top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 6 “Agano la Watoto na MUNGU!”

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa Nabii Hannah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa Januari 21, 2019

Ujumbe wa Kinabii


Kando ya Kiti CHANGU cha Enzi, NIna sanduku za hazina nyingi zilizopeanwa na Watoto WANGU. Na agano ni mojawapo, kwamba muheshimu kile NImewapa na NImependezwa. Nyinyi nyote yapaswa muandike moja na hilo litakuwa NAMI.


Maisha yenu ni ushuhuda KWANGU. NImefurahia kusikia Watoto WANGU wanaNIheshimu na kuNIstahi.


Mnasimama juu ya kiota cha tai, mkitazama chini. NInapoonyesha windo mbele yenu, nyoka wenye sumu kali, wakiiba panya. Mtawararua na kucha zenu za dhahabu. Mkiwa mmetiwa mafuta Matakatifu. Mtawararua maadui katika JINA LANGU pekee. Pigana vita katika JINA LANGU, ulizine Malaika WANGU wawasaidie. Wanawalinda nyinyi nyote. Wakingoja tu kuachiliwa.


Ukuta wa Trump, msisahau kumuombea. Ako chini ya mateso mengi na moto, ombeeni muhula wa pili na NItampa muhula wa pili. Kama watu wa kutosha watauombea. Ana wengi wanaomuunga mkono kuliko CNN habari bandia wanaonyesha.


NInakasirishwa hata na wale wanaomnyamazisha Edward Snowden. Alifichua hiyo njama lakini serikali ya Marekani inajaribu kumnyamazisha.


(Naskia MUNGU Akipumua nje [Akitoa pumzi]) Nachukua pumziko kabla ya kuenda katika vita. Malaika WANGU wote wanangojea amri YANGU kurejesha urithi wa BiArusi WANGU, piga kelele, “Hallelu YAH!” Na Nitafanya hiyo kazi kubwa! Simba wa 15 atakuja na kurarua, kufanya kazi ya MWENYEZI.


Kwa hivyo furahieni Watoto WANGU, pigeni kelele, “Hallelu YAH!” kwa ajili ya kuja KWANGU. Nakuja kuokoa Biarusi WANGU. NInapaswa kuchukua Biarusi WANGU kabla apotoshwe. Lazima NIfanye kazi YANGU haraka, na Mpendwa WANGU ulihisi kasi iliyo ndani yako (kufanya vitu haraka).


Watoto WANGU wote wanapaswa wawe Biarusi aliyekomaa ili NIweze kuwatumia kwa wingi zaidi. Ukomavu unakuja na tajiriba, na Biarusi WANGU aliye na tajiriba ndiye Biarusi WANGU bora zaidi. Watapata ustadi wa vitu vya asili [ardhi, hewa, moto, maji]. Watatembea kikamilifu 100% katika roho. Kwa hivyo msikosee kama vile dunia (jinsi wanafikiri kudhibiti vitu vya asili inamaanisha). Wanajua tu ile bandia ambayo shetani anapeana. Lakini Nampa Biarusi WANGU kile kitu halisi! (1 Wafalme 8:38, Marko 11:23, Kutoka 14:21, Mathayo 14:29, Marko 4:39-40, 1 Wafalme 17:1) Watapata ustadi wake kwa ajili YANGU ili kutimiza mapenzi YANGU ndani yao!



Mwisho wa Neno

8 views

Recent Posts

See All
bottom of page