top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 11 “Ee Yerusalemu, NIrudie, Asema BWANA MUNGU Wako!”

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa Nabii Natan’El kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 7 Februari, 2019

Maandiko Husika


Isaya 3:8-9: “Yerusalemu inapepesuka, Yuda inaanguka; maneno yao na matendo yao ni kinyume na YEHOVAH, wakiudharau Uwepo WAKE uliotukuka. Nyuso zao zinavyoonekana zinashuhudia dhidi yao, hujivunia dhambi yao kama Sodoma, wala hawaifichi. Ole wao! Wamejiletea maafa juu yao wenyewe.”

Mathayo 23:37-39 “Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauao Manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwako! Mara ngapi NImetamani kuwasanya watoto wako pamoja, kama vile ndege akusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hukutaka! Tazama nyumba yenu imeachwa ukiwa. Kwa maana Namwambia, hamtaNIona tena tangu sasa mpaka mtakaposema, ‘Amebarikiwa YEYE Ajaye kwa JINA la YEHOVAH.”


Ujumbe wa Kinabii


Ee Yerusalemu, jinsi ulistahili kuwa sifa katika dunia nzima (Zaburi 62:7)! Ee Yerusalemu, Ee Yerusalemu! Jinsi ulivyogeuka aliyenajisiwa!


Kipenzi CHANGU, njiwa WANGU, umeenda wapi? NIlikutafuta kwenye Mwanya wa MWAMBA lakini ilikuwa bure. Kutoka kwenye kiota chako, ulipuruka, ukiacha mayai NIlikuwa NImekupa.


Ee yu wapi mpendwa WANGU na kwa mwisho upi ameenda? NIlitafuta na kutafuta hadi NIkapata mpendwa WANGU akilowa katika dhambi na kunajisiwa na tope la udongo. Ni nini hili kwamba anaenda dhidi ya asili yenyewe? Jinsi gani njiwa, kipenzi cha macho YANGU anaweza kaa kwenye majivu, katika taka na tope la unajisi? Maana NIlikuwa NImempamba katika kitani bora cheupe – alama ya utakato wake (Ezekieli 16:9-14).


Lakini sasa amenajisiwa. Sasa ni mchafu (Ezekieli 16:15). NItamfanyia nini yeye ambaye mara moja alikuwa mrembo kutazama, mrembo machoni MWANGU? Mbona ajaribu mwindaji na mtego wake, kuenda pale upako haulekezi? Atajifunza lini, maana amerudi – nyuma?


Kiburi kimekuwa joho lake na chuki imejaza macho yake. Oh giza lililomo ndani! Kwa kweli ni mbaya mno kutazama. Lakini NItamtakasa wakati atarudi, wakati atatubu na kuita katika JINA LANGU, YESHUA HAMASHIAKH (Mathayo 23:37-39). Halafu Tutakuwa Wapenzi mara moja tena, Tukitembea mkono kwa mkono. Ataomboleza na atalia lakini hii lazima iwe ili asiwahi wacha kiota, ili asitembee katika kutotii (Zekaraya 12:10-11). Selah.


Mwisho wa Neno

4 views

Recent Posts

See All
bottom of page