Unabii 58 “Wewe ni Nani Ewe Mtu Hodari? NInapopeana Sheria Uumbaji Wote Unatii!”
Updated: Mar 25, 2024
Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umepokewa 11 Juni, 2019
Ujumbe wa Kinabii
Achilia moto WANGU na usizuie. Maana NImeghadhabika na mataifa na kuNIpuuza kwao. Lakini hili linakuja kuisha sasa. Nyinyi nyote mNIsikize sasa. Tubuni na mgeuke kutoka kwa uovu wenu. Kwa maana huu ni wakati wenu wa mwisho, maana huu ni wakati wa mwisho na safina inafunga haraka. Safina YANGU ya usalama. Na wale wote ambao wako nje, mvua itakuja; mvua ya hofu YANGU kuu (hili ni fumbo ya ghadhabu ya YAH, ambayo Atai-“mwaga duniani” na utawala [Ufalme] WAKE ambao unakuja. MUNGU Ameahidi kutoangamiza dunia na maji tena). Kwa maana mtajifunza jinsi wa kuogofya na Mkali BWANA, NDIMI NILIYE Mkuu Alivyo (2 Wakorintho 5:11)! NInapotuma mapigo YANGU juu yenu. Pigo baada ya pigo na kuwaadhibu hadi muinamishe goti lenu KWANGU; na mkiri dhambi zenu mbele YANGU. Mambo yenu ya kuchukiza kabisa. Na NInaYE Mfalme WANGU Azungumze nanyi, tubuni na mrudi KWANGU! Zile nafsi zote ambazo ni ZANGU kabla ya kuwekwa kwa msingi wa dunia (Waefeso 1:3-5,11; Warumi 8:29-30; 9:23). Kwa wale mliobaki mnaenda jahanam, moto wa jahanam. Kwa maana imeteuliwa nyinyi [kwa wale wa kuenda kwa moto wa jahanam na pia]: wale kwa njaa kuenda kwa njaa, wale kwa upanga wa nchi mbili kuenda kwa upanga wa ncha mbili, wale kwa utumwakwa utumwa, na hukumu haitarudishwa nyuma. Kwa maana imeamuriwa nyinyi, [kwa ajili] ya usaliti wenu wa MIMI kabla ya hivi vitu vyote. Na NInaimarisha hukumu YANGU juu yenu.
Kwa maana ingawa hamNIkiri, bado NInatawala juu yenu. MIMI ni YEHOVAH na wote wataNIjua, watajua utukufu WANGU unapojaza dunia, kutoka bahari hadi bahari. Na mataifa yote yatainama mbele YANGU... mbele ya MWANANGU YESHUA. MFALME wa Wafalme wote. Na katika hizi nyakati za mwisho NImewaamuria nafasi, tumaini la kugeuka nyuma. Kwa hivyo Nazungumza sasa kwa wote ambao watasikiza. Utakuwa yupi? Yule anayeinamisha goti lake na kutubu? Au yule anayeNItikisia ngumi yake? Ingawa katika huruma YANGU NInawasihi. Hiyo ndiyo maana hukumu imekuja. Hiyo ndiyo maana adhabu zimekuja! Kwa maana NInawasihi! Vimbunga vinapoinuka, NInawasihi. Bahari inapoinuka, NInawasihi. NIrudieni! Ni heri mrudi KWANGU! Na mpande katika safina ya usalama, AMBAYE ni MWANANGU YESHUA na uokoe nafsi yako. Ijapokuwa katika wakati huo hautakuwa na ulinzi wa kimwili, nafsi yako NItaokoa.
Mnahitaji afya na uponyaji na YESHUA pekee Anaweza leta hiyo. Kwa hivyo, kwa wale ambao wameamuriwa wokovu, njoo! Maana ROHO na Bi-Arusi Wasema “Njoo!” Na wanaNIita na NInakuja. Na NInawaita mtwayehaya Maji Yaliyo Hai kwa uhuru. Kwa hivyo njoo (Ufunuo 22:17).
Maana nyinyi nyote mmepotosha ukweli. Na kwa kweli umeanguka, umeuawa njiani (Isaya 59:14-15). Lakini katika hizi nyakati, wote wataNIjua. MIMI NI YEHOVAH na kile Nasema ndicho. Na amri YANGU yasimama. NInatawala na kumiliki kutoka Mbinguni juu, NInatawala wanadamu wote. Mtaona ghadhabu YANGU. Kitu cha kutisha mno kwa yule yuko huko, yeyote, kusimama mbele ZANGU ikiwa haujafunikwa na Damu ya MWANANGU [YESHUA].
Kwa hivyo nyinyi nyote njooni. Nyinyi nyote mliolemewa na mizigo, njooni. Pateni pumziko lenu ndani YANGU (Mathayo 11:28). Pateni afya yenu ndani YANGU. NIpeni nafsi zenu. Kwa maana katika wakati huo NInaahidi kuwaokoa. Lakini ikiwa wapatikana bila Damu YANGU, bila MIMI, ni uchungu mkubwa utapitia. Maana kifo kitatoroka wengine kama mojawapo wa adhabu YANGU, nidhamu YANGU (Ufunuo 9:6). [Kwamba] Ingekuwa rahisi sana kwa kifo kuja tu, lakini mtateseka matokeo ya dhambi zenu duniani kabla muende jahanam. Kwa hivyo NInawaomba kama NInavyofaa kuja na NIruhusini kuwarejesha kwa kile ukweli kilicho. Sio kile dunia imekufunza, bali ukweli. MIMI NDIYE Ukweli, Njia na Uzima. Na hakuna ajaye kwa BABA ila kupitia MIMI. Na ikiwa una tumaini lolote la ghadhabu YAKE kutulizwa, basi utakuja KWANGU. Na NIruhusu NIkufunike. Na NIkuvishe mavazi mapya. Mavazi ya uadilifu. Mavazi masafi. Mavazi yanayong’aa, meupe pe bila alama au mkunjo. Isipokuwa wewe mwenyewe ulichafue. Lakini hata wakati huo, NItakuwa nawe kukufunza ukweli. Toba ya kweli na Damu YANGU vitakufunika kuyaosha tena. MIMI NDIMI NILIYE MKUU. Na katika wakati huu, Naisema tena! Wote watapata kujua MIMI ni nani! Hakutakuwa na asiyeamini duniani! [Kutakuwa na] Maadui tu ambao wanafikiri wanawezapigana dhidi YANGU. NIna ujumbe kwenu: NItawaua. Ni rahisi jinsi hiyo. NItawaua. Kwa hivyo jiingizine katika msitari na muifanye iwe rahisi KWANGU. Na kwa mpigo mmoja NItapita ndani yenu. Wale wote wanaotafuta kuzuia njia YANGU, MUUMBA, NDIMI NILIYE MKUU.
Nazungumza nawe ewe dunia, MIMI NDIMI NILIYE. MIMI ni YULE YULE jana, leo na milele. Na SIbadiliki (Waebrania 13:8, Malachi 3:6)! Na vitu ambavyo NIlitengeneza, NIliJItengenezea na kile Nasema ndicho kile Nasema na hilo linasimama (Mithali 16:4)! Kwa hivyo ni heri mmbadilike! Kwa maana huu ni ujumbe kwa mwanadamu wote! TUBUNI kama bado kuna wakati! Tubuni kama bado kuna wakati! Kwa maana ni jambo la kuogofya kuanguka katika mikono ya MUNGU ALIYE HAI. Na haijalishi ni mara ngapi inaNIlazimu NIseme hili katika neema na rehema YANGU sikuzote kuna wale wakaidi na wenye shingo ngumu ambao wanafikiri wanawezajaribu NDIMI NILIYE. Kwa hivyo ikiwa unataka kujaribu NDIMI NILIYE, endelea basi. “Ishi maisha yako mazuri kabisa wanavyosema.” Kwa maana siku moja mbele ZANGU utasimama. Hukumu! Na bado Nasema “NIondokee ewe mtenda dhambi.” Na jahanam unaenda na hakuna chochote unawezafanya “Ewe mtu shupavu na hodari.” Kwa maana hakutakuwa na siku ambazo NItainamisha goti LANGU kwenu! Kwa maana NIambie lini ulinyosha timazi, ukapima mbingu, ukapatia nyota utaratibu zao na kusema “hii ni sheriakwenu. Msiizidi!” (Ayubu 38:8-11). Kama vile tu NIlifanya na bahari na mchanga! MIMI ndiYE NDIMI NILIYE MKUU! NInapopeana sheria uumbaji wote unatii. Wewe ni nani mtu hodari? Mtu mnyonge! Ili wewe usitii sheria ZANGU? Usiheshimu na kustahi sheria YANGU? Kwa hivyo wewe NIambie lini uliita waridi [likawa] bila kutoka popote, ukaweka nyota juu, ukaumba jua, mwezi na dunia kwa nguvu zako. Halafu NItakupa heshima. Hadi hiyo siku ambayo haipo, tubu na utii.