Unabii 82 “MIMI, YESHUA, Nawapeleka Kwenye Vimo Vipya vya Utukufu!”
Updated: Mar 23, 2024
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umepokewa 28 Aprili, 2020
Maandiko Husika
Wagalatia 6:8
Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa ROHO, katika ROHO atavuna uzima wa milele.
Yohana 14:23-24
23 YESHUA Akajibu, Akamwambia, “Mtu akiNIpenda, atalishika neno LANGU; na BABA YANGU Atampenda; naSI TUtakuja kwake, na kufanya makao kwake.
24 Mtu asiyeNIpenda, yeye hayashiki maneno YANGU; nalo neno mnalolisikia silo LANGU, ila ni LAKE BABA AliyeNItuma.
Ujumbe wa Kinabii
NItazame MIMi, mwanaNGU, na ujue utukufu wa ukuu WANGU. NInawapeleka kwenye mwinuko wa juu zaidi wa imani yenu. Nawapeleka kwenye upeo mpya wa utukufu! Jilisheni MIMI. NIjueni na mjue BABA (Yohana 14:7-11). Nawasanya KWANGU ili mpatanishwe na BABA katika njia zote (Wakolosai 1:19-23).
NItumainie MIMI, kwa maana SItawahi kuangusha. NItafute na ujue UKWELI, kwa maana UKWELI utakuweka huru (Yohana 8:31-36). NIjue na ujue UTUKUFU WANGU. NIngependa uone UTUKUFU WANGU, urithi UTUKUFU WANGU.
Ufalme huinuka na ufalme huanguka kwa sababu hazijatulia, msingi wao sio MWAMBA IMARA. Ufalme WANGU pekee ndio milele, milele kama UTUKUFU WANGU (Danieli 7:27). Utaona. Utaona, mwanaNGU, kila kitu kikiingia pahali pake panapofaa, panapofaa sawa, mazingira yanayofaa.
NIjue na ujue UTUKUFU WANGU. Naheshimu BABA YANGU na unapaswa kuheshimu wako (Yohana 8:49). Naja kuleta mwangaza, kuangaza njia. Hakuna kinachokaa kilivyo kwa mwili. Kupitia macho ya mwili, mtu anafikiri anaona kwa ung’avu, kwa udhahiri. Lakini Nakuambia la, mwanaNGU, kila kitu ni giza na muozo, kimepindwa. Mwili hauoni sahihi bali kwa upotovu.
Tazama kupitia macho ya ROHO na yote yatakuwa vyema. Tumainia katika MAMA yako SHEKINAH GLORI. Hatawahi kupotosha, kuelekeza vibaya. Anakuongoza KWANGU, MIMI, YESHUA, UTUKUFU wako. Kwa hivyo Mtumainie unavyoNItumaini, kwa maana Anakuongoza kwa Wokovu (Yohana 16:13-15).
Mtumainie, kwa maana Anakuletea moto wa utakaso WANGU. Usishtuke, lakini simama tuli na ujue kwamba MIMI NI MUNGU MWENYEZI. NItafanya NItakavyo ndani yako kama ilivyokuwa na yule kondoo dume aliyeshikwa katika kichaka. Tazama na ujue kwamba MIMI NI MUNGU, hata ELOHIM wako, Amejaribiwa na ni Mkweli. SItawahi kuacha. SItawahi rudi nyuma lakini sikuzote NItakuwepo nawe (Waebrania 13:5). Tu usikane JINA LANGU. Usikane yote yaliyotakatifu. Ishi kwa amri, amri ZANGU na NItajua kuwa unaNIpenda MIMI NDIMI NILIYE MKUU (Yohana 14:15, 22-24). Kwa hivyo sikiza na utulie. Jua kuwa MIMI NI MUNGU na hakuna mwengine.
Usitazamie bahari wala anga, lakini KWANGU MIMI MUUMBA wako AketiYE juu ya Mlima Sayuni AliYEtawazwa katika UTUKUFU katika makazi ya milele. Selah.