upate uheri?


Yohana 1:14

NaYE NENO Alifanyika mwili na Akakaamiongoni mwetu.


Ujumbe wa Kinabii


Je hamNIsikii MIMI, ee Israeli? Tazama nyota ZANGU saba na jinsi zinavyong’aa kwa ajili YANGU, jinsi zinavyong’aa kwa ajili ya MIMI, YESHUA, zikiangaza njia mbele YANGU, zikiwa kama taa kwenye nyayo ZANGU, zikitayarisha Njia ya BWANA wao, zikitayarisha Njia ya BWANA katika hizi nyakati za mwisho, katika nyika ya mwanadamu (Ufunuo 1:12-16).


Tazama, ee Israeli, na muogope (Kumbukumbu 10:12-13)! Ogopeni mbele ZANGU! Tetemekeni mbele ya MUNGU wenu! NInakuja kukagua. Naja kuona kile mmefanya na Sheria ya Torah YANGU. Mmetendea nini huu mti ambao NImepanda katikati yenu (Mithali 3:18)? Hamko kama taifa lolote, maana kwa taifa lipi NIlipatia kwa neema mnoTorah YANGU, Mwongozo wa Milele – yasiyo ya kawaida yakija kwa ya kawaida.


Na NIliJIvisha mwili, ee Israeli, ili tu NIngekuja kuwaona, kutabenakulo miongoni mwenu (Yohana 1:14). Ee gharama ya juu iliyoje NIlilipa ili kutabenakulo miongoni mwenu! DAMU NIliyomwaga kwa ajili ya kila mmoja wenu. Lo mito ya DAMU NIliyomwaga toka kwa mishipa YANGU yenyewe. Hamna hata nusu ya picha, ee Israeli, kwa maana hakuna nambari ya vitabu ambavyo vingeweza kushikilia kile NIlifanya kwa ajili yenu hiyo siku. Inameni na muabudu mbele ZANGU. MIMI NI MUNGU MILELE NIkiwa NImekuja chini katika mwili kuzalia BABA YANGU matunda mengi mazuri. Lakini ni kina nani mnaoNIpokea kama baraka na sio laana?


NDIMI NILIYE haheshimu [hadhi ya] mtu yeyote (Warumi 2:11). NInakemea mmoja NInavyokemea mwengine. SInyimani marekebisho YANGU. Maana kwani si kairipio ZANGU ndizo mwongozo wa maisha? Kwa hivyo NInawakemea, ee Israeli! Njooni KWANGU na acheni NIwaoshe. Acheni NIwaoshe, ee Israeli, dhambi zenu. Kwa maana ingawa dhambi zenu ziwe kama nyekundu, NItawafanya nyeupe kuliko theluji (Isaya 1:18).


Je hamNIsikii ee Israeli? Kwa maana NItawabeba kwa upole ikiwa tu mtaruhusu. MIMI NDIYE MCHUNGAJI (Isaya 40:9-11, Yohana 10:11-16). Nyinyi ndio kondoo. Naja kuwakomboa, kuwaweka huru kutokana na mbwa mwitu [aliye] katika mavazi ya kondoo. Anasimama katikati yenu akiwa tayari kuwameza. Tahadharini na muonywe. Pendeni vitu vilivyo juu, sio vitu vinavyowatukuza nyinyi (Wakalosai 3:1-4). Kwa maana katika kujitukuza unaanguka katika uwongo. Wakati tu mnatafuta UTUKUFU WANGU ndipo mnapotoka katika makubaliano na uwongo.


Kuweni kama MIMI, takatifu na takaso. Kuweni kama MIMI, bila lawama na kweli. NImeweka mbele yenu njia ya Amani. Chagueni uzima ili muweze kuishi (Kumbukumbu 30:19). Mnajua kile Nazungumzia, kwa maana NIlitembea barabara za Yerusalemu. DAMU YANGU bado inalia hadi siku hii, bado inaombea Yerusalemu ndogo sana. Ee NIsikizeni MIMI na mjue uzima! MIMI ni YESHUA HAMASHIAKH, hata MASHIAKH wenu. NIdaini MIMI leo na muache kuNIfukuza!



Mwisho wa Neno.

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page