top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 84“NInakuita Ee Israeli! NIsikie!”

Updated: Mar 23, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa SIfa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 30 Aprili, 2020


Maandiko Husika


Ezekieli 36:23-25

23 NaMI NItalitakasa JINA LANGU KUU, lililotiwa unajisi katika mataifa, mlilolitia unajisi kati yao; nao mataifa watajua ya kuwa MIMI NDIMI YEHOVAH,” Asema BWANA YEHOVAH, “NItakapotakaswa kati yenu mbele ya macho yao.

24 Maana NItawatwaa kati ya mataifa, naMI NItawakusanya na kuwatoa katika nchi zote, na kuwarudisha katika nchi yenu wenyewe.

25 NaMI NItawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; NItawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote.


Yeremia 6:16

YEHOVAH Asema hivi: Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, Iko wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, “Hatutakwenda katika njia hiyo.”


Ujumbe wa Kinabii


Ee NIsikizeni, ee Israeli! Nawapenda. NImewapenda. Na upendo wa milele NImewavuta KWANGU MIMI (Yeremia 31:3). NIsikizeni na msijue woga wowote. Epukeni njia na mipango ya shetani kwa kutubu dhambi zenu. Nyinyi si watakatifu KWANGU, ee Israeli. Kwa maana mmeruhusu kila aina ya chukizo katika nchi yenu.


Je, mnafikiri hili linaNIpendeza kuona umalaya, kuona uavyaji mimba ukienea pote?! NInaruhusu kile NInaruhusu kuona pale moyo wenu upo. Mnajua pale mlipo, ee Israeli? Mko mbali na MIMI (Isaya 29:13-14, Mathayo 15:7-9). Geukeni nyuma na mkimbilie mikono ya upendo ya MASIA wenu YESHUA. Njoni KWANGU na muache NIwaoshe uovu wenu wote. Uvundo wa dhambi zenu umefika Mbinguni.


Ee Israeli, je hamuoni umbali wa mlionguka? Njoni KWANGU na acheni NIwaoshe safi (Ezekieli 36:22-36). Upotovu umejaza macho yenu, umejaza mitaa yenu. Je, hamfahamu jinsi hili linavyoNIkasirisha? Mnasoma Torah, lakini je, mnafahamu mnachosoma? Mwawezaje soma “usizini” na kufumba na kufumbua tazama mwanamke kwa tamaa? Nawauliza ee Israeli, mko wapi? Ee israeli, vitu haviko vinavyoonekana! Amkeni kuNIhusu sasa kabla kuwe kumechelewa kabisa! NInawaita kupitia zama, lakini je mwaNIsikia?


NIko tayari kuguruma na hakuna taifa moja ambalo halitaathirika. NItaangusha nguzo za juu kabisa. NItaharibu hekalu za ibada za kukufuru. Kimbieni vinyago vyote na hata sura ya dhambi (1 Wathesalonike 5:22). Telekezeni uabudu sanamu au mhukumiwe na sanamu zenu (Walawi 26:30). Naja kuleta moto, kuleta upanga WANGU (Mathayo 10:34). MIMI ndiYE YULE MWANAKONDOO AliYEuawa, lakini pia MIMI ndiYE SIMBA AngurumaYE kutoka kabila la Yuda.


NIlienda kwenye kaburi katika unyenyekevu, katika unyonge na NIliinuka mshindi, kwa maana hakuna dhambi ilipatikana ndani YANGU (2 Wakorintho 13:4). Kila kitu BABA YANGU AliNIuliza kufanya, NIlifanya na upendo usiosemeka na uliojawa na utukufu. SIkuja kufanya mapenzi YANGU, bali mapenzi ya BABA YANGU wa MBINGUNI (Yohana 6:38). Na ikiwa NIngefanya mapenzi YANGU, ee Israeli, basi hamngekuwa na wokovu.


Lakini NIlifanya mapenzi YANGU kuwa mapenzi ya BABA YANGU (Mathayo 26:36-42). SIkusikiza mwili. Kwa ajili ya furaha iliyokuwa mbele YANGU, NIlistahimili msalaba (Waebrania 12:2). Sasa NImeketi juu zaidi ya mamlaka na himaya zote, juu ya ufalme [wote] na viti vya enzi vyote (Waefeso 1:20-23). NIisikizeni ee Israeli, kwa maana NInayo manufaa yenu mazuri kabisa moyoni. NIrudieni na NItawarudia. NIsikizeni na NItawasikiza. MIMI, YESHUA, Nawaita. Mtainamisha goti.


NIsikieni ee Israeli, kwa maana Nawapenda na upendo wa milele. Kwa taifa lipi NImeonyesha subira nyingi zaidi? NImewapa maaguzi ya MUNGU na mmefanya nini nayo (Warumi 3:1-2)? Bado mnatukana manabii hadi leo hii mnapofasiri maandishi yao kulingana na mwili wenu. NInawawajibisha kwa ajili ya hili! NIliwaambia msiguse NIliowatia mafuta na msidhuru manabii WANGU (Zaburi 105:15)! Ni nini kisingizio chenu?


Msilaumu manabii wenu, kwa maana NIliambia kila mmoja wenu kusoma na kujionyesha mmekubalika (2 Timotheo 2:15). Je, unagawa Neno la MUNGU visahihi? NItawajibisha marabii kwa kusema wongo, lakini wapi wajibu wenu? Wote lazima watimize wokovu wao wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Wapi kicho, ee Israeli? Wapi heshima? Je, SIstahili? Je, MIMI si MUNGU wenu, ELOHIM wenu tsevaot (MUNGU wa majeshi)?


Kwa hivyo NIheshimu na NItawaheshimu. Someni njia za zamani na mNIrudie (Yeremia 6:16). Toeni nta toka kwa masikio yenu, kwa maana nyinyi ni wazito wa kusikia, wazito katika moyo. Nyinyi ni vuguvugu. Mnakariri Torah, lakini wapi toba? MnaNIkataa, ee Israeli, MIMI, YESHUA. Ni nini kisingizio chenu?


NIsomeni MIMI. Jipateni ndani YANGU, ee Israeli. Someni Agano Jipya wanavyokiita. Tafiti MIMI ni nani. NImeandikwa kuhusu katika Torah na Manabii pia Brit Khadasha (Yohana 5:39). Soma na ujionyeshe umekubalika. Nawapenda, ee Israeli, na Nawaita. NIsikieni.

Mwisho wa Neno.

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page