top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 9 “Yerusalemu, Mbona Unatesa Manabii WANGU?”

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa Nabii Hannah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 24 Januari, 2019

Ujumbe wa Kinabii


(Tulipokuwa tunasoma 1 Yohana 5, niliweza kusikia nyimbo katika roho yangu, na niliona YESHUA Akinitabasamia na kusema…)


Unaimba katika Nyua YANGU, kelele ya furaha ya milele.

Ukiwa wa Dunia unakusanyika, mwaka baada ya mwaka, zama baada ya zama. Imeonywa mara nyingi sana.

Watoto, sikizeni. Hazina ZANGU, tumaini katika mkono WANGU. Kile NImewafanyia ni kazi iliyo barikiwa. NInashona katika kila mmoja wenu uzi WANGU wa Uhai (naona YESHUA Akishona ndani yetu uzi wa fedha). NIliweka maisha YANGU katika kila mmoja wenu, kufanya kazi YANGU. Siri za siri. Tafuta na mtapata.


Wanatesa watu WANGU, si chochote kipya. Yerusalemu huua Manabii WANGU. Wako radhi wabaki viziwi, na kutotaka Maneno YANGU yaandikwe kwenye mwili wao mzima. Jinsi Navyohuzunika kwa hilo. NIlikuja kurejesha kazi NIlipatia Moshe, ambayo anaongoza. Mambo mengi yaligeuzwa maana.


MIMI ndiYE TORAH INAYOISHI! Unapoishi ndani yake, unaishi ndani YANGU. Na Nazungumza nawe, nanyi nyote. Kiasi tofauti tu. Nawathamini nyinyi nyote kuliko chochote kile. Moyo WANGU ulihisi kuvunjwa [kwa wale wanaoNIkataa].

Nawapenda, nyinyi nyote! Mna vipande vya moyo WANGU ndani yenu. Hapo NIliweka Olam YANGU (Ulimwengu, Mhubiri 3:11, Ha’olam – ulimwengu, mara nyingi katika Kimombo hutafsiriwa ‘Milele’).


NIletee kile hamuelewi na NItawapa majibu. Ikiwa hamtauliza, hamtawahi jua. Msiende kwa uelewa wenu. shetani huwa pale daima kupotosha.


Si tu kiroho, lakini kimwili. Mhuri u mkononi MWANGU, na NInatia mhuri wale watiifu. Upepo hautawagusa. Lakini upepo wa hukumu utapuliza! Hu! (YEHOVAH Anapuliza upepo kutoka mdomoni MWAKE). Yote imekwenda! Hu! Kumvi, yote imeenda, imechomeka! Hamuwaoni tena!


Zawadi ZANGU huja pamoja naMI. Kama vile NENO LANGU lasema kwa wazi. Na miguu yenu itakimbia na haitachoka. Fanyeni kazi YANGU, Watoto. Fanyeni kazi YANGU na msikawie.



Mwisho wa Neno

5 views

Recent Posts

See All
bottom of page