top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 52 “Nguvu ZANGU Zimekuja Chini Kwenye Hii Dunia Kuonya na Kujaribu Mwanadamu.”

Updated: Mar 24, 2024


Umepewa Nabii Shema’Yah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 20 Julai, 2019


Maandiko Husika


Ufunuo 11:3-6

NAMI NItawapa mashahidi WANGU wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.” Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za ELOHIM wa dunia yote. Kama mtu yeyote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo impasavyo kufa mtu yeyote atakayetaka kuwadhuru. Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.


Yoeli 2:1-3

Pigeni shofar [tarumbeta] katika Tisyon; pigeni mbiu katika mlima WANGU mtakatifu. Wote waishio katika nchi na watetemeke, kwa kuwa siku ya YEHOVAH inakuja. Iko karibu, siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na utusitusi. Kama mapambazuko yasambaavyo toka upande huu wa milima hata upande mwingine jeshi kubwa na lenye nguvu linakuja. Jambo kama hili halijakuwepo tangu zamani wala halitakuwepo tena kamwe kwa vizazi vijavyo. Mbele yao moto unateketeza, nyuma yao miali ya moto inawaka kwa nguvu. Mbele yao nchi iko kama bustani ya Edeni, nyuma yao ni jangwa lisilofaa: hakuna kitu kinachowaepuka.


Ujumbe wa Kinabii


NIsikieni sasa, nyinyi nyote watumwa wa hii dunia. Kwa maana nguvu ZANGU zimekuja chini kuwaonyesha njia ya Ukweli. Na ikiwa mtu yeyote hatawapokea ninyi Mashahidi WANGU Wawili hapo ndipo panapo hukumu (Yoeli 2; Ufunuo 11).


Matumaini kwa watoto WANGU ambao wanapokea ukweli na ahadi za Neno LANGU zilizoandikwa kutoka zamani. NIsikie mwanaNGU, endelea kuzungumza! Nguvu ZANGU zimekuja chini kwenye hii dunia kuonya na kujaribu mwanadamu na kufichua matendo yao maovu. Katika saa hii, Nawatuma wajumbe WANGU na wangapi wataamini katika kuja kwa Mwana wa Adamu tena (Mathayo 23:31-39)?! Lakini hii ni nafasi yenu ya mwisho ee dunia!


Na haijalishi hiziufunuo, ikiwa unazipokea na kuamini, lakini jua ukweli huu ambao umetegemezwa na Maandiko YANGU! Ikiwa haupokei ukweli, hili neno, mwito WANGU, kurudi kwa Torah, hizi kweli za Torah, basi ujue, SIkujui na katika Ziwa la Moto utaenda (Mathayo 13:41-42).


(YEHOVAH Anasema kwamba si jambo la wokovu kupokea ufunuo ambazo Amefunua katika hii Huduma ya Torah Keeper (Mshika Torah), lakini kile ambacho ni muhimu zaidi ni kwamba Torah Keeper (Mshika Torah) inafunza ukweli wa wokovu katika YESHUA MASIA na hitaji la kushika zile Amri 10 na Sheria za Torah. Ikiwa hutapokea huu ujumbe wa toba na kurudi kwa Torah, basi utaenda Jahanam na Ziwa la Moto.


Ndipo Yuda, siyo Iskariote, akaMwambia, “BWANA, itakuwaje kwamba Utajidhihirisha kwetu na si kwa ulimwengu?” YESHUA Akamjibu, “Mtu yeyote akiNIpenda atalishika Neno LANGU na BABA YANGU Atampenda, naSI TUtakuja kwake na kufanya makao YETU kwake.” [Yohana 14:22-23])


Kwa maana hizi kweli zimetegemezwa na upendo wa watoto WANGU ambao kila siku wanaweka katika utendaji Sheria za Torah YANGU na wako wazi mbele ya wote kuonekana jinsi wanavyopendana vile NImwewapenda. Wakiweka chini maisha yao kwa ajili ya kila mmoja wao, kama vile tu NImewafunza (Yohana 13:34; Yohana 15:12-17). Lakini enyi ee dunia, ambao hampokei hizi kweli, ni hukumu tu inayobaki!


Hakuna hofu kwa watoto WANGU! Hamna lolote la kuogopa. NInapotuma wajumbe WANGU kwenu kuwaokoa kutoka kwa hatia zenu wenyewe, kutoka kwa njia zenu wenyewe. Kutoka kwa uongo ambazo mliamini ndani yake. Vitu vibaya ambavyo mlifunzwa. Na NInatangaza baraka YANGU juu ya wote ambao wanapokea Mashahidi WANGU Wawili. Kwa maana imeandikwa katika Yoeli 2, ‘...na mbele yao ni Edeni, na nyuma yao ni jangwa lisilofaa na nchi kavu.’ Na hili linamaanisha nini ee dunia? Kwamba NImekuja chini kwenu, katika Mashahidi WANGU Wawili, watoto WANGU. Na wale ambao wamependa ukweli na kuamini watachanua. Tunda lao litapewa, baraka YANGU itafuata (YEHOVAH Asema kwamba Atabariki wale ambao watapokea Mashahidi WAKE Wawili kukua haraka katika maarifa YAKE, ambayo ni uzima wa milele [Yohana 17:3]). Lakini kwa wale ambao hawajali na wamependa giza na [hawajapenda] ukweli, [wa]taingia katika nchi iliyokauka na kavu na chovu. Na NItawabandua kila kitu mshawahijua. Kila baraka hii dunia ishawahiwapa. Kwa maana silika YANGU, silika ZANGU hamjui ikiwa mnakana hawa watoto WANGU. Kwa maana wanawaletea matumaini ya wokovu katika MWANANGU YESHUA wanapoMtayarishia njia.


Na kila jicho litaona utukufu wa YEHOVAH ukijaza dunia na kila goti litainama na kila ulimi utakiri kwamba YESHUA ni MWANANGU (Habakuki 2:13-14; Wafilipe 2:9-11)!


Mwisho wa Neno

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page