Unabii 49 ‘YESHUA HAMASHIAKH Asema, “Pokeeni na Muamini DAMU YANGU, Ee Israeli!”’
Updated: Mar 24
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa Julai 14, 2019
Maandiko Husika
Warumi 5:8-11: “Lakini MUNGU Anaudhihirisha upendo WAKE kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, MASHIAKH Alikufa kwa ajili yetu. Basi, kwa kuwa sasa tumehesabiwa haki kwa DAMU YAKE, si zaidi sana tutaokolewa kutoka ghadhabu ya MUNGU kupitia KWAKE! Kwa kuwa kama tulipokuwa adui wa MUNGU tulipatanishwa naYE kwa njia ya kifo cha MWANAWE, si zaidi sana tukiisha kupatanishwa, tutaokolewa kwa uzima WAKE. Lakini zaidi ya hayo, pia tunafurahi katika MUNGU kwa njia ya BWANA wetu YESHUA HAMASHIAKH, ambaYE kupitia KWAKE tumepata upatanisho.”
Kumbukumbu 30:19-20: “Leo ninaziita mbingu na nchi kama mashahidi dhidi yako kwamba nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana. Basi sasa chagueni uzima, ili wewe na watoto wako mpate kuishi, na ili upate kuMpenda YEHOVAH MUNGU wako, uisikilize sauti YAKE na kuambatana naYE. Kwa kuwa YEYE ndiYE uzima wako, na Atakupa wingi wa siku ili upate kuishi katika nchi Aliyoapa kuwapa baba zako Abrahamu, Isaka na Yakobo.
Ujumbe wa Kinabii
Nyinyi nyote katika Israeli, kote dunia hii, ambao mnaombea kuja kwa MASHIAKH kama kwamba Hakuwahikuja mara ya kwanza, mkifikiri Hakuwahikuja mara ya kwanza – tubuni! Nyinyi mnaokana MWANANGU YESHUA HAMASHIAKH – tubuni! Hakuna amani ya kuokoa bila YEYE! Hakuna mkataba wa amani ulioheshimiwa katika macho YANGU, katika macho ya MIMI, YEHOVAH, ila ile iliyozaliwa kupitia Damu YAKE iliyomwagika pale Kalvari; hili Agano Jipya ya Damu ya Maisha YAKE mwenyewe iliyomwagika pale Kalvari. Ni kupitia tu hili Agizo Lililohai lililopeanwa na Mkono WANGU wa Kulia kwamba mtu yeyote anapatanishwa na MIMI, YEHOVAH (Warumi 5:8-11). Kwa maana yule MWANA Anaweka huru yuko huru kweli (Yohana 8:36).
[YESHUA Azungumza] Pokeeni na muamini, ee Israeli. Pokeeni na muamini enyi Makabila Kumi (Efraim). Pokeeni na muamini, ee Yuda. Acheni kuamini katika waandishi wenu, katika mikono yao ya uovu. Kwa maana SIkuwaonya kutahadhari na waandishi na mafarisayo (Luka 20:46-47)? SIkuonya kwamba ikiwa hawaishi Takatifu, [hawaja]takaswa na Damu YANGU iliyomwagika pale Kalvari, kwamba hawangeaminiwa?
Kwa maana wanatafuta kubadilisha nyakati na misimu. Tazameni na mtahadhari. Tazameni na muangalie katika hofu kubwa wanapowauza kwa mzabuni mkubwa zaidi, kwa mpinga-kristo, kwa shetani, babake. Wakati hauko mbali wakati shetani atainuakichwa chake hunde (Ufunuo 12:1-9). Katika njia ambazo hamjui atainuka katikati yenu, ee Yerusalemu. Kwa aibu yenu, mtampokea, kwa maana Watu WANGU wanaangamia kwa kukosa maarifa (Hosea 4:6).
Pateni maarifa ya kuokoa (1 Timotheo 2:4)! Pokeeni YESHUA leo! YEYE ni mlio wa moyo wenu, MKOMBOZI wenu AnaYEokoa. Na ukombozi utakuja! Kama tu kwa hakika MIMI, YEHOVAH MUNGU, Natawala! Vivyo hivyo kwa hakika NItakuokoa ewe Yakobo. Usiogope, NItumainie tu MIMI, YEHOVAH, kupitia MWANANGU wa Pekee YESHUA HAMASHIAKH. NDIMI NILIYE bado Anakungojea, ee Israeli. NDIMI NILIYE Anakusanya yale Makabila Kumi kurudi Israeli, kurudi kwa ardhi ya Yuda.
Watakuwa Mmoja katika Mkono WANGU, Mmoja – Ekhad ndani YANGU (Ezekieli 37:16-23). Ni kupitia tu MASIA Ahadi ZANGU, Baraka ZANGU ni “ndio na amina” kwenu, ee Israeli (2 Wakorintho 1:20). Tu msiogope, mtii tu. Tubuni tu na mkuje kwa MWANGAZA. Njooni KWANGU, ee Israeli, na mNIruhusu NIwaoshe, NIwanyunyize na Damu YANGU inayotakasa iliyomwagika pale Kalvari (Isaya 52:15). Msiruhusu mitazamo mibovu ya historia kugeuza fikra zenu kuhusu NDIMI NILIYE ni nani, kuhusu YESHUA HAMASHIAKH ni nani. Tafuta uhusiano na MIMI. Pata kuNIjua wakati NIngali bado Napatikana.
Kila siku NIkiinuka mapema MIMI, “NDIMI NILIYE” Mkuu, NImekuja kwenu kupitia Manabii WANGU, kupitia Mitume WANGU. NInawaandikia. NInazungumza nanyi. Ombi LANGU kwa ajili yenu, ee Israeli, ni kwamba mje KWANGU na mweke kando tamaduni zenu za wanadamu, chafu na najisi. Matendo yenu yote ni kama matambara najisi mbele ZANGU (Mathayo 11:28-30). Kile ambacho kinawazuia kupokea MWANANGU ni najisi machoni PANGU. NImewaambia msiguse kile kitu najisi, lakini mwe Watakatifu, mtengwe kwa ajili YANGU MIMI, YEHOVAH. Ni kupitia tu Damu ya MWANAKONDOO, Damu ya ALIYEFUFUKA – YESHUA HAMASHIAKH wa Kalvari na Nazareti – ambapo mtu yeyote anaweza kutengwa kwa ajili YANGU.
Ee Israeli, utiifu ni bora kuliko dhabihu (1 Samweli 15:22). NItii na mshike Amri ZANGU. MIMI, YESHUA, SIkuwahi sema Torah itupwe nje, Sheria ya Musa itupiliwe mbali. MIMI NDIYE TORAH ILIYO HAI (Mathayo 5:17-18, Yohana 14:6).
Mshawahi shangaa mbona mnahisi kiu, ee Israeli? Mshawahi shangaa kwa nini ndimi zenu zimekauka hata kama mtu aliyesafiri muda mrefu katika jangwa bila maji, bila riziki? Ni kwa sababu mmekataa MIMI, MAJI YALIYO HAI, Kisima cha UHAI wa Milele. Lakini hili litabadilika, ee Israeli. Utashuka chini, jinyenyekeze ili unywe MAJI YALIYO HAI ambayo yanatiririka kutoka upande WANGU.
MIMI, YESHUA, NIlitoa zaidi sana kwa ajili yako, ee Israeli... Hata maisha YANGU yenyewe NIliyopewa MIMI na MWENYEZI MUNGU (Warumi 6:10). Kwenye huo Msalaba mpweke NIlisulubiwa kwa ajili ya jina lako, kwa ajili ya ukombozi wako. Ni sababu gani nyingine MIMI, MFALME wa Wafalme wote, NItoke kwenye Kiti CHANGU cha Enzi na kuwekwa chini ya aina zote za dhihaka na fedheha? Ni sababu gani nyingine NIteseke matone ya Damu YANGU kutiririka bila kuzuiliwa kutoka kwa mishipa YANGU yenyewe, ee Israeli?
Kwa maana jinsi MUNGU Alivyoupenda ulimwengu hata AkaMtoa MWANAWE wa Pekee ili yeyote aMwaminiYE atapata uhai wa milele, asipokee au awe katika ile laana kuu (Yohana 3:16). Someni Maandiko yenu, ee Israeli. Na ndiyo, Agano Jipya ni Maandiko yenu pia. SIdanganyi.
NIsikieni, ee Israeli. MIMI, YESHUA, SIdanganyi. Mwanadamu anaweza feli na atafeli kwa sababu ya unyonge wa mwili, lakini MIMI, YESHUA, SIwezi. Mkono WANGU wa wokovu ni mkuu kuokoa, usioweza kushindwa na kifo au hata shetani mwenyewe.