top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 78 “Shikeni Ujasiri WANGU na Msijue Woga Wowote!”

Updated: Mar 23, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 23-24 Januari, 2020


Maandiko Husika


Wagalatia 6:7-8

7 Msidanganyike, MUNGU Hadhihakiwi; kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. 8 Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa ROHO, katika ROHO atavuna uzima wa milele.


Isaya 41:10

Usiogope, kwa maana MIMI ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana MIMI ni MUNGU wako; NItakutia nguvu, naam, NItakusaidia, naam, NItakushika kwa Mkono wa Kulia wa Haki YANGU.


Ujumbe wa Kinabii


Andika, kwa maana maneno haya ni aminifu na kweli. NItaangamiza maadui WANGU na hakuna atakayebaki amesimama. Ni mara ngapi inabidi NIonye, msiwaguse NIliowatia mafuta na wala msiwadhuru manabii WANGU (1 Nyakati 16:22)?! NIMEKASIRIKA! Na Nanguruma toka Juu! Je mnaNIsikia, ee maadui WANGU?! NItachinja kutoka mashariki hadi magharibi. MIMI SIdhihakiwi (Wagalatia 6:7-8). Hauchezei MUNGU! HamNIdhihaki, kwa maana mtalipa na nafsi zenu siku ii hii ikiwa hamtatubu! NIMEKASIRIKA!


Lakini SIjakasirikia Bi-Arusi WANGU Mpendwa. Nakubusu. Nakupapasa kwa mahaba. Je, unahisi mguso WANGU? Ni mtakatifu. Ee jinsi NInavyotamani kuwa na Bi-Arusi WANGU! Nalia, kwa maana Nakuona ukidhulumiwa lakini Sisimami pale kwa uzembe. NIko nawe hadi hata katikati mwa dhoruba. SItakuangusha au kukutelekeza, kwa maana hii ni Ahadi YANGU na waweza ipeleka benki [Yaani Ahadi za MUNGU ni hakika na za kutegemewa] (Waebrania 13:5). Neno LANGU halidanganyi. ALEF na TAV haijagawanyika, lakini ni UMOJA! MIMI YEHOVAH, MIMI YESHUA, na MIMI IMMA GLORIAH – SISI ni UMOJA na hakuna mwingine – hakuna kifano (Kumbukumbu 6:4).


Usiogope, kwa maana NIko nawe kukuthibitisha na Mkono WANGU wa Kulia wa Haki. Soma Isaya 41:10. Ishikeni akilini. NItaenda mbele zenu kuwaongoza katika njia zote. JINA LANGU ni YESHUA na MIMI ni ujasiri. MIMI ndiYE SIMBA kutoka Kabila la Yuda na SItashindwa (Ufunuo 5:5). Haiwezekani. Kwa hivyo shikeni ujasiri WANGU na msiupoteze. Msiupoteze watoto WANGU, kwa maana NImewafanya mashujaa, sio goigoi. Simameni wima. Simameni imara. Jipangeni kivita. Ingieni katika msitari. Tiini JENERALI wenu. Hii si kwata.


Maisha yanawezapotezwa lakini hayatapotezwa ikiwa tu mtatii. Kaeni katika mpangilio, kwa maana NImechora msitari wa vita. MIMI naMI na Nyumba YANGU, TutaMtumikia BWANA YEHOVAH MUNGU MWENYEZI, BABA YANGU. Kwa hivyo tilieni maanani, watoto WANGU, na msiwe na wasiwasi (Wafilipi 4:6-7). Nyinyi nyote mmekua sana na mtaendelea kukua ikiwa mtaegemea KWANGU hata kama vile mmea hunyooka kuelekea kwa jua. NItawategemeza. NItawaponya. NItawathibitisha. NItawatakasa. MIMI ni BWANA wenu na nyinyi ni kondoo WANGU wa thamani ambao Napenda sana (Yohana 10). Je, SIkuwafia, SIkufufuka kwa ajili yenu? Ee upendo WANGU kwenu, hamwezi fahamu!


Kazieni tu fokasi kwenye Msalaba. Jione mfu kwenye msalaba lakini hai ndani YANGU (Wagalatia 2:20). NIna Ufufuo na Uzima (Yohana 11:25-26). MIMI Najua yote, [ni] Mweza yote. “Inameni na mtii,” haya ndiyo maneno NInayo kusema. Kuweni tu katika amani na msijue woga wowote. NInachezea maadui WANGU. NItakuwa na kicheko cha mwisho; naam, MIMI, YEHOVAH, na MIMI, YESHUA, na MIMI, IMMA GLORIYAH. Kwa hivyo kazieni fokasi kwenye amani na mwe na amani. Pumzikeni ndani YANGU, kwa maana MIMI, BWANA MUNGU MWENYEZI, NImependezwa nanyi.


Mwisho wa Neno.

4 views

Recent Posts

See All
bottom of page