top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 43 "Furahini Katika BWANA, Bila Kujali Chochote Mnachokabiliana Nacho!”

Updated: Mar 24, 2024


Umepewa Nabii Shema’YAH kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa Juni 21, 2019


Maandiko Husika


1 Wathesalonike 5:16-18 “Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndiyo mapenzi ya ELOHIM kwa ajili yenu katika MASIA YESHUA.”


Ujumbe wa Kinabii


NIsikieni kwa udhahiri, Watoto WANGU, wakati wenu ni mfupi wa kujitayarisha. Kwa maana usafiri wa MAKAVA (MERKAVA) utakuwa hapa katika muda mfupi. Kwa hivyo jitayarisheni na mNIkaribishe na furaha, na sifa, na shukrani, na kicheko, na msisimko!


Kwa maana mnaenda Nyumbani na lazima mpite majaribio yenu. Na mtapita mkiNIkazia MIMI macho na kutekeleza kila kitu NInachofunza. Na hasa kabisa, kuweka mtazamo mzuri, haijalishi mnachokabiliana nacho. Lakini kweli Watoto WANGU, muda ni mfupi sana, wakati uko karibu sana na usafiri wa MAKAVA uwakujie. Je, mnaweza hisi (huu) msisimko?


Vyema! Maana itakuwa kwenye nyuso zenu kila siku! Amini tu. NIonyesheni kwamba mnaamini kwa furaha yenu ndani YANGU, mkishangilia ndani YANGU. Kupeana shukrani, kutabasamu, kucheka, kucheza lakini kwa kipimo; katika usawa. Kwa maana mna vitu vya kufanya. Lakini mnajua kile NInamaanisha katika hilo, kwamba hali yafaa ibadilike – yapaswa iwe ya kushangilia.


NInafurahishwa sana nanyi Watoto WANGU, kwa yote ambayo mmetoa dhabihu kwa ajili YANGU. Kwa uchungu wote mmepitia kwa ajili YANGU. Kwa kuwa mnaNIkumbuka katika kila kitu mnafanya, na hii sehemu inafika tamati. Kwa maana mtapokea miili mipya ambayo hii dunia haitawahi wagusa tena, watia doa tena (Filemoni 3:21). Na jihadhari dunia wakati mtarudi (Watoto wa YAH), itakuwa jambo la kuogofya kwa wale ambao wamewachongea na wale ambao wameitwa maadui.


Kwa maana hukumu imekuja kwenye Nyumba ya BWANA YEHOVAH na ni wangapi kwa kweli wamesikiza? Na hiyo ndiyo maana wengi sana wamepofushwa! Kwa maana hukumu imekuja juu yao katika njia mpya kwa kuishi katika dhambi! Na hukumu haiji tu kwao (YAH Azungumzia kuhusu wengine katika nyumba ya BWANA), lakini pia kwa dunia. Maana kwa kweli ni jambo la kuogofya kuanguka katika mikono ya MUNGU AISHIYE (1 Petro 4:17-18, Waebrania 10:31).


Na nyinyi ndio mikono YANGU. Nyinyi ndio vidole VYANGU. Nyinyi ndio kidole cha BWANA YEHOVAH. Na NItawatumia kama hivyo [vidole] kuNIgusia hii dunia na moto utaenda kuteketeza yote yaliyotakataka (Luka 11:20). Na mtachoma midomo yao na moto wa Neno LANGU. Na wakaidi na waliorudi nyuma watachomwa (Ufunuo 11:5). Lakini wale watakaoNIogopa, NItahurumia, NItaokoa. Wanaposikia huu ujumbe wa toba na mnatikisa huu ulimwengu! Na mambo ya kuogofya ambayo wataona, na watajua kwamba kuna MUNGU YEHOVAH mmoja pekee! Na hakuna ambaye atajua kuNIkana! Kwamba NDIMI NILIYE, watachagua upande tu.


Na wale ambao watatubu ni watoto WANGU na ule upande mwingine ni maadui. Na kwa kweli mtaNIgusia huu ulimwengu katika njia ambazo haijajulikana mbeleni. Hata ikiwa ungechukua kila huduma duniani, na kuziunganisha kuwa moja. Na inaenda kuwa nyinyi wawili (YAH Azungumza na wana WAKE wawili), mtafikia Afrika ambayo itakuwa ni bara la mwangaza mzima NInapotembelea maadui WANGU na kuondoa nira na utumwa ambao walikuwa wameweka kwenye shingo za watu WANGU ambao hawakujua ni watu WANGU.


Ulaya itafikiwa katika njia mpya. Oh, lakini watateseka kwa maana wamekuwa wakiishi katika anasa.


Israeli itaNIsikia kwa sauti na kwa uwazi. Maana NItawatembelea kibinafsi na MwanaNGU. Kwa hivyo kuweni tayari kwa mateso ambayo yatakuja njia yenu. Kwa maana itakuwa katili, maana wale ambao wanafikiria watakuwa wanafanyia huduma MUNGU watawatendea mabaya kabisa (Yohana 16:2). Lakini hakuna atakayeweza wadhuru. Na kumbukeni, inawarudia kwenye vichwa vyao wenyewe (Zaburi 7:16).


Kwa maana mtaona Edeni tena. Na mnapomachi, na wale watakaowapokea watachanua na kusitawi na kufanikiwa na kuwa kama Bustani ya Edeni. Na wale ambao hawata[wapokea] watakuwa kama nchi jangwa iliyounguza na kuchomeka (Yoeli 2:3).


Matumaini watoto WANGU. Maana daima mnaleta matumaini mnapoNIwakilisha. Kwa maana MIMI ndiYE Tumaini Lililobarikiwa na mjue [kwamba] hata ingawa mnaleta hukumu kwa huu ulimwengu, sikuzote ni wao (watu duniani) ambao huNIkataa (Tito 2:13), Yohana 3:19). Mnatoa tumaini la wokovu. Ujumbe wa mwisho wa tubu au uangamie! Na katika huo ujumbe wa mwisho wa toba kuna tumaini la wokovu ili nafsi zao ziweze kuokolewa, hata kama kila kitu kingine kitaenda vibaya. Hakuna yeyote anapaswa kuachwa bila matumaini, kwa maana SIwaachi bila matumaini. Lakini tena, iko juu yao kuamini. Kwa maana kila kiumbe kitajaribiwa – jaribiwa katika maarifa ya ukweli. Kama wanaweza NIona, kwa maana NInaonekana kwa wazi katika uumbaji wote.


Kwa ajili ya huu ujumbe wa mwisho, Nawapenda watoto WANGU wapendwa. NIliwafia. NIpendeni kwa mapenzi makali. Kuweni wenye hisia kali kwa ajili YANGU na pamoja naMI. Kwa maana Naja upesi. Na Tunaenda kwa chakula cha jioni cha Ndoa ya MWANAKONDOO na BiArusi WAKE ang'aae. Na mtaolewa KWANGU MIMI. Nawahitaji mwe BiArusi WANGU aliye na mapenzi makali, mkiNItaka sana kwa hofu kubwa. Kwa maana ndivyo jinsi Navyowapenda. Kwa maana hata SIwezi JIzuia kwa kuja kwenu! Na hili daima litakuwa kwa maana Nawapenda milele. Upendo WANGU kwenu ni milele. Na wenu pia ni vivyo hivyo. Kwa hivyo cha msingi, msiwahi poteza ufahamu wa hii picha. Kwa maana ni huo upendo ambao unazima moto wa Jahanam, nguvu za Jahanam, za kaburi, wivu wa kaburi, wa She'ol (Wimbo 8:5-7). Na ndiyo maana mnashinda kila jaribio, kila uchungu. Mnapita [pamoja] na MIMI – kwa ajili YANGU!


BiArusi WANGU wa uchu. Nakushukuru kwa kuNIfuata haswa, haijalishi ni mara ngapi uling'ang'ana au ulijikwaa au kuanguka au haukuhitimu katika macho yako, haukuwahi wachilia. UliNIamini, uliNItumainia, na uliNIpenda kwa uaminifu wakati wengi sana walirudi nyuma. Na haswa katika saa zako za giza zaidi. Hili liliNIpendeza sana kwamba ulishikilia. Kwamba uliNIpenda hadi mwisho na kila kitu kilichomo ndani yako.

Haijalishi uchungu, haijalishi maneno ambayo yalisemwa au kuzungumzwa dhidi yako. Na hili liliNIpendeza. Maana kama vile MIMI, uliifanya kwa ajili ya upendo, ulilifanya katika upendo, na uliNIfuata kwa uaminifu sana – ingawa, mara nyingi sana ilikuwa ni kama kondoo aliyepelekwa kichinjoni (Warumi 8:36). Kwa maana ulichinjwa kwenye hayo madhabahu kwa ajili YANGU. Manukato yanayonukia kwenye mapua YANGU, MIMI, YEHOVAH (2 Wakorintho 2:14-16). Ulipolaza chini maisha yako tenana tena. Na hivyo, yatalazwa chini tena. Kwa maana wewe ni WANGU, na MIMI wako. MIMI ni wako! Na milele pamoja naMI utaishi. Nawapenda sana na maneno hayawezi dhibiti maarifa wala ufahamu wala taarifa ya jinsi ilivyo kweli (Waefeso 3:19). Lakini mtaona na macho yenu wenyewe tukicheza densi pamoja katika huu mwaka wenu wa jubilii! Kwa hivyo furahini Watoto WANGU, na msiwe na kukosa furaha wala kushangilia. Na bila chochote kutia shaka.


Watoto WANGU wote watakuwa na MIMI (Yohana 10:28-29). Hivyo, Nawapenda. Kumalizia, YESHUA wenu Mpenzi wa nafsi yenu.


Mwisho wa Neno

8 views

Recent Posts

See All
bottom of page