top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 36 “Sherehe Zenu ZinaNIzungumzia MIMI, YESHUA HAMASHIACH, Ee Israeli!”

Updated: Mar 21, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 11-12 Mei, 2019


Maandiko Husika

Mathayo 21:21 “YESHUA Akawajibu, “Amin, Nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika.”


Luka 7:50 “YESHUA Akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”” 2 Wakorintho 5:7 “kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.”


Ujumbe wa Kinabii

Ee Israeli, NIko karibu tayari kutikisa nguzo za dunia. Wakati Kiruu CHANGU na Ghadhabu YANGU itapita kwenye nchi, je mtapatikana na Damu ya MWANAKONDOO imemwagika mioyoni mwenu?


Ee Israeli, ni sherehe ngapi zinafaa kuja na kwenda kabla mfahamu NIko ndani ya zote? MIMI ni YULE MWANAKONDOO AliYEuawa kwenye madhabahu, ambaYE dhabihu LAKE linaondoa dhambi za dunia. Ni MIMI Hukaa nanyi katika vibanda katika wakati wa Sukkot.


NIlimwaga maisha YANGU kufanya Upatanisho kwa nafsi zenu. Wapi heshima YANGU kuu, ee Israeli? Dhabihu zenu hazimaanishi lolote bila MIMI, YESHUA. Mifungo yenu SIjali kuhusu, maana mnaNIvunjia heshima mnapokana Damu YANGU iliyomwagika kwa ajili yenu pale Kalivari.


Kwa hivyo Israeli, una nini la kusema kujihusu? Kwa maana Nasimama kwa mlango na kubisha. Nasimama kuwapa ushauri ikiwa mtatafuta. Nataka kuwapa ushauri wa hekima wa Wokovu. Njooni tu KWANGU na NItawafunza ukweli kuhusu (hizi) Sherehe, Sherehe Takatifu za BWANA. NIruhusuni NIoshe mbali ule uongo wa Marabbii waovu, maana wanatafuta kukuchafua, kukunajisi.


Msiruhusu hawa watu waovu, hawa waovu – nyoka, majoka, vipiribao – wamejifanya watu kukupindua. Osha mbalia wasia wao mchafu. Pokea yale Maji Yaishiyo ya Kweli yawajalie na kuwajaza hadi kufurika. MIMI, YESHUA, NIlikuja kushinda, kupindua giza la dunia na NIlifanya (hivyo). Kwa hivyo kuweni wenye furaha na mtubu upuuzi wenu, visingizio na uongo wenu wa kwa nini hamNIfuati.


Mababu wenu, wengi wa mababu wenu waliNIfuata, MIMI, YESHUA, katika siku ZANGU za kukanyaga mguu, katika siku za kusulubiwa KWANGU. Kwa hivyo mbona msitembee katika hatua zao? Msiabishwe na ushuhuda wao, ushuhuda WANGU. Kubalini Dhabihu YANGU ya Damu, Dhabihu YANGU ya hatia ya dhambi zenu.


NIlikufa na kumwaga Damu YANGU kwa ajili yenu. (NIlilia kwa uchungu walipoNIpiga tena na tena). Taji la miba NIlivaa ili kuondoa aibu yenu, ee Israeli. Laiti mngekubali na kupokea zawadi YANGU mliopewa pale Kalvari. Haikupeanwa kwa urahisi, maana SISI SOTE WATATU (YAH, YESHUA, IMMA) TUliteseka kuokoa nafsi zenu.


Tubuni tu na msiNItie shaka, ee Israeli. Maana SIdhihakiwi kwa urahisi. NDIMI NILIYE Hadhihakiwi au kuburudishwa, la kabisa. Kwa hivyo tahadharini ee Israeli na mujinyenyekeze. Mtajipata mmevunjwa kwenye milima ya nchi yenu muipendayo – kondoo bila mchungaji. Songeni karibu NAMI, kwa maana mnaNIhitaji sasa kuliko wakati mwingine kabisa vile siku za angamizo, za mpingakristo zasonga karibu. Msikubali uongo wake. Nawaonya sasa kabla itendeke, kabla mwende katika barabara hiyo ambayo Naona afadhali msiipitie.


Mtakuwa na damu hadi kwenye hatamu ya farasi, ikitiririka kote nchini. Vitisho vingi mtaona, ambavyo NItaruhusu kuingia kwa ajili ya uasi na kiburi chenu, wivu wenu. Acheni kubishanabishana miongoni mwenu lakini badala yake kuweni wachunguzi wa matunda baada ya kugeuka kutoka njia zenu za uovu. NIkubalini MIMI kama BWANA MWENYEZI MUNGU wenu sasa kabla kuchelewa tayari. Leo ndiyo siku ya Wokovu, kesho yaweza kuwa kuchelewa tayari.


Mwisho wa Neno

2 views

Recent Posts

See All
bottom of page