top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 33 “Kuweni na Imani Ndani YANGU kama vile Nina Imani ndani Yenu, Asema YESHUA HAMASHIACH!”

Updated: Mar 21, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 18 Aprili, 2019



Maandiko Husika


Mathayo 21:21

YESHUA Akawajibu, “Amin, Nawaambia, kama mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ngʼoka, ukatupwe baharini,’ litafanyika.


Luka 7:50

YESHUA Akamwambia yule mwanamke, “Imani yako imekuokoa; nenda kwa amani.”


2 Wakorintho 5:7

kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona


Ujumbe wa Kinabii

Kuweni na imani ndani YANGU vile MIMI Nina imani ndani yenu. Upendo WANGU kwenu haufi, kwa maana haungeuawa pale kwa Msalaba. Sikieni ujumbe WANGU siku hii, kwa maana SItawapotosha. Ni kwa tamaa zenu wenyewe ambazo mtu anapotoshwa.


Shikilieni kwa nguvu kwenye pindo la Vazi LANGU na msiachilie. Msishikilie au kugandamia kwa vazi fasiki la Babiloni. Limeota ukungu, liko na baka. Juu yake kunapatikana dhambi zote za wanadamu.


Ikiwa hauwezi NItumaini sasa, nini kinafanya ufikiri unaweza NItumaini wakati huo? Hiyo ndiyo maana Nakupa nyakati rahisi kufanya mazoezi, kukamilisha kile kinachokufanya adili, ili unapokuwa umegandamizwa kila upande, hautaporomoka. NIsikie, MwanaNGU, na usiogope!


Nanena nawe katika mafumbo na hadithi za mafumbo MwanaNGU. Kwa hivyo, kuwa msikivu mwanaNGU, maana NIna ufunguo na ujuzi wa kufungua mafumbo, kukuonyesha njia. Ufunguo ni Utakatifu, mwana WANGU, na Nakupa ufunguo huu maalum siku hii. MnaNIpendeza mnapotii, kwa maana hii inaonyesha upendo wenu KWANGU. Ndiyo, MIMI, YESHUA wenu, Niko nanyi sikuzote.


Kwa hivyo tafakari juu YANGU hii leo unapofanya kazi, unapoendelea na siku yako ambayo NImekupa. Kuwa na shukrani na moyo wa mtumishi, kwa maana haya ndiyo yale yote yanayohusu Ufalme. NaMtumikia BABA YANGU, naYE AnaNItumikia. SISI UTATU MTAKATIFU, TUnatumikiana na hili ndilo TUnalotarajia kutoka kwa watoto WETU.


Pendaneni na mtakuwa mnatimiza [zile] amri. Namwaga upendo WANGU ndani yako siku hii, WANGU Unayeng'aa kwa ung'avu. Ng'aa, metameta kwa ajili YANGU siku hii, kwa maana NInang'aa kwa ajili yako, maana si MIMI MWANGAZA wako UONGOZAO? NInang'aa na NItang'aa kwa ajili yako ili giza lisikukumbe. Kuwa tu mnyenyekevu. Kuwa tu upesi. Hakuna muda mwingi kabla ya siku za maangamizi. Nitakulinda. NIkazie tu macho – BWANA MKUU na MWOKOZI wako.


Nakuvuta KWANGU, kwa maana WEWE ni WANGU na MIMI ni wako. NInakupenda sana. NIonyeshe moyo wako wa upendo siku hii. Selah.


Usingojee hisia. Usingojee hisia, mwanaNGU, kwa maana zitafanya kinyume na imani yako ukiruhusu. Hisia hazifai kamwe kuamuru ukweli, ukweli ni nini. Wafalme wengi wameuawa kwa sababu walingojea hisia bure, mvutio wa bure kwa mwili. Lakini [NIngependa] kuwaepusha na hili.


Kwa hivyo usingojee – lakini kumbuka sikuzote – imani ni jambo la hakika, sio hisia. Hisia hudanganya. NIlisema mara nyingine mwanajeshi hutaka kutoroka kwenye vita kwa sababu ya uchovu, unyong'onyevu, woga. Lakini Wanajeshi WANGU ni Mashujaa na sio waoga; wanaume na wanawake jasiri ambao NItatumia kama shoka la vita katika hizi Nyakati za Mwisho.

Kwa hivyo NIkazieni fikra MIMI, kwenye ukakamavu WANGU, kwenye ushupavu WANGU, kwenye imani YANGU. Sitawahi waangusha, lakini sikuzote NItawathibitisha na mkono WANGU wa kulia wa haki wa Wokovu. Selah.


Kwa kweli Nakuambia mwanaNGU, Nawatuma kama kondoo miongoni mwa mbwa mwitu. Hawa si mbwa mwitu wa kawaida bali ni aina ya wale wakali kabisa. Lakini NItavunja kiburi chao, [NIta]fadhaisha meno yao.


Nitakuwa na huruma nyingi kuliko hukumu (Alimaanisha Anatamani kuonyesha huruma kuliko mtu aangamie). Napenda kusamehe, ama kwa nini Ningetuma MWANANGU wa Pekee kulipia adhabu ya makosa na dhambi yenu? Alimwaga Damu YAKE kufanyia upatanisho nafsi zenu. NIabuduni siku hii. Tazama upendo WANGU kwenu! Hauwezi elewekakatika haya maisha. Jua tu neema YANGU inawatosha katika mambo yote. Mkono WANGU uko juu yenu, kwa hivyo pumzika ndani YANGU. Nawapa nguvu. Nawapa nishati. NInafanya njia zilizo kombo zinyooke na bahari [iwe] laini [ya] kusafiri.


Sio katika mambo yote mtahitaji kujua sababu kwa nini. Kuwa tu na imani na NItateketeza adui. Naam, MIMI, YEHOVAH NItawaondoa kabisa na kuwaangamiza, NItatupa chini kila kitu kinachoweza kutupwa chini. Kile ambacho kinapaswa kupandwa kitapandwa na kusitawi.


Nyinyi 7 [wana na mabinti] mmepandwa na MKULIMA WANGU MKUU wa Bustani, ambaYE JINA LAKE ni EZRA, katika JINA LA YESHUA. Nyinyi nyote mnasitawi mbele ZANGU. Kwa hivyo jipeni moyo na msitie shaka, msiogope, maana BABA yenu YEHOVAH yu hapa kuwaokoa, kuwakomboa kutoka kwa mkono wa mwindaji (Zaburi 91:3). Niko nanyi hadi mwisho wa nyakati (Mathayo 28:20). Selah


BABA! BABA! BABA! YEYE ni nuru YANGU na furaha YANGU. Raha ya maisha YANGU. Ni ndani MWAKE NInakaa, ambamo NInaishi, Natembea na kuwa na Uzima WANGU. Usiwahi tia shaka Upendo wa BABA kwako, mwanaNGU mpendwa. Je, ulijua kwamba kito kinacho – kuwakilisha kiko katika taji YAKE, kimepachikwa pale na upendo?


Hapotezi hazina YAKE, mpendwa WAKE, mahabubu WAKE. Wewe ni vitu hivi vyote na hata zaidi. NImewakabidhi mengi na NIta-kabidhi katika siku zijazo, lakini sasa sio wakati wa kuzungumzia mambo haya, kwa maana. MIMI YESHUA, SItaki shetani ajue mipango YANGU mizuri NInayo juu yenu.


Ni mizuri na ya kuwafanikisha katika njia zote. Mtaokolewa kutoka kwa hofu zenu zote na hamtazikumbuka; hata kama vile mama anayezaa husahau huzuni wake wote mara moja mtoto anapozaliwa. Kwa hivyo Nawaacha na haya Maneno siku hii. Je, mtaNIimbia? Je, mtaNIfariji?


Ee binti YANGU, binti YANGU, jinsi umetamani sana kuwa na MIMI. Jinsi NImetamani sana kuwa na wewe! Haiko mbali. Karibuni NItakuja katika saa ya usiku wa kati na mng'aro wa kuvutia wa moto na nuru machoni MWANGU kukunyakua.

Baki tu mwaminifu. Kuwa kweli. Tumaini dada zako, maana wanajua jinsi ya kukusaidia. Hakuna tena kuegemea kushoto au kulia, ukiyumbishwa na hisia zisizo za kweli. NInayo mipango mikubwa kweli juu yako, mifano yake ambayo hakuna jicho limeona au sikio kusikia. Kwa hivyo baki mnyenyekevu na NItakuinua. Kila kitu katika wakati na msimu wake kamili.

Ee mwana mpendwa. Nakuita katika saa ya usiku wa kati. Barabara zilizo [kuwa] kombo zimenyooshwa, milima imesawazishwa, vipande vimewekwa pamoja tena, kile hakiko kizima kimefanywa kizima. MIMI ni MREJESHAJI wa vitu. Nafsi yako ni muhimu KWANGU.


Kama FUNDI STADI, Nafanya kazi masaa mengi, siku nyingi, wiki nyingi kuregesha pamoja kile kimevunjwa vunjwa. Ninapata kile kimepotea na kukiregesha, kufanya kizima, kufanya kizuri tena. Haya ndiyo yale Nafanya kwa sababu ya upendo.


NImefanya masaa yasiyohesabika ya upasuaji juu yako, maana MIMI ndiYE TABIBU MKUU. Wewe ni mgonjwa WANGU na NItafanya kamili, maliza ile kazi nzuri NImeanza ndani yako. Kuwa tu na imani na usitie shaka, usitoe bendeji hadi ni wakati. Najua ni nini kilicho bora zaidi, ni nini dawa nzuri zaidi.

Neno LANGU NInakuagizia kila siku. Hilo ni ponya-yote isipokuwa ikikataliwa, maana Sitalazimisha yeyote kupona. Hivyo sivyo inavyofanya kazi. NIshalipa Gharama, hata hadi chini kwa lile tone la mwisho la Damu YANGU.


Kwa hivyo Nataka kukuona ukisitawi, kukuona ukiruka kwa furaha. NImekuita na kukutia wakfu kwa wakati huu na hii saa. Kamwe Sichelewi. Unafikiri tu NIna[chelewa]. NInafunga vidonda vyako. NInapaka malhamu. NInakuosha na kukufanya mzima tena. Kwa hivyo NIpe umakini, mwanaNGU. Fuata mwongozo WANGU na utasitawi katika njia zote.


Utaona. NInakupenda. Sasa kimbilia Mwito wa Juu wa kuwa Bi-Arusi. Fanya upesi. Na upendo, YESHUA wako.


Upande wa 2 wa Unabii

Ufaransa, Ufaransa! NItakupasua vipande viwili kwa ajili ya ule ukatili ambao umefanywa dhidi ya wale bado hawajazaliwa [wale waliomo tumboni mwa mama zao]. Kwa ajili ya makosa matatu na kwa ajili ya manne, NItakuhukumu: kwa ajili ya kiburi unabeua MUUMBA wako. Sijafurahishwa. Sidhihakiwi.


MUNGU Mkuu YEHOVAH Atakuhukumu kwa ajili ya matendo yako ya uovu. NIlituma Mariamu Magdalena kwenu. Mmefanya nini na ule urithi aliacha nyuma? Sioni chochote bali kuzorota kwa maadili, uvundo katika mapua YANGU, uvundo wa kuoza na mauti, dhambi. Mtalipia hili!


Wapi huruma yako, ee Marekani? Fursa nyingi NImekupa. Nakupa moja zaidi (Trump atashinda muhula wa pili). Lakini Najua kile kitatendeka vile mstari juu ya mstari, agizo juu ya agizo yanatimia.


Neno LANGU halidanganyi. Kile kimefanyika mbeleni kitafanyika tena. NItumainieni tu, ee Waliobaki WANGU. NItawaweka salama katika moyo wa Marekani. Kombora zitapita juu lakini hazitakuja karibu na makao yenu. Hazitawateketeza. Amkeni wajinga watano (Mathayo 25:1-13)! Amkeni! Msishikwe ghafla.


Kujihukumu si kazi yenu, lakini ni kazi ya BABA wenu wa MBINGUNI. NInakarimu mno yule NInayekarimu mno. Msitie shaka. Najua umbo la mwanadamu, umbo la vumbi, na Najua roho zipi NImeweka katika 7 WANGU.


Mwili ni bure KWANGU. Siweki fokasi kwenye [yaliyo] upande wa nje bali wa ndani. Jifunze hili somo vizuri, mwanaNGU, na utaepuka mitego ya mashimo yaliyofunikwa funikwa na huzuni kubwa, Asema, MIMI, YEHOVAH, ambaYE Amezungumza siku hii. Sasa itilie maanani!


NInakupenda mwanaNGU. UnaNIsikia? Ndiyo kuna kiwango na utaratibu, lakini hiyo haibaini thamani yako. Thamani inapatikana katika Damu ya MWANAKONDOO, MWANAKONDOO WANGU wa Pasaka, YESHUA HAMASHIACH. Katika YEYE unatumaini. Kuwa tayari, kwa maana utaona moto ulio machoni MWANGU unaopenyeza nafsi. Niko kwa [uzuri] wako na sio dhidi yako. Ni baba yupi apendaye ambaye yuko dhidi ya mtoto anayependa mno? Haiko hivyo.


Kwa hivyo kuweni waangalifu na wanyenyekevu. Natazama kila kitu mnafanya na Nawafunza, Nawaongoza. Wakati ujao si jambo la kuogopa, lakini la kutazama kwa mshangao wa Utukufu wa JINA LANGU na unashikamana ndani yake kwa msisimko. Na upendo, BABA wenu YAH AnaYEwapenda na Anawaweka kama bendera angani. Selah.


Ndiyo, NItawaonyesha Mpango Makini Mkuu, mpango makini wa BWANA, wa mwito wenu, wa kudura yenu. BABA wenu Ashaonyeshwa nyingi yake tayari. Hiyo ndiyo maana Ana uhakika sana mtafanikiwa. Hata hivyo, bakini wanyenyekevu mbele ZANGU, maana hamtaki kile kilifanyika kwa wengine wanaoanguka kuwafanyikia. HamNItaki MIMI NIsiwaache mchukue hiyo simu katika njia hiyo.


NInakupenda mwanaNGU, na NInanena tu baraka juu yako, kwa maana hilo ndilo lile BABA mzuri hufanya. Mimi ni YEHOVAH na NInaMtuma MWANANGU wa pekee kukujia. Kwa hivyo fanya haraka na ufanye vile vitu NImekuitia kufanya. Bado kuna kazi nyingi ya kufanywa, lakini ukiwa na bidii, itatimizwa katika wakati WANGU kamili.


Hakuna mmoja wenu kwa kweli anayefahamu ukubwa wa huu wakati na msimu. Bakini tu watiifu na mfurahie kila rekebisho, kwa maana rekebisho ni malhamu ya uponyaji. Ipake. NInakupenda, mwanaNGU, na NIna mipango mizuri sana kwako. Kile MIMI YEHOVAH, NImeweka pamoja, mtu yeyote asitenganishe, kwa maana ingekuwa bora ikiwa asingewahizaliwa. Selah.


Usimtazame mwanamke mgeni, kwa maana ingawa anabembeleza na macho yake, vita vimo moyoni mwake kuchukua hiyo nafsi ya thamani kuiongoza kwenye daraja ya Jahanam kupitia kwa lile lile lango lake. MwanaNGU, egemeza masikio yako KWANGU. Msikize MAMAko Mzuri (ROHO MTAKATIFU), kwa maana Anatunza kwa uhai ndani yako, sio kifo. HApotoshi yeyote bali Anawavisha na Mavazi ya Kimwana Mfalme, ndio, hata mavazi ya Bwana na Mfalme. Kwa hivyo kuwa mnyenyekevu na mwepesi wa kutubu.


Toba ni adili, pia subira. Beba mkatale WAKE na usitawi katika zile nyakati ngumu. Kana mkatale na HEKIMA YAKE, na mauti yatakukwamilia. Kwa hivyo siku hii Mkwamilie. Usitelekeze maagizo YAKE ambayo yanatunza pekee kwa uhai. Fuata njia ZAKE ambazo zinaelekeza juu, kwenye mlima ambamo, wenye moyo takaso wanaishi mbele ya Uso wa BWANA. Aliinuliwa mbele za BWANA; daima furaha YAKE.


Anayepata mke mwema anapata baraka kutoka kwa BWANA. Siku zake zitakuwa ndefu, zitarefushwa ili aweze kufurahia utamu wake na tunda lake karimu. Ana bidii katika kazi ya mkono wake, kila siku akipakia nafsi yake na fadhila za ALIYE JUU SANA. Yeye si mwenye kiburi au mfidhuli, lakini daima anaendelea kutafuta njia za kuboresha unyenyekevu wake. Anatiisha njia zake kwa bwanake, maana yeye ni Mtawa, akiwa mwangalizi wa nafsi yake.


Wanafurahia pamoja katika upendo, hawaachi tangi la ujana wao lililobarikiwa. Katika ndoa takatifu walioana na katika ROHO kwa ukweli wanaishi kwa uadilifu siku zao zote. Kando wanaweka tofauti zao, [wana]pata umoja katika ALIYE JUU SANA ambaYE faida na huruma ZAKE ni “ndiyo" na “amina.” Wanatafuta kuMpendeza YEYE pekee, maana ni KWAKE wanawia maisha yao.


Kwa hivyo furahieni Watoto WANGU, maana wabarikiwa ni nyinyi miongoni mwa wanaume na wanawake, miongoni mwa wanadamu. Bariki BWANA, ee nafsi yangu! Bariki JINA LAKE na sifu MFALME MKUU! Hallelu YAH! Selah.


Mwisho wa Neno

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page