Unabii 19 MIMI, MELEKH TSEDEK, NIna Utaratibu Ndani ya Utaratibu WANGU na Viwango Ndani ya Viwango Vyangu!
Updated: Apr 13, 2024
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umeandikwa 8 Machi, 2019
Maandiko Husika
Mwanzo 14:18-20: “Ndipo MELEKH TSEDEK Mfalme wa Salemu Alipoleta mkate na divai. Alikuwa Kuhani wa EL ALIYE JUU SANA. Naye Akambariki Abramu, Akisema, “Abarikiwe Abramu na EL ALIYE JUU SANA, MUUMBA wa mbingu na nchi. Abarikiwe EL ALIYE JUU SANA, ambaYE Amewaweka adui zako mkononi mwako.” Ndipo Abramu akampa MELEKH TSEDEK sehemu ya kumi ya kila kitu.”
Waebrania 5:5-6: “Pia MASIA hakuJItwalia utukufu YEYE MWENYEWE wa kuwa Kuhani Mkuu, bali Mungu AliMwambia, ‘WEWE ni MWANANGU; leo MIMI NImeKUzaa.’ Pia mahali pengine Asema, ‘WEWE ni Kuhani milele, kulingana na utaratibu wa MELEKH TSEDEK.’”
Ujumbe wa Kinabii
NIng’arie MIMI! Ee NIsikizeni na acheni nuru yenu ing’ae! Acha mng’aro wa MUNGU wenu, hata MUNGU WANGU, uinuke juu yenu (Isaya 60:1-3). Na mjazwe na nuru ya ALIYE JUU KABISA na muingieni chini ya ulinzi wa mbawa ZAKE. Kwa maana bado muda kidogo tu na ghadhabu na hamaki YAKE zitapita.
Jificheni katika Hekima ya ALIYE JUU KABISA – MWENYE Mbingu na Dunia – MIMI, MELEKH TSEDEK (Melkisedeki), Nazungumza. Msijifiche katika hofu ya yale yatakayokuja au yanaweza fanyika au yale mtakayosikia. Kuweni wenye bidii, kuweni haraka. Tilieni maanani njia ZANGU na hamtatoka nje ya utaratibu, nje ya viwango. Kaeni katika umoja na MIMI.
Tembeeni pale Nasema tembea. Kimbieni wakati Nasema kimbia. Jificheni NInaposema jifiche. Mtakuwa salama mradi mnatii, mradi mtii. Juhudi lenu lipasalo ni kufanya kila kitu Nawaamuru (Mhubiri 12:13). Kila kitu Nawaamuru ni ‘ndiyo’ na ‘amina’ (2 Wakorintho 1:20). Kwa hivyo NIsikizeni kwa bidii pamoja na kila pumzi NInayochukua, mnayochukua.
MIMI MELEKH TSEDEK, NIna utaratibu ndani ya utaratibu WANGU, viwango ndani ya viwango VYANGU – kila kitu stahifu na katika utaratibu (1 Wakorintho 14:33). Kila kitu katika wakati na msimu wake kamili – utaratibu bila kukawia. Sichukui amri. MIMI, MELEKH TSEDEK, Napeana amri. Kumbuka MUNGU ni nani. Kumbuka MUNGU ni nani na mtastawi. Ni rahisi sana Watoto WANGU. Vijisababu vinatatiza mambo, tatiza jambo.
MtaNIona, Watoto WANGU. MtaNIona na kuNIpa Utukufu na Heshima mnapoona njia ZANGU zilizo za neema na wingi wa huruma kwenu – zawadi kutoka kwa BABA. Afadhali NIwe na huruma kuliko hukumu, heri huruma kuliko hukumu (Mathayo 9:13). NItafunika macho YANGU katika majonzi na huzuni kwa yale yatakayotendeka, kwa yale lazima yatendeke.
Je unafikiri MIMI, YEHOVAH, Napenda kuona uangamizi wa waovu? Ndiyo, Natamani kuisha kwa uovu, lakini NIngetaka kwamba waovu watubu na wachague maisha – hiki ndicho kilio cha moyo WANGU, kwa maana sio hii sababu MUNGU Alituma MWANAKE wa Pekee, maana Alipenda sana dunia (Ezekieli 33:11, Yohana 3:16)? Naam, MIMI YEHOVAH, ni Upendo; lakini kumbuka, NDIMI NILIYE pia Amesawazika na vita – KUU ni JINA LANGU (Kutoka 15:3)!