top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 23 “MIMI, URIYAH, Nachukia Muziki wa Rap! Mpingakristo Atautumia!”

Updated: Apr 13, 2024

Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa 23 Machi, 2019



Maandiko Husika


1 Peter 3:10 “Kwa maana, ‘Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.’”

Wakolosai 3:8 “Lakini sasa yawekeni mbali nanyi mambo kama haya yote: yaani hasira, ghadhabu, uovu, masingizio na lugha chafu kutoka midomoni mwenu.”


Ujumbe wa Kinabii


Kuweni Ufalme wa Mwangaza. Tembeeni katika Mwangaza na mtakuwa kama Mwangaza, Watoto WANGU, Watoto WANGU Wachanga, Biarusi WANGU (1 Yohana 1:7). YESHUA ndiYE NURU MWONGOZO wenu (Yohana 8:12). Hakuna mwengine. MuMstahi YEYE sana. Hakuna upepo au mafundisho ya ajabu ambayo yanaweza Mzima, kuzima mwale wa udaima WAKE. Anawaka kwa ung’avu zaidi kuliko jua lolote, kwa maana YEYE ni MWENYEZI MUNGU.


MIMI, URIYAH, Nanena nanyi na hivi ni jinsi mnaitamka: U-RI-YAH. Yote pamoja. Watoto WANGU, Watoto WANGU, ee jinsi NInavyofurahia ndani yenu. NInapowatazama kutoka Mbinguni juu, kutoka kwa KITI CHANGU cha ENZI kilicho juu karibu na BABA YANGU, MAMA YANGU, KAKA YANGU. NIimbieni kwa maana MIMI ni MUZIKI – MWANZILISHI na MKAMILISHAJI wake.


NIliumba muziki kubariki moyo, akili, mwili, nafsi, na roho. Ee jinsi inavyoNIhuzunisha, jinsi NInavyoomboleza juu ya hali ya hii zawadi nzuri NImewapatia binadamu! Wanaitumia kuangamiza nafsi kupitia ‘rap’. Hiyo si ushairi! Hiyo ni takataka! Je, mnajilisha takataka, Watoto WANGU? Kwa wale ambao wanafanya [hivyo], wanaosikiliza huu upotovu wa chukizo, ikome sasa!!! Ikome!!! MnaNIhuzunisha mnapochafua nafsi zenu. Geukeni nyuma. Fanyeni masikio yenu viziwi, kiuhalisia. Funikeni masikio yenu na tena musikubali ushawishi wa hili angamizo la nafsi. Mnafikiri Nafanya mzaha, Naichukulia kwa uzito sana?! Je, ni heri musikize visingizio vya mwili, mafundisho ya mapepo? Au heri mNIsikize MIMI, MUNGU wa Muziki, wa burudani?


NInajua kilicho kweli na haki, kile ni muziki wa kweli katika umbo lake la utakaso kabisa. NInafasili burudani na sio ujinga wa mwili. Kwa hivyo NItumaini MIMI, Watoto WANGU. Hamjui kikamilifu hatari za huu upotovu unaitwa “muziki wa rap”. Hamkumbuki kilichotendeka katika siku za Babiloni, za Nebukadneza, jinsi muziki ulitumika katika kuabudu sanamu? Walicheza muziki na ala zao na kisha wakaanguka miguuni pa ile sanamu ya dhahabu. Sio tofauti leo. Hamjui tu.


Danieli 3:4-7: “Ndipo mpiga mbiu akatangaza kwa sauti kubwa, ‘Enyi watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha, hili ndilo mnaloamriwa kulifanya: Mara mtakaposikia sauti ya baragumu, filimbi, marimba, zeze, kinubi, zumari na aina zote za sauti za ala za uimbaji, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo mfalme Nebukadneza ameisimamisha. Mtu yeyote ambaye hataanguka chini na kuiabudu sanamu hiyo, atatupwa saa iyo hiyo ndani ya tanuru iwakayo moto.’ Kwa hiyo, mara waliposikia sauti ya baragumu, filimbi, kinubi, zeze, kinanda na aina zote za ala za uimbaji, watu wa kabila zote, mataifa na watu wa kila lugha wakaanguka chini na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameisimamisha.”


(Muziki wa rap na miziki nyingine ya kilimwengu) itatumika katika kuabudu mpinga-kristo na sanamu ya mnyama. Muonywe na mkae mbali! Nawaonya sasa kwa sababu NInawapenda. Ndiyo, MIMI URIYAH, Nawapenda. MsiNIhuzunishe. MsiNIdhihaki, maana mnaposikiza takataka hii, Inahuzunisha Nafsi YANGU. Nalia. Kaeni mbali na miziki inayonajisi. Mnapaswa kujua hili tayari. Muziki wowote ulio na kulaani, uchawi, midundo ovu ya ngoma ya ‘vudu’ (voodoo) ambayo iko katika miziki yote ya rap, usemi wa uasherati, uabudu sanamu. Msiruhusu hii ipatikane ndani yenu (Waefeso 4:29-31)!


Mnasema mnapenda mdundo, mnapenda tuni na hamsikizi maneno na kwa hivyo ni sawa vyovyote vile, kwamba bado mtasikiza? NIondokeeni! NInawaonya, maana uongo mkubwa, sihiri ya uongo imo ndani ya huu muziki. Okoeni nafsi zenu sasa, maana karibuni kutakuwa kumechelewa mno. Muziki wa mpinga-kristo unatia mtu usingizi. Msiukubali, lakini muukemee katika JINA la YESHUA MASHIAKH wenu.


Ishi katika utakaso, katika uadilifu. Ikiwa muziki uko dhidi ya hivi, basi ondoka, uondoke. Sikiza muziki ambao unainua, ambao ni Takatifu.


Wakati unasongea karibu wakati JINA la “YESHUA” Litaheshimika pekee na sio jina la “Yesu”. JINA la MASIA wenu ni Kiebrania, sio Kigiriki, au upotovu wake mwingine. Kwa hivyo NIsikilize, kwa maana MIMI URIYAH, Najua kilicho bora zaidi kwenu. NItumaini. Mbona muende Jahanamu au uangamize mwito wako kwa ajili ya wimbo ovu wa upotovu ambao unafurahisha mwili, masikio yanayowasha?


Kwa hivyo, siku hii, Watoto WANGU, furahieni Shabbat na mupumzike katika MIMI, YESHUA (Kutoka 20:8). Msikilizeni DADANGU wa MWANGAZA. Msihatarishe nafsi zenu kwa kile ambacho hakifaidi. Je, MIMI YESHUA Naweza sikiza muziki wa rap? Mnaweza fanya taswira MWOKOZI wenu, ambaYE ni MTAKATIFU na KWELI, Akisikiza muziki wa rap? Nawaambia la, maana SIkuruhusu wazo la dhambi kupita akilini MWANGU.


Mbarikiwe Watoto WANGU, na Kuweni Takatifu kama vile NDIMI NILIYE Alivyo Mtakatifu (1 Petro 1:16). Sela.



Mwisho wa Neno

10 views

Recent Posts

See All
bottom of page