Unabii 44 “Israeli, Kuweni Tayari Kutembea Katika Laana Nzima za Kumbukumbu 28 Hadi Mtubu!”
Updated: Mar 24, 2024
Umepewa TORAH KEEPER kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa Juni 21, 2019
Ujumbe wa Kinabii
Jifunzeni Kiebrania, neneni Maandiko YANGU katika Kiebrani! Nguvu zaidi katika [hayo] Maneno. Si, MIMI, YESHUA Husema MIMI ndiye Torah Iliyo Hai?
Oh Israeli, Nawalilia! NIna uchungu wa kuzaa, oh Israeli! MIMI ni YESHUA! MIMI ndiYE MASHIAKH pekee! Mnadhubutu vipi kujaza barabara zenu na mikutano ya kiburi ya mashoga?! Mnadhubutu vipi, oh Israeli?! Kukufuru JINA LANGU! La MIMI, YEHOVAH! Hamtelekezi tu Torah Iishiyo, mnaNItelekeza MIMI, YEHOVAH! Mnakufuru JINA LANGU! Hukumu kwa kweli yaanza katika nyumba ya MIMI YEHOVAH!
Na NIlituma Moshe kwa Farao na kwa Wamisri, na Nawaweka katika kumbukumbu ya Wamisri. Wale wawili waliweza kufanya miujiza pia. Hamjajifunza lolote, oh Israeli? Ishara na maajabu ya uongo! Nyinyi kizao kiovu na kaidi.
Ishara pekee ambayo mtaona ilikuwa ni ya Yona katika tumbo la nyangumi – vivyo hivyo pia MWANA wa YEHOVAH Atakuwa katika tumbo la dunia – kwa mchana 3 na usiku 3, oh Israeli! Na hakika NIlikufa na NIlichukua funguo za kifo, Jahanam, na kaburi na NIkafanya Jahanam yote ijue – NIlizungumza na hasatan na NIkasema, “Damu YANGU inawafunika! shetani ulishindwa!”
Je, hiyo inawatosha, oh Israeli, au NIonyeshe yale mapigo ya Moshe tena?! Hamkujifunza lolote katika lile jangwa! Mlizunguka miaka 40 mkilalamika, mkinong’oneka na kunung’unika! Ndiyo yote NIliyosikia. Maneno yenu yalilia masikioni MWANGU mchana na usiku hadi NIkafanya ardhi ifunguke na kumeza wale wote ambao walinung’unika dhidi YANGU. Vivyo pia ilivyo nanyi, oh Israeli! Wanung’unikaji! Walalamikaji! Ni nini kinachowatosheleza oh Israeli!?
Mnataka MASHIAKH mwengine? Basi, MASHIAKH mwengine mtapata! Hadi mtubu na mfahamu MIMI ndiYE MASHIAKH pekee. MIMI, YESHUA, NIlikuja kuwaokoa, oh Israeli! Na NIna Kondoo na Wanakondoo WANGU katika Israeli.
Bi-Arusi WANGU hata yuko Lebanoni. Bi-Arusi WANGU ameenea kote duniani. Wengine wamo katika nyumba za kujificha; mateso ya serikali za kikomunisti kote duniani. Wakristo wanachinjwa kila mahali. Na wapi maombi kwa ajili ya Israeli?! Kwa ajili ya Watoto WANGU wa kweli, Nawaambia hili – hayatoshi!
Oh Israeli, MIMI, YESHUA, Nasema: hili lazima likome! Wapi toba yenu!? MIMI ndiYE Torah iliyofanywa mwili! Mnazungumza kuhusu Torah, imo katika sinagogi zenu na mnatangaza hata kutoka paa za nyumba, lakini Nawaambia hili – haijaandikwa kwenye mioyo yenu, sio tena.
Kwa maana MIMI, YEHOVAH, Nanena, NIlituma MWANANGU wa Pekee. NIliMtuma kwenu! Na NIlitayarisha Mjumbe WANGU, Yohana Mbatizaji, Yokhanan – ambaye [roho ya] Mafarisayo ilimuua, ilikata kichwa. Ni Manabii wapi ambao hamkuwapiga mawe kabla ya MWANANGU YESHUA? Isaya alikatwa nusu na msumeno! Na kama hamkuwaua kimwili, mliwachinja kiroho! Nyinyi nyoka na vipiribao!
Oh, Nahukumu Mafarisayo! Naja kwa Sinagogi! Na NInavuta ndevu moja kwa moja kutoka kwa uso wenu! MIMI, YEHOVAH, SIfanyi mchezo! NItatuma Manabii WANGU wa kweli kuwaonya. NItatuma Mashahidi WANGU Wawili kwa Ukuta wa Kilio wa Yerusalemu! Watasimama mbele yenu wakitangaza hukumu ZANGU, wakitangaza mapigo! Giza litafagia juu ya dunia kama katika siku za Moshe, lakini baya zaidi! Baya zaidi, oh Israeli! Nawaambia ni baya zaidi! Ni heri mtikisike na mtetemeke na muogope! Kwa maana tazama, Mashahidi WANGU Wawili tayari wako hapa! Na kila mmoja wao atasimama mbele yenu kwenye huo Ukuta wa Kilio ambao mnapenda kulia juu yake!
Kuashiria machozi YANGU, MIMI YEHOVAH, ya ukufuru wenu dhidi YANGU, ya ukataaji wa MWANANGU YESHUA! Kwenye uo huo mchanga mnaosimama na kulia juu yake, Alimwaga Damu YAKE kwa ajili yenu! Damu YAKE imerowesha katika huo mchanga, oh Israeli!
Na MIMI, YESHUA, Nanena! Mavazi, Mavazi YANGU waliNIvua. WaliNIdunga na taji la miiba! Mapigo YANGU ya Moshe yako juu yenu, oh Israeli! Nawaambia hili, tayari NIshakuwa katika hilo tumbo la nyangumi kama vile NIlishawaambia na NImewatuma Wayahudi wa Kimesaniki kwenye hekalu zenu, kwenye sinagogi zenu kuwaonya. Mnawafukuza na kupiga mawe Wajumbe WANGU. Lakini wakati huu, wakati NInatatuma WANGU Wawili Waliotiwa Mafuta, afadhali mwapokee, oh Israeli! Afadhali mtikisike na kutetemeka! Kwa maana wakati huu, SItaonyesha huruma yoyote hadi kuwepo na toba. NItachoma barabara zenu.
Hebu tuzungumze, Netanyahu. MIMI, YESHUA, NItakuwa na kicheko cha mwisho – Nakuahidi. Hakikishiwa kuwa MIMI ni MUNGU ambaye Nashika kila Neno LANGU, kwa maana SIwezi danganya, na MIMI si mwanadamu wa upumbavu! UnaNIdhihaki MIMI Netanyahu kisiri! Familia yako inanidhihaki pia! Wakati unakaribisha mpingakristo, mpingamashiakh! Unaweka mapatano na mikataba na viongozi wa Kipalestina. Unaafikiana! China wanashika kisu nyuma ya migongo yao kwako, oh Israeli. Netanyahu, kwa ajili ya mikataba yako ya amani ya uongo, NInaenda kukuponda! Kwa maana unapeana ardhi ambayo SIjakupa ruhusa ya kufanya hivyo. Sio ardhi yako ya kupeana kwa vyovyote vile! Soma Torah YANGU! Hii ni ardhi YANGU! Na utalipa Netanyahu. MIMI, YEHOVAH, Nasema, weka alama hii siku kwenye kalenda yako Netanyahu. Huku ni kuhesabu kurudi nyuma hadi kwa uangamizaji wako, huku ni kuhesabu kurudi nyuma hadi kufa kwako! NInatuma Mashahidi WANGU Wawili na moto machoni mwao kukuangamiza wewe binafsi.
Na wewe, Israeli na Yerusalemu, isipokuwa mtubu, hadi mfanye hivyo – maana hukumu yaanza kwa Nyumba YANGU, ya MIMI, YEHOVAH – mtajua tu – na hii ni sehemu ya kiapo NIlifanya na Abrahamu – na NIliwaambia katika Torah YANGU: ikiwa mtaNIacha MIMI, mtatembea katika laana za Kumbukumbu 28! Yapaswa mwe mshajifunza kufikia sasa – kila wakati Naona mmeasi dhidi YANGU, kuta zenu zilizingirwa kwa vita. Maana mlitenda uhaini dhidi YANGU na mkavunja kila kiapo, mmevunja kila ahadi mliahidi NDIMI NILIYE. Nawakumbusha mlipokuwa mmesimama mbele YANGU pale kwa mlima na mliposema, “Ndiyo YEHOVAH, tutatii kila sheria! Ndiyo YEHOVAH, nitafuata Sheria ZAKO!” (Kutoka 19:8, Kumbukumbu 5:27).
Na NIkasema, kwa sharti, “Ikiwa mtafuata Sheria ZANGU na, ikiwa mtashika Amri ZANGU na ikiwa mtafuata Maagizo YANGU, yote yatakuwa sawa nanyi, lakini ikiwa hamtafanya (hivyo), tazama hizi ndizo laana mtavaa kama ngozi ya pili...” Na sasa tazama, oh Israeli, maana maadui wako watatoboa kuta zako tena, lakini wakati huu, itakuwa karibu kabisa kwa uangamizaji wako. Lakini SItairuhusu, kwa sababu Najua mwisho wako ni nini. UtakapoNIlilia katika toba, NItakusikia, lakini oh Israeli, hadi wakati huo SIwezi kukusikia.
Hadi wakati huo, mpingamashiakh anakuja kuwadanganya na mtaanguka moja kwa moja katika uchawi wake, moja kwa moja hadi katika sihiri yake. Kama vile buibui anaweka windo lake katika utando wake, vivyo hivyo pia nyinyi mnaanguka katika mitego ya mpingamashiakh. Atajaribu kuwakula mkiwa hai, oh Israeli! Amri moja ataondoa baada ya nyingine, hadi kusiwepo na uhuru wowote kabisa. NIliwaonya! MIMI YEHOVAH NIliwaonya!
Kwa hivyo kuweni tayari oh Israeli, kuweni tayari kutembea katika laana nzima za Kumbukumbu 28. Maana tazama! Naziachilia usiku huu kupitia mdomo wa Moshe.