top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 81 “MUNGU ALIYE HAI Atahukumu Dunia!”

Updated: Mar 23, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa/ umeandikwa 25 Januari, 2020 kati ya saa 7 jioni na saa 8:15 jioni



Maandiko Husika


Waebrania 10:31

Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya MUNGU ALIYE HAI.


Warumi 2:5-6

5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya MUNGU,

6 “Atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.”


Mithali 28:13

Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;

Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.


Ujumbe wa Kinabii


Ee hii dunia itatetemeka kwa uwepo WANGU NInapokuja chini katika hasira na kiruu kikubwa kutembelea wana wa binadamu, wana wa vumbi (Isaya 24:17-22). NInashika kila mmoja wenu katika mkono WANGU na ee jinsi ni kitu cha kuogopesha, cha kutisha kuanguka katika mikono ya MUNGU ALIYE HAI YEHOVAH (Waebrania 10:26-31)! NItakuponda! NItakuseta kwa ajili ya njia zenu za moyo-mgumu, shingo ngumu, zisizo na toba. InaNIudhi na NIko karibu kukasirika mno na si hamaki za kitoto! MIMI NI HAKIMU! MIMI NI MFALME! Na ole kwa wale ambao walikuwa wakiwaumiza na wanaumiza watoto [WANGU] wachanga, bi-arusi, wachaguliwa na wateuliwa WANGU! Ingekuwa heri kwenu msingewahizaliwa, kuwa na uwezo wa kuonja jua!


Mnataka chuki? Mnataka kifo? Mnataka mauaji? Mtavuna kile mnapanda, enyi wafalme waovu wa dunia, wana wa uovu (Wagalatia 6:7-8). SItashiriki sehemu yoyote nanyi. Gawo LANGU haliko katika kambi yenu. Mliuza haki yenu ya kuzaliwa kitambo kabisa kama Esau alivyofanya kwa ajili ya tamaa za mwili, kwa ajili ya upuuzi, kwa ajili ya upumbavu (Waebrania 12:14-17). Tazameni NInapotikisa hii dunia kuliko wakati mwingine abadani! Mnadhihaki Sayari X? Yaja! Iko hapa tayari mnapohisi athari zake za mwanzo. Mnazieleza kuwa upuuzi, kuwa hali ya mambo, kuwa tu upumbavu katika macho yenu.


Lakini ngojeni muone kile NImewahifadhia (Warumi 2:5-11)! Ngojeni muone, chamchela mtavuna NInapomwaga hukumu ZANGU, kiruu CHANGU kwa ajili ya utovu wa shukrani wa hii dunia KWANGU MIMI, YEHOVAH, KWANGU MIMI, YESHUA, KWANGU MIMI, IMMA GLORIA RUAKH HAKODESH, ROHO MTAKATIFU Mzuri. TUlitoa CHETU bora zaidi ili kukomboa wanadamu. Kila mmoja WETU Alilipa gharama kubwa kukomboa nafsi zenu na ee isipokuwa tu wachache sana, yote TUnayokutana nayo ni dhihaka na bezo, chuki (2 Nyakati 36:15-16). Ee lakini ngojeni muone wakati maafa yanapokuja yakigonga mlangoni penu. Je, DAMU ya YESHUA inapatikana pale? Ee ni heri ipatikane au hofu kuu ndiyo yote mtakayoona.


Je, ghadhabu YANGU itapita? Au maangamizo yatasakini ndani yenu? Ni chaguo lenu, ee ulimwengu. Kwa maana jinsi NIliupenda ulimwengu NIkatoa MWANANGU wa pekee – MWANAKONDOO TAKASO – kuondoa dhambi za ulimwengu (Yohana 3:16-21). Lakini mlifanyia nini DAMU ya MWANAKONDOO? – YESHUA WANGU, bila doa kabisa, takatifu kabisa. Je, mliikanyagia chini? Je, mliipaka kwenye mihimili ya mlango wa moyo wenu? Mlifanya nini?


Muda unayoyoma. Uvumilivu WANGU unapungua na hilo ni jambo la kuogofya, kwa maana fikiria jinsi Neno LANGU lasema MIMI ni mwingi wa neema na rehema (Hesabu 14:18). Mmefanya nini na wakati ambao NImewagawa? Kuweni wenye busara na kuweni upesi. Ni wakati wa kuwa wanyenyekevu ili msianguke. Kiburi huenda kabla ya mwanguko. Msichukulierehema YANGU kama kwamba NInapuuza dhambi yenu. Angukeni mbele YANGU katika toba pamoja na unyenyekevu wa kweli. Kiri makosa yenu na NItasamehe (Mithali 28:13). Ee jinsi Navyopenda uumbaji WANGU, lakini wapi upendo wa MIMI?


Jinsi Navyolia na kuomboleza! BABA yenu Anahitaji kufarijiwa. UTATU MTAKATIFU Unahitaji kufarijiwa, kwa maana TUnatoa na kutoa, lakini ni nini TUnapata badala yake? Dhihaka na uchongezi zaidi. Tubuni, ee wafalme wa dunia! Tubu, kwa maana muda ni mfupi sana. Njoni katika mikono ya BABA yenu Aliye na upendo. Maana bado muda kidogona NItaficha uso WANGU katika kiruu kikuu (Kumbukumbu 31:17-18).


Kuweni tu wanyenyekevu na kuweni tu upesi kutii BABA wenu wa MBINGUNI. Kila amri NInayopeana yaja kutoka kwa moyo wa upendo, maana Najua njia iliyoko mbele yenu – pale mnapaswa kuenda na kile mnapaswa kufanya. NIko kila mahali, je, sivyo? NInatenda kwa manufaa yenu (Zaburi 68:19).


Mwisho wa Neno.

13 views

Recent Posts

See All
bottom of page