top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 12 “Njooni, Tujadiliane Pamoja!”

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa TORAH KEEPER kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 7 Februari, 2019

Ujumbe wa Kinabii


YESHUA Asema,


Watu, angukeni kwenye nyuso zenu. Heshimu sana, Heshimu sana, Heshimu sana! NIKO HAPA.


Waambie, dunia inatetemeka kwa ghadhabu YANGU maana NImejawa na hasira YANGU. Dunia inadhihaki “Passion of the Christ” (Mateso ya Kristo ambayo ni filamu)! Hawajui mateso watakayostahimili kwa ajili ya hili. Wanadhihaki Damu YANGU pale Kalvari iliyomwagika kwa ajili yao kwenye mchanga wa Yerusalemu. Msiwe kama wapagani, waonye! Kwa maana ghadhabu za BABA ziko mwisho na Mizeituni YANGU 2 itainuka!


Kwanza usiku lazima uje halafu asubuhi. Mwaweza sikia ndege wakiimba? Ee halafu mbona mnanung’unika ee dunia!? MIMI YESHUA Nalia! Nalia kwa maana Pendo LANGU la shauku linakanyagwa na kutupwa katika moto wa uangamizaji wa nafsi na wengi! Nawaona wakiNIdhihaki! Je, mnafikiri mtakwepa ee wapagani wa hii dunia?! Ee, sikieni na mtilie maanani huyu Nabii! Kwa maana ghadhabu YANGU inachemka moto zaidi kuliko jua! Mnathubutu vipi! Ndoa ya jinsia moja kama tauni inafanya wengi sasa kutenda dhambi kwa kufanya dhambi ya kuamua ndoa ya jinsia moja na kukubalika kwake. Hamjui imeandikwa katika Sheria ya Torah, hili ni chukizo KWANGU MIMI YEHOVAH, YESHUA, IMMA GLORIA?! Dhihaka ya yote yaliyoTakatifu!

Ee Nakupenda! Na sasa andika kile Nanena, Neno lisizidi wala Neno lisipungue, kwa hivyo usiogope kile wapagani wanasema! Maana NItaweka hofu katika mioyo ya wanadamu wakati NItaweka mapigo YANGU juu yao kwa kuja dhidi ya Mzeituni WANGU, Matawi YANGU kwenye kinara CHANGU cha Mshumaa.


Jinsi gani bado hamuelewi? MIMI ndiYE Torah inayoishi! MIMI ni NENO lililofanywa mwili na NIliwafia, ee dunia, ili mungeweza kufurahia BABA YANGU na MIMI na MAMA YANGU milele daima!


Watakatifu WANGU wote sikizeni! Gabri’El anapuliza pembe yake na sauti YANGU inapigishwa king’ora katika ulimwengu! Mkisikiliza, mtasikia. NIulize (Niwafanye) msikie. NIko hapa. NIko karibu zaidi kuliko pumzi yenu ya karibu kabisa. NIko nanyi na Nampulizia mabusu Biarusi WANGU! MIMI ni MPENZI wako na MIMI ni BWANA ARUSI wako, JAMAA wako wa Kiume MKOMBOZI (Kinsman Redeemer) na NInastahili!



Mwisho wa Neno

22 views

Recent Posts

See All
bottom of page