top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 56 "Kuweni Waaminifu na Mwe Waangalifu! Neno la 2019 na Kuendelea"

Updated: Mar 24, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 25 Februari, 2019


Maandiko Husika


1 Nyakati 21:13

Naye Daudi akamwambia Gadi, “Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa YEHOVAH; kwa kuwa rehema ZAKE ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa mwanadamu.


Zaburi 37:5-6

5 UMkabidhi YEHOVAH njia yako, Pia uMtumainie, naYE Atakutendea.

6 Ataitokeza haki yako kama nuru, Na hukumu yako kama jina la adhuhuri.


Ujumbe wa Kinabii


YESHUA Azungumza: Ee Bi-Arusi WANGU mrembo, jinsi moyo wako umekuwa nyororo mbele YANGU. YESHUA wenu Amependezwa na ukuaji Anaoona. Kutoka utukufu hadi utukufu Nakupeleka na SItawahikoma, kwa maana tamanio LANGU ni kwamba muwe WANGU kama Bi-Arusi WANGU – mmetiwa sahihi,mmetiwamuhuri, mmekombolewa. Na mtakuwa. Endeleeni tu kuwa wanyenyekevu mbele YANGU.


Nyinyi nyote kuweni wanyenyekevu mbele YANGU. Huo unapaswa kuwa mtazamo wenu. Kila wakati kuwa radhi kuchukua pigo, kuteseka kwa ajili ya JINA LANGU. Lazima NIongezeke na lazima mpungue. Hakuna njia nyingine ya uzima, uzima WANGU kusitawi ndani yenu. MIMI NDIYE Ufufuo na Uzima, je, MIMI siYE? Kwa hivyo NIruhusu kusitawi katika kila hali, katika kila jambo. Pungua na MIMI NItaongezeka, inuka.


Natan’El azungumza: “Kuweni waaminifu na muwe waangalifu,” ndiyo maneno nayosikia kwa ajili ya 2019.


YESHUA Azungumza: Kwa hivyo kuweni tayari Bi-Arusi WANGU, kwa maana NItakuja katika saa ya usiku wa kati, moto wa tamaa – Shauku YANGU. Ilikuwa ni Shauku YANGU kwa Bi-Arusi WANGU NIlikufa, NIkiwa NImesulubiwa kwenye mti wa Kalivari. Kwa ajili yake [Bi-Arusi] NIlikufa na kwa ajili yake NIlifufuka. Kwa hivyo kaa kando YANGU na msiNIvunje moyo. Msiegemee kwa kushoto au kwa kulia lakini juu YANGU pekee. Angalia katika macho YANGU na muone siri ya ajabu. MIMI ndiYE MFALME wa Wafalme na BWANA wa Milele, MWAMBA wa Milele na hata zaidi. [HALLELU YAH!]


Kwa hivyo msitie shaka upendo WANGU kwa Bi-Arusi WANGU. Namkujia karibuni na hakuna chochote kinaweza NIzuia. Fanya taswira ya poromoko likija chini kwenye mlima. NInashuka na yowe na ukelele wa ushindi. Kwa hivyo jitayarisheni Bi-Arusi WANGU na muwe tayari.


Puliza mwanaNGU, kwa maana upepo wa mabadiliko unakuja tena, umeachiliwa toka kona zote za dunia. Puliza, puliza, puliza, puliza. Ndio, mwanaNGU, nyakati zinabadilika, kubadilishwa kwa walinzi, msimu wa nne, nyakati za mwisho, unyakuzi wa Bi-Arusi WANGU huku wakifurahishwa mno na upendo WANGU. Ee jinsi Navyopenda Bi-Arusi WANGU! Neema, neema, neema ambayo NImekabidhi juu yake haitaondoka kuenda kushoto au kulia. Amevishwa katika ukweli, rehema YANGU, ELOHIM. Ndio, kwa maana mmevaa KRISTO (Warumi 13:14, Wagalatia 3:27). Yeye, Bi-Arusi WANGU, haridhiki na chochote kingine, sio kabati la Babiloni – ukahaba wa ukahaba.


Ukatili mkubwa uko karibu kuachiliwa juu ya hii dunia, hii sayari dhaifu. Kuweni tayari! Kuweni tayari! Kuweni tayari, watoto WANGU! Pakieni mifuko yenu. Tayarisheni mifuko yenu ya kutoroka [nayo], kwa maana itawabidi kukimbia na kujificha. Jificheni katika neema tele ya mikono YANGU ya pumziko. SIwafanyi muogope, bali Nawapa ukweli wa hali. Siku za Obadia ziko hapa! Ingieni katika mapango yenu, watoto WANGU na mjifiche kwa muda kidogo (Isaya 26:20-21).


NItakapowafanya muibuke, itakuwa kama wakati MWANANGU YESHUA Aliibuka kutoka kwa kaburi la kuazimwa.


Ufufuo uko nanyi! Uzima! NInawawezesha zaidi na zaidi kila siku. Ishike! Twaa siku! Carpe diem (Karpe diem ni Kilatini cha, “twaa siku”)! Kwa maana hii na kila siku ndiyo siku YEHOVAH Ametengeneza kwa hivyo tufurahie na tushangilie ndani yake (Zaburi 118:24)! Je wajua hakuna chochote chaweza kutendekea ila NIkiruhusu? Kila siku fanya vile Daudi alifanya. Jiweke katika mikono YANGU ya rehema. Sema, “ABBA YEHOVAH, siku hii ninachagua kuweka maisha yangu katika mikono YAKO ya rehema kama kitendo cha hiari yangu, kwa maana ni heri nianguke katika mikono ya MUNGU AISHIYE kuliko katika mikono ya wanadamu” (2 Samueli 24:14).


Tazama na muone, tazama na muone kile NItakachofanya. NItasongeza milima kwa ajili yenu. NItaua waovu. NItapeana ukombozi. Tazama na muone miujiza. Tazama na muone maajabu. NDIMI NILIYE YUKO nanyi hadi hata mwisho wa nyakati (Mathayo 28:20). HALLELU YAH!!!



Mwisho wa Neno

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page