Unabii 54 "Mitindo ya Kipagani Hufungua Mlango Katika Nyumba Yako"
Updated: Mar 24, 2024
Umepewa Nabii Shimshon kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 1 Novemba, 2019
Maandiko Husika
Yohana 5:45
“Lakini msidhani kuwa MIMI NItawashtaki mbele za BABA, yuko anayewashitaki, hata Musa, ambaye mmemwekea tumaini lenu.”
Malachi 4:4
“Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.”
Marko 7:8
“Ninyi mwaiacha amri ya MUNGU, na kuyashika mapokeo ya wanadamu.”
Mithali 2:8
“Kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki na kuhifadhi njia ya waaminifu WAKE.”
Ujumbe wa Kinabii
Nilikuwa nimeona maono ya malaika kwa maji. Alikuwa ameshikilia ngao mbili mikononi mwake, moja ikiwa dhahabu katika mkono wake wa kulia na moja ya fedha katika mkono wake wa kushoto. Nilitanabahi pia maneno ‘Shema’ na “Moshe” yalikuwa katika ndimi zangu mara nyingi tulipokuwa tukiombea dunia wakati wa sikukuu ya uovu ya ‘Halowin’ [Kimombo – Halloween].
Nilisikia hili,
“Msikie Moshe WANGU (Yohana 5:45).
“Ikiwa mngeshika Torah, watu wa hii dunia na mNIpokee MIMI, YESHUA, NIngewezawaweka nyote salama. Lakini ninyi kina mama na kina baba wajinga mlipeana watoto wenu kwa nguvu za adui wa nafsi zenu kunyanyaswa, kuteswa, kuua, kuiba na kuangamiza.
Kumbukeni Torah ya mtumishi WANGU Moshe, kwa maana Moshe WANGU wa Sasa Anakuja kuhukumu (Malachi 4:4). Ndiyo Moshe yuko hapa. NInarudisha nyuma nguvu za giza mbali na watoto WANGU watiifu. Hii ndiyo taswira, inategemea juu ya jinsi mlivyo watiifu watoto WANGU, hii inaamua ulinzi, kwa maana NIliwaambia muache mitindo yenu ya kipagani (Marko 7:8). Mlifungua mlango wa kuingia katika nyumba zenu kwa sababu hamkusikiza watumishi WANGU manabii. Lakini kwa sababu ya maombi, NInaonyesha rehema. NInakujia Bi-Arusi asiye na doa. MnaNIpendeza watoto WANGU. Mbinguni yasimama kuwashangilia kwa maombi yenu siku hii, korti za Mbinguni pia zinawashangilia na kuwashukuru.”
Muhtasari: Fasiri ya maono ni hii, ngao ya dhahabu inawakilisha ulinzi mkuu zaidi kwa watoto watiifu wa YAH. Ngao ya fedha inawakilisha ulinzi wa chini kwa wale ambao utiifu wao uko chini. Lakini rehema ya YAH ilionyweshwa kwa watoto WAKE dunia nzima kwa sababu ya kuomba kwetu (Mithali 2:8).