top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 26 “Msitelekeze TORAH ILIYO HAI, Ee Israeli!”

Updated: Apr 13, 2024

Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 29 Machi, 2019


Maandiko Husika


Mithali 4:2

Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiache Torah yangu.

Yohana 1:14

Neno Alifanyika mwili, Akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu WAKE, utukufu kama wa MWANA pekee Atokaye kwa BABA, Amejaa neema na kweli.


Ujumbe wa Kinabii


NIsikieni, ee Israeli! Sikia jinsi NInavyo kwa upendo na shauku waita. Naam, hata na sauti ya Malaika mkuu Nainama chini kutoka Mbinguni MWANGU kuwalilia (1 Wathesalonike 4:16). Na mtasikia sauti yake (ya Malaika Mkuu). Atawaelekeza kwa MASHIAKH ben David (Daudi). YEYE ni MASHIAKH NAGID – YESHUA HAMASHIAKH. Atawaonyesha njia nzuri na adilifu – njia ya mababu zenu Abrahamu, Isaka na Yakobo.


Msitelekeze Torah, ee Israeli (Mithali 4:2). Mnauliza, “Jinsi gani tumetelekeza hazina yetu ya hazina?” Na NInasema, kwa kukataa Torah – iliyofanywa – mwili mmetelekeza Neno LANGU. Mnashika sherehe, Shabbat (Sabato) lakini mioyo yenu iko mbali NAMI. Hamjui kuwa andiko huua na kwamba ni ROHO MTAKATIFU SHEKINAH AmbaYE Anapeana Uhai (2 Wakorintho 3:6). YESHUA ndiYE Neno LANGU lililofanywa – mwili (Yohana 1:14). Amefichwa kote katika Maandiko yenu yote. Ee Israeli, jinsi NInavyotamani kuwapakata Mikononi MWANGU na Nita[wapakata] siku moja!


Mkono WANGU si mfupi sana [kiasi] kwamba hauwezi okoa (Isaya 59:1). Wala sikio LANGU zito kusikia au kiziwi, Niiteni tu, ee Israeli. Niiteni katika JINA la YESHUA HAMASHIAKH – YULE pekee ambaYE Anaweza okoa, YULE pekee ambaYE Anaweza komboa. Msitelekeze MASHIAKH wenu wa pekee. Msipuuze MWANA wa “NDIMI NILIYE” MKUU. YEYE ni MSHIKA – AMRI wenu. YEYE ni KUHANI MKUU wenu MBARIKIWA.


Kwa hivyo njooni KWANGU! Shirikini MAJI YALIYO HAI na mjistawishe. Jiokoeni kutoka hiki kizazi kiovu na kikaidi (Matendo 2:15,40). Ee Israeli, Wanafunzi WANGU si walevi wala wenda-wazimu. Acheni kukataa TORAH YANGU ILIYO HAI ambaYO inakaa ndani mwao. Lini mtakapoacha kukataa hizi Tochi za Mbingu iliyo juu kabisa? Nawatuma kama taa kuangaza giza lenu, kuandalia njia MWANANGU kurudi. Mnawakataa muda baada ya muda. Mtachomeka. Kote katika hii enzi ya dunia mmewakataa, Nyota WANGU kumi na nne. Lakini wanakuja kwenu mara moja tena katika hili kabiliano la mwisho.


Acheni kuwafukuza! SItawaachilia kwa ajili ya [kosa la] uhaini mkubwa. Mtalipa gharama iliyoje, ee Israeli! Mtalipa gharama, ee Israeli! Mtalipa gharama iliyoje inayochoma hadi vina vya Jahanam. Ee Israeli, mbona mwaNIdharau, MIMI MUUMBA wenu?! NItawageuza na kuwapindua juu chini, chini juu.



Mwisho wa Neno

6 views

Recent Posts

See All
bottom of page