top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 51 “Jitieni Moyo na Neno LANGU”

Updated: Mar 24, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Julai 25, 2019




Maandiko Husika


Mithali 13:12

Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima.


Matendo 11:13

akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro,


Mithali 11:18

Mtu mwovu hupata mshahara wa udanganyifu; Apandaye haki ana thawabu ya hakika.


Ujumbe wa Kinabii


Kilichotarajiwa kikiahirishwa, kikicheleweshwa hufanya moyo na nafsi kuugua (Mithali 13:12). Hiyo ndiyo sababu MIMI, YESHUA, NImesema mtiane moyo na Neno LANGU la Faraja na Imani. Kuweni na Imani na kila mmoja wenu na mtembee mkono kwa mkono. Tembeeni mkono kwa mkono mkiwa mmefungwa na kamba za milele za upendo ambazo ni Neno LANGU.


Msiache mikono yenu ining’inie kwa ulegevu na unyonge katika udhaifu wa mwili (Waebrania 12:12-13). Simameni katika ROHO WANGU wa UTAKATIFU kwa NGUVU za JINA LANGU kulingana na usafi na utakaso wa DAMU YANGU iliyomwagwa kwa ajili yenu pale Kalivari. Hamwezi kosea mkiNIfuata MIMI, watoto WANGU.


MIMI, YEHOVAH, Nazungumza hivi na kusema, fanyeni uadilifu na vifuani mwenu mtalipwa zawadi nzuri (Mithali 11:18). Msitelekeze Njia za Zamani. Msigeuke kando kutoka kwa Torah YANGU ya Milele. Kitabu CHANGU, Hati Kunjo YANGU haikuumbwa isanye vumbi (“kusanya vumbi” inamaanisha kuwa katika hali ya kutotumika kwa muda mrefu sana. Mara nyingi, watu wanayo Bibilia lakini waniacha kwenye rafu au meza ambapo inasanya vumbi ikiwa haisomwi. YAH Anasema Neno LAKE halikufaa liwe katika hali hiyo lakini lisomwe kila siku.) Ruhusuni ufufuo uingie katika nyumba zenu, uingie katika maisha yenu. Kung’uteni vumbi mbali! Wekeni maisha yenu katika utaratibu.


Someni Neno LANGU. Zingatieni maagizo YANGU na muishi kulingana na imani ambayo mmepewa kwa neema ambayo NImewapa katika MWANANGU YESHUA MASHIAKH pekee wa kweli. Someni Neno LANGU na mpate kuNIjua MIMI, YEHOVAH, BABA yenu ANAYE UPENDO. Tembeeni mkono kwa mkono naMI, YEHOVAH, na NItawainua na Mkono WANGU wa Kulia wa Uadilifu, ukiwaponya na kuwakomboa kutoka kwa woga na rabsha zote za mwili.


Simameni imara. Salieni wakweli kwa Neno LANGU na SItawahi waangusha. MIMI, YEHOVAH, NIko nanyi watoto WANGU hadi mwisho wa nyakati. NItawabeba binafsi na kwa wororo katika nyakati zote. Njooni tu KWANGU na msisikilize uongo za hasatan. yeye ni muongo na baba wa uovu na upotovu wote (Yohana 8:44). Hakuna kitu chochote kizuri ndani yake. hana chochote kizuri cha kuwapa, watoto WANGU.


Msigeukiane kando. Watambue wale wanafanya utengano na kuleta uzushi na muwaepuke (Warumi 16:17). Msiruhusu uchafuzi kuenea, kuingia katika kambi. Epukeni mropoko bure na wa kijinga. Epukeni kabisa ulimi muovu na kemeeni walaghai. Ikaja wasitubu, wakabidhi KWANGU na NItakabiliana na maadui WANGU.


Msisumbuke wala mhangaike katika mawazo yenu, ee watoto WANGU (Walifipe 4:6-7). Mipango mizuri sana NInayo juu yenu, kwa kila mmoja wenu. Kwa hivyo Nataka kuona mkitiana moyo na Neno LANGU zaidi. 1 Wathesalonike 4:18 “Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.”


1 Wathesalonike 5:11 “Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.”


Neno LANGU ni aminifu na kweli. Kuja KWANGU kuko karibuni tu. Msikawie na msichelewe katika kufanya Mapenzi YANGU, kwa maana hamjui wakati BWANA wa nyumba Atarudi (Mathayo 24:45-51). Naja upesi! Naja haraka kwa hivyo ingiene katika utaratibu. Msitamani vitu vya mwili, kwa maana hivi ni kama utajiri wa dunia, kama nyasi za shambani – ziko leo, kesho zimeenda. Msitelekeze utajiri wa kweli ambao ni imani yenu, kwa maana majaribio ya imani yenu ni enye thamani kuliko dhahabu (1 Petro 1:7).



Selah.

11 views

Recent Posts

See All
bottom of page