top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 90 “Ee Israeli, Msikatae DAMU na MAJI!”

Updated: Mar 23, 2024


Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umepokewa 22, 24 na 31 Oktoba, 2020



Maandiko Husika


Kumbukumbu 10:15-17

15 Hata hivyo YEHOVAH Alikuwa na shauku na baba zenu pekee, Akawapenda

na Akawachagua ninyi, wazao wao, kuliko mataifa yote, kama ilivyo leo.

16 Kwa hiyo tahirini mioyo yenu, na msiwe na shingo ngumu tena.

17 Kwa kuwa YEHOVAH MUNGU wenu ni MUNGU wa miungu na

BWANA wa mabwana, MUNGU MKUU, Mwenye uweza na wa kutisha,

ambaYE Hana upendeleo na Hapokei rushwa.


Mhubiri 12:13-14

13 Hii ndiyo jumla ya maneno;

yote yamekwisha sikiwa:

Mche MUNGU, nawe uzishike amri ZAKE,

maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

14 Kwa maana MUNGU Ataleta hukumuni kila kazi,

pamoja na kila neno la siri,

likiwa jema au baya.


1 Yohana 5:8

Pia Wako Mashahidi Watatu duniani]: ROHO,

MAJI na DAMU; Hawa Watatu Wanakubaliana katika umoja.


Ujumbe wa Kinabii


Uko na ndevu za Baba yako. Hekima inapatikana katika ndevu. Siri kuu zimetiwa ndani. NItafute ukitaka kujua Zaidi. Haijalishi urefu wa ndevu (kimwili), kwa maana hili ni la kiroho. Hili si la kimwili bali ukweli.


NIna njia ZANGU katika mawingu, mbinguni juu, katika dunia chini. Hakuna mahali ambapo SIna njia ZANGU. Hata katika jahanam chini (Nahum 1:3-5). MIMI NImejaribiwa na Mkweli lakini SIna hitaji la kuthibitishwa. MIMI ni MUNGU MWENYEZI, BWANA wa Mbingu na Ardhi. Sujuduni mbele ZANGU, ee Dunia! Pigeni magoti! NItafuteni katika njia ZANGU zote na sio katika njia zenu. Njia ZANGU zimejaribiwa na ni kweli. Njia zenu ni za kupotoka na kufedhehesha, za karaha (Luke 16:15). Kwa maana wapi utakatifu?!


Hamjui kuwa urafiki na hii dunia, hiki kipindi cha sasa ni uadui na MUNGU?! Kwa hivyo takaseni mikono yenu enyi watenda dhambi (Yakobo 4:4-8). Msitazamie yaliyopita, njia za zamani za mwili. Ule utu wa kale lazima usulubiwe (Warumi 6). MIMI, YEHOVAH, Natoa amri hii! Hakuna yeyote wa kimwili anayeweza kurithi Ufalme wa UTUKUFU WANGU. Lazima uwe takatifu (1 Petro 1:13-16). Lazima utengwe. Lazima uwe kweli.


Njoni kupitia DAMU ya YESHUA. Njoni kupitia DAMU ya MWANAKONDOO, kwa maana kupitia hili pekee unaweza kutakaswa, unaweza fanywa huru (1 Yohana 1:7).


Msikatae maji ya METATRON. Msikatae Ukweli WAKE. Anakuja Amebeba Injili ya matayarishp ya Amani (Isaya 52:7). Anakuja Akitegemeza MWANA MFALME wa AMANI, SAR SHALOM.


WAnakuja WAkiwamebebana – ALEF na TAV (Ufunuo 1:8).


MsiNIsahau katika manufaa YANGU yote (Zaburi 103). Wakati NInapomwaga manufaa YANGU yote, baraka ZANGU juu yenu, msiNIsahau (Kumbukumbu 8). MIMI, YEHOVAH, Nafanya Dunia izunguke Jua. Ni MIMI pekee NInaYEjua nyota na njia ya siri zinazosafiri. Wewe ni nani, ee mwanadamu?! Wewe ni nani kusema kile NDIMI NILIYE Anaweza na Haweza kufanya?! NItakutunduwaza. NItakufanya uonekane mjinga. Watu WANGU wanaangamia kwa kukosa maarifa, kwa maana wamegeuka kutoka KWANGU MIMI (Hosea 4:6). Si tofauti na siku za zamani.


NIgeukieni, ee Israeli. Kusoma kwingi kunachosha mwili na kunawezadhuru nafsi kusipofanywa katika roho nzuri (Mhubiri 12:11-13). Acheni MIMI, “NDIMI NILIYE’ MKUU, NIwaongoze, NIwaelekeze, NIwafundishe. Acheni NIwaonyeshe njia kweli na adilifu, njia ambayo mababu zenu wa zamani walijua. Naja kufunza, lakini ni nani atasikiza? Acheni NIwafanyie hukumu iwe tamu.


Ee Israeli, kama hii ndiyo mipango NInayo kwa ajili yenu – mipango ya amani na sio uovu, mipango ya maji na uzima, sio mauti (Yeremia 29:11-13). Kwa hivyo mbona mnageuka kutoka KWANGU MIMI, ee Yakobo? Mbona mnarudi nyuma, ee Israeli? Naja kuwafanya wapya, kuwafanya wazima tena. Ni kweli Siwezi tazama dhambi. SIidhinishi matendo ya mataifa. SIwaidhinishi nyinyi, Israeli, kwa maana mmegeuka kutoka kwa njia ZANGU na kuleta aibu kubwa kwa JINA LANGU. JINA LANGU ni UTAKATIFU na vivyo hivyo yapaswa mwe, watu wanaoitwa kwa JINA LANGU, kwa Torah YANGU.

Kwa hivyo geukeni kutoka kwa njia zenu za uovu na mrekebishe matendo yenu. NInaangalia kwenye moyo. Mtararua moyo wenu (Yoeli 2:12-13)? Je, mtatahiri govi la moyo wenu (Yeremia 4:3-4)? Mtafanya nini? Nawapa chaguo aidha uzima au mauti. NIjue MIMI na mjue uzima. Mtafanya nini?


NImekuwa mvumilivu. NImekuwa mwenye huruma. NImezuia mpango wa shetani kwa muda mrefu sana. Lakini mmefanya nini na muda ambao NImewapa? NInawatazama, ee Israeli. Macho yenu yanaangazia nini? Macho yenu yanatazama nini katika saa za usiku? YEHOVAH Asipokuwa kwa ajili ya mji, mlinzi analinda bure (Zaburi 127:1). Je, wewe ni mlinzi wa ndugu yako au unajilinda tu ya kwako? NInawajaribu. NInawajua.


Tazameni, ee Israeli! Hampendezi machoni MWANGU na kwa hili mtakunywa mara dufu kwa ajili ya dhambi zenu (Yeremia 16:18). Mtaona hofu kuu na tisho, kwa maana mnakaza macho kwa utulivu kupitia tamaa za mwili kila mmoja baada ya mke wa jirani yake, baada ya cha jirani yake. NInajua jicho la tamaa ambalo mnatazamia (Yeremia 17:9-10). HamNIpendezi, ee Israeli. MIMI, YEHOVAH, NImechoshwa. Uvumilivu WANGU umeisha na saa yenu ya kulipia makosa i karibu. Hiyo ndiyo maana NInatuma METATRON WANGU na kumi na nne WANGU. Mtawajua. Mtawatambua.


Lakini hamtapenda kile mtaona, kwa maana watakuja kusadikisha, kuwajaribu katika njia zenu zote. Hata kama vile chuma kinajaribiwa katika tanuru, vivyo hivyo pia watawajaribu, ee Israeli (Yeremia 6:27). Msigeuze uso wenu dhidi YANGU. Msitelekeze siku ZANGU takatifu, kwa maana kuzipitia mtajua MIMI NDIMI NILIYE na HAKUNA aliye kama MIMI. EHYEH ASHER EHYEH (Kutoka 3:14). Msitazame ushauri wenu bali tafuteni WANGU, kwa maana nyayo zenu zitawapotosha, [zita]waelekeza jahanam.


Nataka kuzungumzia kuhusu Hahukkah, jinsi makuhani walijitwalia bila haki mamlaka YANGU. Wahasmonea, Wahashmonaim NIliheshimu. Kwa muda na msimu NIliwapa mamlaka lakini sio kusahau MTAWALA wao wa haki. WaliNItelekeza. Kuhani akawa mtawala, lakini je, vipi kuhusu Kabila la Yuda? Vipi kuhusu ukoo, urithi? Taji la mfalme halipitii ukoo wa Lawi bali wa Yuda (Mwanzo 49:8-10). Ee usaliti mwingi, uharibifu mwingi ungeepukwa!


Mbona mfanye mapatano, mfanye maafikiano na shetani? Nani alileta Roma katika Israeli? Haikufaa kuwa kamwe! Haikufaa kuwa kamwe! NInaruhusu kile NInaruhusu, kwa maana kuna matokeo ya dhambi, ya nia mbaya. Je, mnaona kile kinachofanyika watoto WANGU mnapotafuta uso wenu wenyewe, mnapotafuta mapenzi na njia yenu wenyewe? Maafa. Mnakutana na maangamizi (Mithali 14:11-12). Mnakaribisha ndani adui wa nafsi yenu.


Israeli, makuhani hawakutafuta mapenzi YANGU bali faida ya kisiasa. Na sasa Roma ina mkono katika kila kitu. Wao ni baka, baa kwenye nchi. Fuata Utaratibu WANGU na utawakamilisha. Fuateni Njia YANGU na haki mtarithi.


Kuweni hiyo nchi inayotiririka na maziwa na asali tena. Kuweni hiyo nchi iliyo na maji yanayomwagika kutoka kwenye jiwe. Ee, laiti haki ingeinuka kama jua la mchana wa kati, kama tufani la jicho LANGU (Zaburi 37:6)! Lakini sasa upotovu ndio yote Naona. Uovu ndio lugha, sheria ya nchi. Mtavuna kile mnapanda, ee Israeli, na mmekuwa [mkivuna] (Wagalatia 6:7-8).


Hadi mlie, “Mbarikiwa ni YEYE AjaYE katika JINA la BWANA!”, hadi mruhusu WAFALME wa UTUKUFU kuingia, hamtakuwa na utukufu wenu wenyewe. Mtabaki uchi na hawinde, kwa maana je, SIkusema nyumba yenu mtawachiwa hame (Luka 13:35)?!


Ee jinsi Danieli anapaza sauti na kuwalilia! Manabii wote wa kale wanawalilia! Kati ya baraza na madhabahu wanapaza sauti, “Ni lini Israeli itarudi? Ni lini MASIA Atarudi? HAKADOSH BARUKH HU.” NInatimiza Neno LANGU, kwa maana halitarudi KWANGU bure (Isaya 55:11). Je mnatimiza lenu, ee Israeli? Kipi kilikuwa kiapo mlichoapa KWANGU jangwani, katika jangwa la Sinai? Kufuata na kushika njia ZANGU katika matendo yenu yote (Kutoka 24:3,7). Na bado katika matendo yenu yote mmekuwa wapi? Ingawa Maneno YANGU yamo mdomoni mwenu, tafakari za mioyo yenu iko mbali naMI (Isaya 29:13). Uongo! Kashfa!


NIpe ukweli! NIpe Waadilifu, kwa maana Najua Njia yao na wanaNIjua (Zaburi 37:23). Nchi inayokaa katika giza imeona mwangaza mkubwa, maana Nyota ya Mchana imeinuka juu yao. Na Atakuja na mafuriko ya kupita kiasi kutakasa nchi, kutayarisha njia, kutengeneza njia kwa ajili ya MFALME. Tayarishieni MFALME! Tayarisheni barabara kuu mbele ZAKE! Wekeni njia YAKE takatifu! Msitelekeze Chemichemi za Maji ya Uzima (Yeremia 2:13)! Msitelekeze vijito vilivyo jangwani!


Bahari ziko mbele zenu, ee Israeli. Bahari za chemichemi za kina. Msitelekeze Njia YANGU. Msikosee katika neno, tendo au fikra. Tafuteni amani na binadamu wote kiasi cha uwezekano lakini msitelekeze Torah, mwangaza uongozao (Zamburi 119:105).


Kila mashine ina mwongozo wake. Je, ni uzushi kufuata maagizo yake? Vivyo hivyo pia maisha yana mwongozo wake, mwelekezo wake. Na NIngependa kwamba mchague uzima na sio mauti (Kumbukumbu 30;19-20). NItafuteni katika jinsi ya kutumia Torah. Angalieni kwa makini na mfuate YESHUA, kwa maana Hakukosea katika nukta au herufi moja ya Sheria. Hakuja kufuta Sheria na Manabii, bali kutimiza (Mathayo 5:17). Kwa hivyo msiamini uongo kwamba MASIA wenu sio Mkweli, Hayuko kwa ajili yenu. Alizaliwa Myahudi. Alikufa Myahudi na kufufuka Myahudi. YEYE ndiYE UFUFUO na UZIMA wenu (Yohana 11:25-26).


Msitelekeze Chemichemi za Maji ya Uzima! Msitelekeze kile kilicho kweli – ALEF na TAV. WAO ni WAWILI na bado UMOJA (Isaya 48:12). Herufi mbili na bado MOJA kwa maana ni sehemu ya alef-bet moja, sehemu ya familia moja. Je, mnaelewa? Ni kweli. YESHUA ndiYE MASIA, MWOKOZI wa dunia. Na METATRON ndiYE MREJESHAJI. NIsikieni! METATRON ndiYE MREJESHAJI wa [dunia], jiwe la juu kabisa la mwisho (Zekaria 4:7). Kile YESHUA Alianza, METATRON Anamaliza. ALEF na TAV, WAnafanya kazi pamoja – daima wamekuwa wakifanya na daima watafanya. Selah.


Mwisho wa Neno.

8 views

Recent Posts

See All
bottom of page