Unabii 20 Ufunuo wa BINTI wa MUNGU, “URIYAH ni JINA LANGU!”
Updated: Mar 21, 2024
Umepewa Nabii D’vorah kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 10 Machi, 2019
Onyo!
Kabla ya kusoma, unaonywa kuwa huyu si mwanamke tu anayezungumza haya maneno. Ikiwa una tashwishi au unashuku hili Neno kuwa la YAH au la, usizungumze dhidi yake bali lipeleke katika maombi. Unaonywa pia YAHUVEH Alisema kuhusu kukufuru ROHO MTAKATIFU ni dhambi ya chukizo kuu ambayo haiwezi samehewa. HUYU ni BINTI wa YAHUVEH. Kwa hivyo unaonywa, ikiwa utazungumza dhidi YAKE, utakuwa unaweka nafsi yako hatarini. Nakuhimiza kutumia hadhari na nafsi ambayo YAH Amekubariki nayo na utafute Hekima kabla ya kuzungumza maneno yanayoweza kukuhatarisha na kukupeleka kwa moto wa Jahanamu milele. YAHUVEH ndiYE HAKIMU, si mimi, lakini lazima niwaonye la sivyo mimi mwenyewe nitawajibishwa. Kwa hivyo, tafadhali, usimpige mawe Mjumbe. Mimi ni msemaji tu na nazungumza ninachosikia kutoka Mbinguni. Ikiwa utazungumza dhidi ya Ujumbe huu, unazungumza dhidi ya MWENYEZI MUNGU WENYEWE!
Pia, URIYAH linatamkwa (OO-REE-YAH).
Maandiko Husika
Zaburi 45:13-17 “Utukufu wote una BINTI MFALME katika chumba CHAKE; vazi LAKE limefumwa kwa nyuzi za dhahabu. Anaongozwa kwa MFALME, Akiwa Amevalia mavazi yaliyotariziwa, Mabikira wenzake wanaMfuata na wanaletwa KWAKO. Wanaingizwa ndani kwa shangwe na furaha, na kuingia katika jumba la MFALME. Wana wenu watachukua nafasi za baba zenu, mtawafanya wakuu katika nchi yote. Nitadumisha kumbukumbu la JINA LAKO katika vizazi vyote, kwa hiyo mataifa wataKUsifu milele na milele.”
Mithali 7:4 “Mwambie HEKIMA, ‘WEWE ni DADA yangu,’ na uite UFAHAMU JAMAA yako.”
Mithali 31:26,29 Huzungumza kwa HEKIMA na Sheria ya wema iko ulimini MWAKE. … “Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini WEWE Umewapita wote.”
Yosefu na Asnati 15:7-8 “Maana TOBA YUmo Mbinguni, BINTI, mrembo zaidi na mzuri, wa ALIYE JUU SANA. Na YEYE MWENYEWE Anasihi MUNGU ALIYE JUU SANA kwa ajili yako nyakati zote na kwa ajili ya wote wanatubu katika JINA la MUNGU ALIYE JUU SANA, kwa sababu YEYE ni BABA wa TOBA. Na YEYE MWENYEWE (TOBA) ni Mlinzi wa Wanawali wote, na Anakupenda sana na Anaomba ALIYE JUU SANA nyakati zote kwa ajili yako na kwa wote wanaotubu Aliandalia mahali pa pumziko Mbinguni. Na Atawafanya upya tena, wote wanaotubu, na kuwatumikia YEYE MWENYEWE milele na milele. Na TOBA ni Mrembo kupindukia, Mwanamwali takato na hucheka siku zote, na YEYE ni raufu na mpole. Na, kwa hivyo, BABA ALIYE JUU SANA AnaMpenda, na Malaika wote wanaMstahi sana. Na MIMI pia, NaMpenda sana, kwa sababu YEYE pia ni DADA YANGU.”
Ujumbe wa Kinabii
(Kabla nisikie ujumbe ufuatao, nilikuwa nimewaza zamani ikiwa ABBA YAHUVEH na IMMAYAH wetu wana BINTI Mbinguni. Ikiwa familia ni mfano wa kile kilicho Mbinguni, si basi Wapendwa UTATU MTAKATIFU WAngekuwa na BINTI pia? Tuna YAHUVEH BABA, na IMMAYAH MAMA wetu Mbinguni, na YAHUSHUA HAMASHIACH ambaYE ni MWANA WAO, lakini je, BINTI? Katika mfano upi binti aliumbwa? Nilipokuwa nimeketi mezani na familia yangu katika YAHUSHUA, nilikuwa na maono ya ‘Mwanamke’ ambaYE Alikuwa MUNGU na hakuwa IMMAYAH! Nilikuwa nimesema maono haya kwa familia na sikuwa naenda kusema kile nilifikiri ilimaanisha kikamilifu kwa sababu ya kutotaka kuleta kikwazo kwa yeyote. Muda mfupi baadaye, nilisikia Neno lifuatalo kutoka Mbinguni kutoka kwa BINTI URIYAH ambaYE Alitaka kuJItambulisha kwa dunia kwa wakati huu.)
Kutoka kwa mdomo wa mashahidi wawili au watatu NENO LANGU linaimarishwa. Manabii WANGU, inamisheni sikio lenu kwa sauti YANGU!
MUZIKI, MIMI ni MUZIKI. MIMI ni MUZIKI. MIMI ni … Nena katika imani, Binti WANGU! Nachukia dhambi! NIsifu! NItafunua zaidi. MIMI ni MUZIKI! MIMI ni ROHO wa UNABII! MIMI ni MUZIKI unaotoka kwa MAMA. NIsifuni Wapendwa WANGU!
NItafunua zaidi kwenu. NInanong’oneza katika kila sikio lenu. Nawazungumzia ufunuo ambao bado haujafunuliwa ambao umefungiwa katika Kitabu cha Danieli. Kwa maana Danieli hakujua kuNIhusu.
ROHO ya UWAZI!
ROHO ya UNABII!
ROHO ya MUZIKI!
ROHO ya HEKIMA!
Hizi zote zinapatikana ndani YANGU! Ee, NIsifuni na NItafunua zaidi!
Ee muhibu WANGU, NImefunua na NItakufunulia zaidi kuhusu BINTI WANGU. YEYE pia ni ROHO ya UNABII.
Maana NIna BINTI na MWANA!
MIMI, YAHUVEH, na MIMI, IMMAYAH, Twanena sasa!
EZRA, lazima Ufunike Watoto WAKO wanapopokea ufunuo hizi. Kwa maana hizi ni siri ambazo shetani hakuwahi taka zitoke kwa Chumba CHANGU cha Kiti cha Enzi. Lakini ee, EZRA, NImeKUfunulia pia mbeleni Ukiuliza, “ABBA YAHUVEH, IMMAYAH wana BINTI?”
Ndiyo! Ndiyo, MWANANGU! NDIMI NILIYE na ni MIMI NInaYEzungumza naWE.
MIMI NDIMI NILIYE!
YAHUVEH ni BABA YANGU!
YAHUSHUA ni KAKANGU!
IMMAYAH ni MAMANGU!
Kwa maana SISI, UTATU, TUna siri nyingi. Ee, Wapendwa! NImewatazama nyote. NImo kifuani mwa BABA YANGU. NImeishi ndani yake. TUnajuana vizuri zaidi kuliko nyote mnavyojua. Hamkumbuki tu.
NIlipowatuma kwa hii dunia, BABANGU Aliposema, “Nenda!” – mlienda; siri kutoka Mbinguni zimefutwa kutoka kwa kumbukumbu yenu. Lakini zimehifadhiwa katika chembe za mafuta, na NInarejesha DNA yenu. Mnapokunywa hayo maji msikadirie pungufu uweza huu!
MIMI ni MOTO!
Kwa maana MIMI na MAMANGU HEKIMA, MAMA yenu SHALOM, IMMAYAH wenu, SISI ni MMOJA na SISI ni MOTO MTAKATIFU!
MIMI ni MUZIKI. Mnaposifu, NIko hapo. Ikiwa mtajua au msijue. NIko hapo.
NIulize Nikuguse ili usifu BABA YANGU, kuNIsifu MIMI, kusifu YAHUSHUA, kusifu MAMANGU IMMAYAH!
Msiwe na tashwishi Watoto WANGU. MIMI ni DADA yenu! MIMI ni MWENYEZI MUNGU! MsiNIweke katika bweta. Msiweke ELOHIM katika boksi, kwa maana SISI NI ELOHIM!
TUnatawala katika Umoja. SISI, UTATU MTAKATIFU na MIMI!
Msifikiri tu kwa sababu macho yenu hayajaona na masikio yenu hayajasikia kwamba SIko. Mnataka ukamilifu wa upako? Kwa hizi siku 40 zinazofuata, hizi siku 40 za mwisho kabla NIwabadilishe, mlihitaji huu ufunuo!
Nyinyi wanawake (MUNGU Azungumza na mabinti WAKE) – Nitawafunulia zaidi. Pokea Maji Yaliyo Hai moja kwa moja kutoka kwa Kiti cha Enzi cha MAMA YANGU!
NIna Kiti cha Enzi pia, mwajua! NIna Kiti cha Enzi, pia. Na kiko pale karibu na MAMA YANGU. Mwafikiri mfano wa binti unatoka wapi?
Puliza Binti! Puliza ufunuo kwenu. (Anapuliza kote mezani) mara 4 na 1 kwa ajili YANGU.
URIYAH!
URIYAH ni JINA LANGU!
Unashangaa mbona umesikia ‘URIYAH’, kwa maana hili ni kike. URIYAH! Binti, umesikia jina hili wiki iliyopita tena na tena! Na la, la, la, sio kwa sababu ya mwanamme yeyote – na ingawa Nakupenda mwanaNGU – Nilikuwa Namwonyesha mapema ili NIweze kuleta huu ufunuo na NIliweka katika ndimi zilizo katika mdomo wake na NIkaamsha upako wa Unabii, ili nyote mweze kushahidi huu ufunuo! Ili nyote muweze kufunuliwa. Na hati-kunjo ambazo NImewapa – msifikiri kwamba hazina sehemu yoyote ya hili. Hivyo ndivyo jinsi ni muhimu kupokea hizo hati-kunjo ambazo zinatoka moja kwa moja toka Mbinguni, kutoka kwa Chumba cha Kiti cha Enzi.
MIMI, YAHUSHUA, Nazungumza sasa, na ya MIMI, BABA YAHUVEH, na ya MIMI, IMMAYAH. Mbarikiwe Watoto WANGU! Pokea huu ufunuo! (Wote walisema, ‘Naupokea!’)
Ni nyinyi pekee Nimefunulia hili katika dunia nzima. Hii ndiyo maana mnapaswa kufunika dada yenu na nyinyi nyote mnafaa kufunika wenzenu!
Huu si mchezo! SIzungumzi tu kuzungumza. Mnadhubutu vipi kuNIsaili? Yeyote kwenu, msiNIsaili! Msisaili! Maana kwani hili halitoshi, maono, ufunuo, ndoto, haya yote ambayo NImewaonyesha hadi sasa.
Nawapenda! Napenda kila mmoja wenu! Nyinyi ni Kaka WANGU na Dada ZANGU. Lakini MIMI ni MWENYEZI MUNGU wenu. Msisahau hili. Napaswa kustahiwa.
Ufunuo nyingi mno, siri nyingi mno Nitakufunulia binti. Kwa wanaume WANGU wote wanaokaa kwenye hii meza, na zaidi kabisa kwa EZRA WANGU!
EZRA, Nakupenda! NIliKufunulia kwanza! Hili limo kwenye hati-kunjo. Na kumbuka Binti maono uliona, ya hati-kunjo, ambapo hati-kunjo iliwekwa katika mfuko WAKE wa nyuma wa mabawa YAKE. Hili ndilo NIlitaka kufunua, hiyo ndiyo maana maono hayo yalibainika kwako.
NInapowaonyesha maono Watoto – kuwa wangalifu! Tena, SIzungumzi tu kwa minajili ya kuzungumza! Lakini siri kuu, kuu zimefungiwa na kutiwa muhuri, tayari kufichuliwa ikiwa tu mtasikiza, ikiwa tu mtaelekeza sikio lenu KWANGU!
Maana hii ndizo siri zilizofungiwa katika kitabu cha Danieli. Lakini Danieli, hata yeye hakujua huu ufunuo. Alijua nyingi.
Zimehifadhiwa katika Chumba cha Kabati Mbinguni. Kimelindwa kabisa na Malaika WANGU Shujaa wa juu, Batalioni.
Vita vinavyopiganwa katika mbingu juu ya ufunuo huu… Oh! shetani anaogopa na anajua kwamba dunia inatingika na kutetemeka sasa kwa Wana [na Mabinti] wa ELOHIM Waliodhihirika! Oh, dunia inatingika na inatetemeka! Na milima inatetemeka kwa sababu haiwezi zuia MIMI, BWANA MUNGU MWENYEZI, kunena ukweli WANGU – hata katika hizi nyakati za mwisho, katika kipindi cha giza zaidi!
[wa]mejaribu kushinda na kufunga mawimbi ya redio, kufunga ufunuo WANGU, kuNInyamazisha katika kila njia – JINA la MUNGU MWENYEZI kunyamazishwa katika fedha ZANGU! Uavyaji mimba – mamilioni juu ya mamilioni ya wenye bado hawajazaliwa ambao wanamwagishwa damu ili kuzuia Washika Amri WANGU. Hii ndiyo maana ukatili huu unaendelea. Ni kuabudu Baali, ndiyo, lakini pia ni kuwa kama silaha dhidi ya Watakatifu WANGU!
Hamjui Watoto WANGU jinsi shetani anawapiga vita sasa hivi. NImewaweka katika ulinzi mkali. NIna mamilioni ya Malaika – kundi za manowari za juu kabisa za Malaika WANGU Wapiganaji kando yenu. NImewaweka katika ulinzi [mkali] na kupiga muhuri na Upako WANGU wa Dhahabu.
Wakati unaTUpokea sote SISI 4, unapokea ulinzi WETU mzima. UnaTUpokea!
Ee, EZRA, NItaKUchukua haraka sana. Ee, bado Natuma wale farasi wenye rangi nzuri. Zawadi nyingi mno NImezihifadhi MWANANGU. Mnafikiri hiki ni kitu Watoto WANGU… Oh, NIna hata zaidi kabisa!
Uko sahihi binti, akili zenu hazitaweza kushika ujazwaji zaidi kupita kiasi ambacho MIMI, YAHUVEH, Naenda kuweka ndani ya kila mmoja wenu. Mtahitaji miili iliyokomaa, mtahitaji akili mpya! Wafunuaji, Wafunuaji, Wafunuaji, NItawaita Mbinguni! NItawafunulia siri kuhusu EZRA WANGU ambazo huu ulimwengu hautawahi jua.
Hamjui BABA yenu ni nani! Maana Alijua wakati huu wote katika Roho YAKE, labda sio kikamilifu akilini MWAKE, lakini Rohoni MWAKE. Kwa maana vitu hivyo vyote vimefungiwa katika Roho YAKE, na Alipokuombea binti, Roho ya UNABII iliachilia kutoka Roho YAKE – kama tu NIlivyotumia Manabii WANGU na kama vile tu Naenda kufanya na nyinyi nyote. Ipokeeni!
Ee Nawapapasa nyinyi nyote, ee, Nawashika nyinyi nyote! Mko katika blanketi ya ulinzi ya MIMI, IMMAYAH na MIMI, URIYAH! Kike 2 si ni bora kuliko 1? Kwa maana TUnafanya kazi katika umoja na mnaona jinsi WAnyenyekevu SISI Wanamke TUlivyo – na SIsemi SISI ni wanadamu, la, la. Lakini je, mwaona jinsi nyenyekevu mwanamke wa hii dunia ameitwa kuwa? Ona jinsi kwa muda gani NImengojea kufunua – hadi mwisho kabisa. Kwa maana SISI ni Kike.
TUfuateni, enyi wanawake wa ELOHIM, fuateni mfano WETU!
Kwa maana SISI TUmejiweka chini na tu Wapole. SISI ni Waraufu.
Yezebeli, Yezebeli, oh jinsi Navyochukia Yezebeli! NItaangamiza Yezebeli kukupitia wewe binti WANGU, kukupita wewe pia binti WANGU!
Nyinyi 2 mtatumika! NItatumikia mabinti WANGU kuangamiza madhabahu za Baali! Kufikicha, kufikicha, kufikicha chini utaenda! Kufikicha chini utaenda. Mnara wa Babeli – anguka, anguka, anguka, anguka chini! Oh unadhubutu vipi kuiba Utukufu WETU!
Ee, wewe mchawi Yezebeli! MIMI, IMMAYAH, MIMI URIYAH, Nakukemea!!! Naja na Moto WANGU! NItakuchoma! NItakuunguza! Naja kuchukua kisasi kikubwa juu ya Yezebeli!
E, mwanamke wa hii dunia, tetemeka na utikisike katika hofu wewe ambaye umechukuliwa na roho ya Yezebeli. Upanga [wenye ncha mbili] utadunga dunia na hii ndiyo maana uliona hayo, [hayo maono] binti WANGU akichopoa upanga huo! Kwa maana hii ni kuua hiyo roho ya Yezebeli na Upanga WANGU wenye ncha mbili wa ROHO – na Neno LANGU Takatifu! Upepo Mtakatifu NInapuliza juu yako! Juu yako binti! Juu yako pia binti! (Anapuliza) Oh, NInawapenda sana!
Ee, URIYAH ni JINA LANGU! NIpokeeni kwa moyo, Watoto WANGU Wachanga, Wachaguliwa WANGU, Wateuliwa WANGU!
Oh mpendwa WANGU, haujui lakini MIMI tayari NInauhusiano na wewe! Kwa sababu unaona, wakati NIlikufunula mwana WANGU, ulipokea. UlipoMpokea kwa moyo IMMAYAH WANGU, uliNIpokea MIMI kwa moyo! Asante mwanaNGU! Asante EZRA! Asante Watoto WANGU Wapendwa!
Oh binti WANGU asante kwa kuNIlipia gharama MIMI, ya ufunuo huu! Ulishangaa kwa nini uliteseka – hii ndiyo maana. Ili NIweze kuzungumza kukupitia wewe binti WANGU.
Yezebeli! NItakuangamiza wewe Yezebeli! Msisahau hili Mabinti WANGU, mnafaa kufanya vita dhidi ya Yezebeli. NIulizeni cha kufanya! NIulizeni jinsi mnapaswa kusonga! Msiwahi kirimu [karibisha] hii roho! Hata katika hila/kujificha kwake! Imejaribu kuwavuta nyakati zingine, lakini mnasema: “La, la, la, la shetani! Nakupinga, roho ya Yezebeli! Sitakuwa mwanamke mtongozaji! Sitakuwa katika kukosa kujitiisha!” msiwahi karibisha roho ya Yezebeli, maana Naja kuwatumia mabinti – Naenda kuwatumia kuangamiza madhabahu ya Yezebeli, madhabahu ya Baali!
Kwa hivyo jitayarisheni Mabinti WANGU, hii ni sehemu ya ufunuo. Na zaidi ya mnayoNItafuta pamoja – sikizeni Mabinti WANGU – zaidi ya mnayoNItafuta pamoja, katika umoja, umoja kamili: bila wivu, bila mashindano, mafananisho, bila chuki, bila machungu, umoja kamili NInadai! Kumbatianeni zaidi! Pendaneni zaidi! Kuweni walinzi wa kila mmoja wenu, rafiki wa dhati wa kila mmoja wenu! Mnahitaji kila mmoja wenu!
Ee Mabinti WANGU, je, bado hamuelewi kile Nataka, kile NInanuia, kile MIMI YAHUVEH Nataka kuwatumia? Nataka hili Mabinti WANGU.
Na sasa Natumia URIYAH WANGU!
Na sasa MIMI, YAHUVEH, Nazungumza! Kwa maana HUYU ni BINTI WANGU!
Natumia BINTI WANGU kuenda kote duniani!
Anataka kuchukua kisasi juu ya roho ya Yezebeli! Anahitaji chombo! Mnasema, “Niko tayari!” Mnasema, “La Yezebeli, hautakuwa na sehemu ndani yangu!” Mnasema, “Nitatumika kuangamiza hizi madhabahu ya Baali!” NInasema, “Raka!” Sema, “Raka!”
Sisimkeni Watoto! Kwa maana huu ni Mwondoko NInaanzisha leo!
Kwa hivyo kuwa tayari, shetani! Kwa maana NInainua kikundi CHANGU cha Wapiganaji Aali! Inuka, binti WANGU! Ee, shetani aogopa hili! “Hakuna silaha, hakuna silaha, hakuna silaha, iliyotengezwa dhidi yetu itakayofanikiwa!” ni kile mnapaswa kusema. Na ‘Torah Keeper’ [Mshika Torah], NInapopuliza sasa itazame ikienea kama moto wa mwituni! Je, mnapokea na kuamini? (Wote walisema ‘Ninapokea na kuamini’) (Kupuliza upepo) Nyinyi nyote pulizeni! (Wote wanapuliza).
URIYAH, URIYAH, MIMI URIYAH, Nawaambia – tumeni Vitu vya Asili vya Kiroho! Binti YANGU unapopuliza, NInapuliza UPEPO WANGU MKUU!
Ee mwanaNGU, NInakufunulia katika Maktaba ya Mbinguni, kama vile tu NInavyo kwa dada na kaka wako! Msikadirie pungufu hii Maktaba! Kile MIMI MELEKH TSEDEK (Melkisedeki), Nawaonyesha hakifai kukadiriwa pungufu! Ee mwanaNGU, kile NInakufunulia na hata sasa, MIMI MELEKH TSEDEK, Nasimama hapo na kukupa! Uko chini ya hayo Maporomoko ya Maji MwanaNGU!
Katika Maktaba hayo kuna Maporomoko ya Maji! Hakikisha uende pale kila asubuhi kufanywa mpya! Na nyinyi nyote mnaweza NIuliza kuenda chini ya hayo Maporomoko ya Maji. Mpendwa, uko pale, NIlionyesha dadako hili. EZRA Anabaki hapo. Mnaona, EZRA Amepandwa hapo. Rusu YAKE inabaki hapo, rusu YAKE imepandwa tu.
Mnajua kwa nini shetani alianguka? Mliwahi waza kuhusu tamaa? Mliwahi waza kwa nini shetani alianguka? Mliwahi waza ikiwa aliNItaka MIMI?
BABA YANGU YAHUVEH Hakuruhusu hili!
Lakini EZRA, WEWE ni wa pekee! Maana Unaingia na kutoka kwa moyo wa BABA YANGU na haulizii abadani zaidi ya kile BABANGU AnaKUpa! Kwa maana WEWE si mwenye wivu, WEWE si mwenye tamaa, Umeridhika kikamilifu na kila kitu BABA YANGU AmeKUpa, na Utakuwa hivyo sikuzote EZRA, maana WEWE ni BiArusi Mkuu wa BABA YANGU!
Kwa maana MIMI, URIYAH, NImezungumza.
Itieni chini Watoto WANGU.
Mwisho wa NENO
Mahabubu URIYAH,
WEWE ni DADAngu mgeni. WEWE ni MUNGU wangu na ninafurahia sana kuKUjua. Ninafuraha sana kujua kwamba YAHUSHUA ana DADA MAPACHA na kwamba NYOTE ni MMOJA na Mnapendana sana! Jinsi Ulivyo wa thamani sana na wa kipekee URIYAH, KIPENZI changu! URIYAH, njoo, njoo kwangu! Nikumbatie leo! Ninakukubali na moyo, akili, mwili, roho, na nafsi yangu yote! Mimi ni WAKO pekee ABBA YAHUVEH, YAHUSHUA, IMMAYAH, URIYAH, MELEKH TSEDEK!!! URIYAH, Ulinena nami baada ya hili Neno na Ukasema jinsi Tulivyokaribu Mbinguni. NinaKUpenda sana. Hili ni tangazo langu la upendo KWAKO BINTI wa ELOHIM. BINTI MFALME Mrembo wa Mbinguni! Nataka kuwa tu kama WEWE! Ninaweza husiana na WEWE kama Binti na ninaKUtazamia sana na nataka kuKUjua zaidi na zaidi na zaidi. NaKUpenda na nahitaji kuKUjua! Nahitaji kuKUjua ee MPENZI wangu wa DHATI URIYAH! Nahitaji kuKUona na nitaKUpenda kwa siku zote za maisha yangu hadi milele yote! Nitafanya kadri niwezavyo kuKUlinda na kuvunja madhabahu ya Baali na roho ya Yezebeli, kwa sababu najua hili ndilo Unataka! Mimi ni WENU! Sitawahi WAondoka na ee jinsi gani nataka kuWApendeza pamoja na yote niliyo mimi! Mna BiArusi pia! Tafadhali nihesabuni kuwa mstahili wa kuitwa BiArusi WAKO, pia wa YAHUSHUA! NInaKUpenda na ule uwazi nilikuwa nao wa dada na maumivu ambayo nimehisi kutoka kwa wanawake maisha yangu yote sasa yameponywa kwa sababu YAKO URIYAH MPENDWA wangu! Sitauliza kama ninapendwa kwa sababu sasa nina BABA, MAMA, KAKA, na sasa DADA! Naweza uliza nini zaidi? Asante sana kwa kunichagua mimi kwa ajili ya ufunuo huu. Ninakuahidi nitatota hili nje kwa Watu WAKO na naKUpenda na upendo wa milele siku zote za maisha yangu. Ikiwa wengine wataKUumiza, nitaKUtetea na ukweli WAKO. WEWE ni Mzuri wangu.
Upendo daima,
Binti YAKO, dada YAKO na WEWE ni MUNGU wangu. WEWE ni BINTI MFALME wa Mbinguni na ninaKUstahi WEWE KIPENZI changu!