Unabii 35 “Oh Israeli, Wakati wa Taabu Chungu uko Karibu Juu Yenu! Tahadharini!”
Updated: Mar 21, 2024
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 22-26 Aprili, 2019
Maandiko Husika
Yeremia 30:7: “Tazama jinsi ile siku itakavyokuwa ya kutisha! Hakutakuwa na nyingine mfano wake. Utakuwa wakati wa dhiki kwa Yakobo, lakini ataokolewa kutoka hiyo…”
Mathayo 24:21-22: “Kwa maana wakati huo kutakuwa na dhiki kuu ambayo haijapata kuwako tangu mwanzo wa dunia mpaka sasa: wala haitakuwako tena kamwe. Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupishwa.”
Ujumbe wa Kinbaii
dikwa katika Kitabu cha MWANAKONDOO. Je, mnaNIsikia? MIMI, BWANA MWENYEZI MUNGU, SIpotezi na SItapoteza mmoja (Yohana 6:38-40).
Wale ambao wanatupwa kando kama Yuda wa Kale – walikuwa wameandikwa katika Kitabu cha Waliofutwa (Ufunuo 3:5). Walianza wakiwa WANGU, lakini wakasaliti Utakatifu WANGU kwa ajili ya njia za shetani za unajisi na utovu wa heshima. Kuna wale ambao walichukua upande wa shetani toka mwanzo wa vile Vita Vikuu Mbinguni. Hawa wamo katika Kitabu cha Waliolaaniwa na Waliofedhehewa Milele.
Uko katika Kitabu kipi? Matendo yanazungumza kwa sauti kuliko maneno, ee Israeli! Matendo yaonyesha mgawo wa moyo. Mchoyo sana umekuwa, ee Binti mpotovu Yerusalemu.
Ni nini kisingizio chako cha kuvunja Oh maombolezo, kulia, taabu chungu na vilio vya machungu vikuu na huzuni wa nafsi!
Maumivu makali (ya moyo/akili) na maombolezo yasiyosemeka! Kwa maana hakujawahi kuwa na wakati kama huu katika historia ya mwanadamu. Giza, zito na baridi, linakamata na kunasa nafsi. Kwa wale ambao hawana joto, ROHO wa msamaha, huu utakuwa wakati wa kulaani na kukereketa kwingi juu ya vichwa vyao.
Esau atapanda na kuvuna tunda la muozo. Ammoni amevunjika. Esau amekaa katika vumbi (na) mfadhaiko – mikono yake bure na silaha zake zimevunjika toka mkononi mwake. Oh, ule huzuni wa mataifa! Mito, bahari za machozi zamwagika lakini nchi haijatakasika. Tabenakulo limeanguka bila yeyote kulifanya liwe sawa tena. Kuhani ametawanyika na Mlawi ameanguka!
Ee, Israeli, tauni za Misri zimekujia kwa ajili ya kutotii kwako. Maana SIjakuonya, ee Israeli, kwamba usipotii, NIngemwaga juu yako zile tauni na maradhi ya Misri (Kutoka 15:26)?!
Maandiko yanatimizwa, yatatimizwa katika kutotii kwako, ee Israeli. Fungua macho yako wazi na ushtuke, ushangae, simama umestaajabika. Ni heri utubu, ee nyumba ya Israeli, ee nyumba ya Yakobo! Kwa maana wengi watakuwa vichinjo na dhabihu ya BWANA hiyo siku. Jiokoe kutoka kwa hiki kizazi kiovu na potovu (Matendo 2:40). Usiingie katika milango ya Jahanam, ya mauti na kizazi hiki. Usijiunge na hili kundi la damu, ukoo wa dhambi na uovu!
Wapi dhabihu yako, ee Israeli? Wapi Damu ya MWANAKONDOO wa Pasaka wa kweli (Yohana 1:29)?! Mnajiwasilisha katika kiburi mbele ZANGU, MIMI, YEHOVAH, kama dhabihu zinazoishi/zilizo hai, lakini damu yenu imechafuliwa na ibada bure ya sanamu – ni nani analo gari ghali kabisa, tuzo la fahari kuu kabisa, nani alienda leo Shul muda mrefu zaidi, nani alienda Ukuta wa Kilio mara nyingi zaidi wiki hii! Finyu sana! Njia zenu ni chukizo sana mbele ZANGU, ee Nyumba ya Israeli! NInawahurumia, kwa maana katika Dhiki Kuu mtapitia!
Je, ulijua kwamba MIMI, YEHOVAH, Nakuhurumia? Nakupenda, Binti WANGU mpotovu! Nakupenda na karibuni utakuwa, utahisi kumbatio LANGU – kumbatio la mpenzi ambaye Hataki kuachilia BiArusi WAKE. Kwa hivyo njoo KWANGU, ee nchi nyonge na chofu, nchi ya ukiwa, nchi bila maji. Acha NIkujaze na Maji YANGU Yaliyo Hai.
Natuma Mashahidi WANGU Wawili kuwa baraka kwako (Ufunuo 11). Nawatuma kufufua wafu, kihalisia na kiroho. Nawatuma kulisha umati samaki na mikate. Kile YESHUA Alifanya, watafanya pia. Kile YESHUA Alifanya, watafanya pia. Miujiza mingi sana watafanya, watatenda. Tu, msitie shaka. Tu, msitie shaka. Pokeeni na muamini tu. Pokeeni na muamini tu.
Msiwafukuze! Nawaonya! Nawaonya sasa! Ikome! Msiwe wamwagaji wa damu isiyo na hatia, kwa maana NInapoangalia juu ya hii dunia Mashahidi WANGU Wawili wakiwa wamelala wafu katika barabara za Yerusalemu na NIpate damu yao kwenye mikono yenu, kutalipwa na Jahanam (Ufunuo 11:7-11)! MnaNIsikia?!!
Najua kile utafikiri hata kabla hilo wazo litengezwe kichwani mwako (Zaburi 139:2-4). Kila mpigo wa moyo wako uko kwenye kiganja cha mkono WANGU, maana kuweko kote, uumbaji wote unasimama kwa usikivu WANGU. SItapoteza mmoja ambaye jina lake limeanSabato ZANGU, kunajisi JINA LANGU TAKATIFU, kubadili muundo/kueleza vibaya Torah YANGU Takatifu, ee Israeli (Ezekieli 36:20-23)? NIliwakabidhi mengi, na haswa Moyo WANGU – MWANANGU. Siku yako ya kulipa madeni ya makosa inakaribia haraka na Taifa ambalo linapaswa liwe linafunza mataifa mengine Utakatifu badala yake linayaongoza katika uasi dhidi YANGU, MIMI, YEHOVAH.
Moyo WANGU unahuzunika. NDIMI NILIYE Amevunjika moyo, Amevunjika moyo kweli. NItafanya nini? Utafanya nini? Utafanya nini katika siku ya maafa, kwa maana nyumba yako umeachiwa katika ukiwa? Je, NItateketeza nyumba hadi kwenye msingi wenyewe na NIsiache jiwe moja juu ya lingine? Ee Israeli, utavuna kile umepanda. Utavuna hadi kwa ukamilifu na utafanywa kiwete kama Yakobo. Halafu NItakubeba kwa mikono YANGU hadi kwa usalama – wakati utalia, “Mbarikiwa ni YEYE Ajae katika JINA la YEHOVAH!” (Mathayo 23:37-39).
NDIMI NILIYE Atatuma MWANAKE wa Pekee kwako katika hiyo saa, katika muda huo. JINA LAKE ni YESHUA HAMASHIACH. UsiMfukuze. Usitelekeze kikombe cha Wokovu kilichomomkononi MWAKE, kikombe cha fedha cha ukombozi. (Ninaona maono ya YESHUA Akiwa na kikombe cha fedha katika mkono WAKE) YEYE ni BWANA na MWOKOZI wako.
Ee Israeli, NInakukujia. Ndiyo, MIMI YESHUA, Nakukujia. Je, wasikia hatua ZANGU? Ita juu ya JINA LANGU na hautavunjika moyo, hautaibishwa (Yoeli 2:32). Usizuie, usikawie, ee Israeli. Leo ndiyo siku ya wokovu, ya kufurah ia, ya shangwe. Ni mara ngapi lazima NIkuweke katika ukumbusho wa Neno LANGU Takatifu? Ni lini utafahamu MIMI NDIMI NILIYE?
Heshimu BABA yako na MAMA yako (Kutoka 20:12). Lakini unapoNIkataa, unafedhehi HASHEM ADONAI. Mnafedhehesha dhabihu YAKE kwa ajili ya nafsi zenu pale Kalivari – Dhabihu YANGU ya Damu.
Ni Damu YAKE pekee itaridhisha ghadhabu YANGU Asema MIMI, YEHOVAH. JINA LAKE pekee likiitwa litakupa usikivu mbele za MFALME MKUU. Ee Israeli, kwa hakika utakunywa kikombe kilichopo mkono WANGU wa kulia. Hadi kwa ukamilifu utakunywa – kwa maana Unabii, kwa maana Maandiko lazima yatimizwe. Na NItakutumia kujaribu mataifa. Utakuwa kikombe cha kutetemeka, cha mduwao kwao na yatashikwa na wazimu (Zekaria 12:2). Mataifa yatakuwa katika vurumai. NItaokoa Waliobaki WANGU – wale ambao hawajainamisha goti kwa Baali au kukubali mpingakristo. Watakuwa Watakatifu KWANGU, hata kama fumba Lililotengwa (Warumi 11:16).