Unabii 14 “Sikieni Neno la MELEKH TSEDEK, Enyi Watu, na Muamini!”
Updated: Apr 14, 2024
Umepewa TORAH KEEPER kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 21 Februari, 2019
Maandiko Husika
2 Nyakati 36:16
"Lakini walidhihaki Wajumbe wa ELOHIM wakayadharau Maneno YAKE na kuwacheka Manabii WAKE mpaka ghadhabu ya YEHOVAH ikawa kubwa dhidi ya Watu WAKE na hakukuwa na namna ya kuituliza."
Mwanzo 14:17-24
“Abramu aliporudi baada ya kumshinda Mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika Bonde la Shawe (yaani Bonde la Mfalme).
18 Ndipo MELEKH TSEDEK, mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa KUHANI wa ELOHIM ALIYE JUU SANA. Naye akambariki Abramu, akisema, Abarikiwe Abramu na ELOHIM ALIYE JUU SANA, Muumba wa Mbingu na nchi. Abarikiwe ELOHIM ALIYE JUU SANA, ambaYE Amewaweka adui zako mkononi mwako. Ndipo Abramu akampa MELEKH TSEDEK sehemu ya kumi ya kila kitu. Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe hao watu na hizo mali uchukue wewe mwenyewe. Lakini Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa YEHOVAH, ELOHIM ALIYE JUU SANA, Muumba wa Mbingu na dunia, na nimeapa kwamba sitapokea kitu chochote kilicho chako, hata kama ni uzi au gidamu ya kiatu, ili kamwe usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu. Sitapokea chochote, ila kile tu watu wangu walichokula na sehemu ambayo ni fungu la watu waliokwenda pamoja nami, ambao ni Aneri, Eshkoli na Mamre. Wao na wapewe fungu lao.”
Waebrania 5:5-6
“Pia MASIA hakuJItwalia utukufu YEYE MWENYEWE wa kuwa KUHANI MKUU, bali Alitukuza YULE AliYEmwambia, “WEWE ni MWANANGU; leo MIMI NImekuzaa.” (Zaburi 2:7) Pia mahali pengine Asema, “WEWE ni KUHANI milele, kwa utaratibu wa MELEKH TSEDEK.” (Zaburi 110:4)”
Yeremia 31:31-36
“Siku zinakuja,’ Asema YEHOVAH, ‘NItakapofanya Agano Jipya na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda. Halitafanana na agano NIlilofanya na baba zao wakati NIlipowashika mkono kuwaongoza watoke Misri, kwa sababu walivunja agano LANGU, ijapokuwa NIlikuwa Mume kwao,’ Asema YEHOVAH. ‘Hili ndilo Agano NItakalofanya na nyumba ya Israeli baada ya siku zile,’ Asema YEHOVAH. ‘NItaweka Toraha YANGU katika nia zao, na kuiandika mioyoni mwao. Nitakuwa ELOHIM wao, nao watakuwa Watu WANGU. Mtu hatamfundisha tena jirani yake, wala mtu kumfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue YEHOVAH,’ kwa sababu wote wataNIjua MIMI, tangu aliye mdogo kabisa kwao, hadi aliye mkuu sana,’ Asema YEHOVAH. ‘Kwa sababu NItasamehe uovu wao, wala Sitazikumbuka dhambi zao tena.’ Hili ndilo Asemalo YEHOVAH, YEYE Aliyeweka jua liwake mchana, YEYE AnaYEamuru mwezi na nyota kungʼaa usiku, YEYE Aichafuaye bahari ili mawimbi yake yangurume; YEHOVAH wa Majeshi ndilo JINA LAKE. Ikiwa amri hizi zitaondoka machoni PANGU,’ Asema YEHOVAH, ‘ndipo uzao wa Israeli watakoma kuwa taifa mbele YANGU daima.”
Ujumbe wa Kinabii
Sikieni Neno la MELEKH TSEDEK (Melkisedeki) enyi watu wote! Ee, amini, amini, amini mko ndani ya Utaratibu WANGU! Amini na mpokee!
Ee, jinsi nyinyi ni spesheli KWANGU MIMI! MIMI ndiYE Utaratibu! MIMI ndiYE TAWI ADILI lililouawa! MIMI ni MELEKH TSEDEK! YESHUA ni JINA LANGU! Nawapenda vipenzi VYANGU! NIko nanyi!
Utaratibu WANGU, ingia katika safu! Ingia chini ya ukuhani WANGU mzima. Je wafanyaje hili? UnaNIpokea kikamilifu moyoni mwako.
Jinsi gani unaweza sema, unastahi NDIMI NILIYE ikiwa hauNIjui kama NDIMI NILIYE? MELEKH TSEDEK ni JINA LANGU! UnaNIkataa MIMI YESHUA ukiMkataa MELEKH TSEDEK! Wengi hawatatubu. Wengine watatubu. Ee njooni KWANGU, ee NIsikie, oh Israeli! Usifuate njia za wapagani lakini tumainia NDIMI NILIYE! MIMI NIKO katika Torah! MIMI NDIMI NILIYE na sina mwanzo wala mwisho. MIMI NDIMI NILIYE!
Ee jinsi Navyowapenda, ee Watoto WANGU. Ee, huruma! NItakuwa na huruma na NItaokoa wale ambao ni baraka kwenu. NItalaani wale ambao wamejaribu kuwaangamiza!
MIMI ni MELEKH TSEDEK! NIogope MIMI! Ni jambo la kuogofyya kuanguka katika mikono YANGU! Ni jambo la kutisha kugusa WANGU Waliotiwa Mafuta na kuumiza Manabii WANGU. Ni heri muende mkikimbia, ee maadui WANGU! Ee ogopeni NDIMI NILIYE Mkuu! NIogopeni MIMI, Watoto WANGU, mnapokumbuka MIMI ni NANI! Napenda mnapoNIogopa na Natamani heshima yenu.
Ukuhani ndio utaratibu. Wale ambao hawashiki utaratibu WANGU hawatakubali hii sehemu ya NDIMI NILIYE!
Hamjui enyi dunia kwamba MIMI, YESHUA, Najua kila mmoja wenu? Mioyo imejaa dhambi! Mioyo yenu imejaa marundo ya samadi na unajisi wa uvundo wa kinyegere! MsiNIsifu enyi makanisa kwa maana Nasema NIondokeeni! Mengi ni maonyesho ya masingizio tu.
Sikia, ee Israeli! YEHOVAH ECHAD, YESHUA HAMASHIAKH, RUAKH HAKODESH! SISI UTATU MTAKATIFU ni MMOJA!
Ee, NIpiganieni! MIMI NDIYE utaratibu! Bakini katika utaratibu! Pokeeni utaratibu watoto WANGU wapendwa! MIMI NDIYE utaratibu. Najua utaratibu! Jifunzeni KWANGU! Jifunzeni kuhusu utaratibu! Ee jinsi yalivyo mazuri ajabu na kweli Maneno YANGU!
NIulize NIwasaidie kukumbuka. Nawaambieni wachaguliwa WANGU, jifunzeni KWANGU na ndiyo, Watoto WANGU, shikeni Amri ZANGU! Ee jinsi njia ZANGU zilivyo kuu na za kustaajabisha!
Ee, kuu ni Huruma YANGU! Amri ZANGU ni safi, takatifu, na kweli, kwa hivyo zishikeni enyi Watoto Wadogo! NIheshimu MIMI, NDIMI NILIYE Mkuu! Stahi na ogopa—kwa maana hili ndio Lango la kuelekea kwa Biarusi Mkuu. Hii ndiyo njia ya kuenda kwa Ukuhani WANGU. Ee heshimu NDIMI NILIYE! Tulia na mNIngojee!
Ee, NInaamsha ghadhabu YANGU kuu juu ya dunia. NInafanya hili katika huruma! Kwa maana kama haingekuwa ni Damu ya YESHUA na Biarusi WANGU nyinyi nyote mngekuwa mmeangamizwa! Kila mmoja wenu anahitaji mwenzake. Ee shikeni Neno LANGU kwa upendo mkubwa! Shikilia Neno LANGU. NIfurahisheni! Kaeni katika utaratibu. Utaratibu, utaratibu, utaratibu! Utaratibu WANGU ni wa thamani na Najua mioyo yenu yote. Mioyo yenu yote hata imehifadhiwa katika utaratibu WANGU. Mioyo yenu moja kwa moja yote imepangika kwa mstari katika utaratibu.
Jinsi NDIMI NILIYE Alivyo Mkuu! Ikiwa tu mngeNIona. Msipoteze imani mkiona dhoruba! Msipoteze fokasi mnapoona wale kando yenu wakishikwa na hofu na NInarejelea kuhusu dunia. Nawajua ninyi na NInajua majina ya nani yameandikwa katika Kitabu cha Uhai cha MWANAKONDOO. Nyinyi Saba mko pale, wakubwa na wadogo. Ee jinsi mlivyo warembo! Ee Biarusi WANGU! Jinsi navyongoja kucheza dansi nanyi! Jinsi navyongoja kuwa mmoja nanyi! Ee NItunzeni kwa upendo!
Thamini [kwa upendo] Neno LANGU na mtathamini NDIMI NILIYE! Thamini sana Neno LANGU! Onea shauku Neno LANGU! Shikeni Amri ZANGU! Kuweni watakatifu! NIwakilisheni vizuri. Sasa NIkumbatieni, nyinyi nyote Watoto WANGU, kamwe kuliko mbeleni! MIMI NDIMI NILIYE! MIMI ni Mkweli! NIthamini MIMI na Utaratibu WANGU na NItawabariki! NItawastahis!
Endeleeni kuNIstahi sana, kila asubuhi. Inuka! Amka, amka, ee! Tulieni na mjue kwamba MIMI ni ELOHIM! SIwezi ngoja kuwaona enyi watu WANGU! MIMI ni MELEKH TSEDEK na MIMI ni YESHUA, Nangojea kila mmoja wenu!
Siri NItafunua. NItawapa binafsi zawadi na lulu na vito vyenye thamani kutoka kwa KITI CHANGU CHA ENZI. Mtajua furaha! NInawatayarisha kwa jili ya siku za huzuni kwamba mtafurahia kabla ya maangamizi kuja. Sasa furahieni watoto WANGU! Furahieni watoto WANGU wachanga! SISI sote ni MMOJA, kwa hivyo bakini katika upendo. NInapobariki mmoja, NDIMI NILIYE Awabariki pia. Oneni nyinyi nyote kama mmoja ndani YANGU. NInawapa macho kuona. NInawapa macho mapya ya kiroho ya utakatifu na utakato. Mtayapokea?
Wanatayarisha madhabahu mbele YANGU MIMI NDIMI NILIYE Mkuu kila wakati kuliko muda wowote katika historia! Ee, kuweni katika amani Watoto WANGU Wadogo! Msiruhusu watesaji kuja kuwatesa katika njia yoyote!
Msijitese, lakini furahieni! Ee, furahieni Naisema tena, furahieni!!! NDIMI NILIYE Anakujia Biarusi WANGU Mkuu na tena, Nasema, furahieni! NDIMI NILIYE YUKO pale! NDIMI NILIYE Asema furahieni! TUnatuma Majeshi ya Mbinguni, wako nanyi. Wanajua jinsi ya kuwasaidia. Pokea usaidizi wao! Pokea usaidizi wao, ee Watoto! Kwa maana nyinyi ni Wapenzi WANGU na Biarusi WANGU! Ee jinsi Navyowathamini na Navyowapenda!
Maana Utukufu WANGU utasogelea karibu nanyi! NDIMI NILIYE Anatayarishia Biarusi WANGU Mkuu kuja nyumbani! NDIMI NILIYE Anafurahia! Kwa hivyo furahieni, furahieni Nahitaji tena kusema – furahieni! Shikeni Amri ZANGU. Shikeni Sheria YANGU ya maisha katika mikono yenu, katika akili zenu, ifungeni kwenye shingo yenu na iandikeni kwenye vibao vya moyo wenu. Kariri! Kariri Torah YANGU.
Pumzikeni tu ndani YANGU na furahieni ee Watoto WANGU wa thamani! Heshimu ELOHIM Mkuu! NIheshimu MIMI! Fanya mapenzi YANGU! MIMI ndiYE utaratibu, kwa hivyo tembea humo! Tembeeni na msizurure kulia au kushoto.
Huu ndio ufunguo na kiini cha Torah. Hili limo ndani YANGU. Huu ni moyo WANGU. Fokasi, fokasi, fokasi, baki ndani YANGU. Kwa maana MIMi ni Torah! Mbona hamwezi ona hilo?! (Wale wanaokataa Torah) Mbona, oh mbona, oh?! Mbona, mbona, ee TUnawalilia nyinyi!
Hati-kunjo! Fungueni hati-kunjo na NItafungua macho yenu! Mtaona Mbinguni yote ambayo NImewahifadhia! Kariri Shema YANGU! Kariri Maneno YANGU! Kariri!
Nataka kumaliza Neno hili na Waridi. Kwa maana Waridi LANGU linawakilisha Upendo WANGU, Upendo WANGU kwenu usioisha! Ee NIfurahisheni! Fanyeni NIjivunie Watoto! Kwa maana NInawaambia sasa, furahieni ndani YANGU!
(Sauti ya YEHOVAH ilipoanza kuwa nyororo zaidi na zaidi, nilikuwa nasikia)
Utaratibu, utaratibu, utaratibu.
Hii ni Asema YESHUA HAMASHIAKH na MELEKH TSEDEK, ambao ni MMOJA.