Unabii 89 "MIMI Ndiye ALEF na TAV. Wekeni Utaratibu katika Nyumba Yenu!"
Updated: Mar 23
Umepewa Nabii Natan’El kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni
Umepokewa 4 Julai, 2020 na
kukamilishwa katika siku zilizofuata
Maandiko Husika
Ufunuo 1:10-11
10 Katika Siku ya BWANA, nilikuwa katika ROHO na
nikasikia sauti kubwa kama ya baragumu nyuma yangu
11 ikisema, “MIMI ndiye ALEF na TAV,
MWANZO na MWISHO,” na, “Kile unachoona, andika kwenye
kitabu haya yote unayoyaona, kisha ukitume kwa makanisa saba, yaliyo Eshia:
Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”
Isaya 26:3-4
3 Utamlinda katika amani kamilifu
yeye ambaye moyo wake umeKUtegemea
kwa sababu anaKUtumaini WEWE.
4 Mtumaini YEHOVAH milele,
kwa kuwa YAH, YEHOVAH, ni Mwamba wa milele.
Ujumbe wa Kinabii
Andika, kwa maana haya maneno ni maaminifu na makweli. MIMI ndiYE ALEF na Tav (Isaya 48:12, Ufunuo 1). MIMI ndiYE MFALME Ajaye karibuni. JINA LANGU ni “NDIMI NILIYE” (Kutoka 3:14). NImekuja kuweka utaratibu katika nyumba. Utaratibu WANGU ni kamili na kweli. Njia ZANGU ni safi, zinadumu milele.
Jione ndani YANGU, mwanaNGU, kwa maana NIko nawe, nawe uko ndani YANGU (Yohana 15:1-17). Usiwahi ondoka kutoka KWANGU MIMI. MIMI ni kimbilio lako imara katika nyakati za taabu na hitaji. Jione safi na takato, kwa maana ukiwa ndani YANGU umefanywa safi. Jioshe katika DAMU YANGU kila siku (1 Yohana 1:5-10). Jitakase katika Maji ya Uzima ya METATRON (Waebrania 10:22). Kila siku NIko nawe.
Utaratibu wa Nyumba huanza katika mawazo. Natembea nawe katika utulivu wa asubuhi, katika kivuli cha jioni. Lakini je unatembea na MIMI, mwanaNGU? Jione ndani YANGU. Tumia ubunifu wako, kwa maana hapo Nakutana nawe, kukutukuza. Tumia akili yako kwa wema, sio kwa uovu (Wafilipi 4:8).
Mawazo yaliyopangika yanapatikana katika Neno LANGU. Kwa maana ukitafakari juu ya Neno LANGU, kila kitu kinawekwa katika utaratibu (Zaburi 1:1-3). Acha mawazo YANGU yawe mawazo yako; Utaratibu WANGU, [uwe] utaratibu wako. Kwa maana Njia ZANGU ziko juu kuliko njia zako na mawazo YANGU kuliko mawazo yako (Isaya 55:8-9). Mipango NIliyonayo kwa ajili yako ni kwa ajili ya wema na sio kwa ajili ya uovu. Kwa hivyo mbona usitake kutafakari juu ya mawazo YANGU, Neno LANGU?
Na kwa hivyo unaona, Neno LANGU ni aminifu na kweli. Tembea naMI. Rithi Ufalme WANGU. Njia ZANGU zote zimejaribiwa na ni kweli. NIlijaribiwa kama unavyojaribiwa. Najua mateso. Najua uaminifu. Najua kutukuzika, kwa maana NIlipokuwa NImepita jaribio LANGU NIlivishwa taji la ushindi (Waebrania 2: ). Na hivyo utakuwa.
Usipepese. Usishangae. Baki tu aminifu na mkweli. Ruhusu Neno LANGU kukujaza kama vile utomvu hujaza mti na kupeana uhai kote katika viungo vyake. NImekuita kwa ushindi, kwa tunda lipeanalo uzima. Tembea tembeanaMI katika bustani – katika bustani ya moyo wako, nafsi yako – na ushiriki mvua ya Mkono WANGU wa Kulia ya kuleta nguvu mpya (Yoeli 2:23).
Sasa ndio msimu wa jubilii yenu. Sasa ndio msimu wa matarajio yenu, wa kuzaa kwenu, wa kuachilia kwenu madeni. Kifedha, kihisia mtasitawi katika njia zote. Acheni tu NIwajaze hadi kufurika. Acha hicho kikombe kimwagwe kama dhabihu yakinywaji kinachoNIpendeza kabisa. Uzito wa maji haukuwahi kuwa wako wa kubeba lakini wa kuupeana tena KWANGU. Maana unapopoteza uhai wako, unaupata milele yote (Marko 8:35).
NIliteseka. NILimwaga DAMU YANGU, maji YANGU (Yohana 19:33-34). Fanya NIlivyofanya na mtasitawi kama NIlivyo[sitawi] na Na[sitawi]. Ni kweli ni hukumu ya kifo, hukumu ya kifo kwa mwili, lakini ndani YANGU mnaishi, mnakwenda na kuwa na uhai wenu. NInapeana uzima kama vile BABA YANGU Anavyopeana uzima (Yohana 5:21). Chochote Asemacho, NInafanya. Hata sasa.
[YEHOVAH] Tulieni na mjue kwamba MIMI NDIMI MUNGU, ELOHIM. Na NItafanyaNItakavyo ndani yenu; kama vijito viendavyo njia yao katika jangwa. NItatengeza njia pale paonekanapo hapana njia na hata nanyi mtashangazwa, mtatoka kwa usingizi, mtatoka kwa kusinzia (Isaya 60:1).
Kama mshtuko wa baridi, itakuwa. Hata kama vile mtu anapoamshwa na mrushio wa maji baridi kwenye uso. Hayo maji baridi ni kicho cha MUNGU. Lakini kinafanya upya, kinazalisha. Nyinyi nyote mtakuwa na tukio hili, kwa maana lazima NIamshe Bi-Arusi WANGU. Hiyo ndiyo maana NInatuma METATRON WANGU katika hizi nyakati za mwisho (Malachi 3:1-3). Kwa hivyo ingieni katika viwango vyenu, ingieni katika laini, maana mstari juu ya mstari, kanuni juu ya kanuni lazima itimizwe. Na Neno LANGU halitarudi KWANGU bure (Isaya 55:10-11). Hakilazima itimizwe.
Uumbaji wote unaNIlilia kwa ajili ya utimizaji wa Neno LANGU, kwa ajili ya udhihirishaji wa Wana wa MUNGU, ELOHIM (Warumi 8:19). Uumabji wote unaNIlilia MIMI, YEHOVAH, kwa ufunuaji wa YULE UMOJA. MIMI ni UMOJA. MIMI ni EKHAD. EKHAD ni UMOJA. Shema Yisrael YAH ELOHEINU YAH EKHAD (Kumbukumbu 6:4).
Nyote mnaNIhitaji, wanaNGU na mabinti WANGU. Nyote mnahitaji kuja chini kwenye Mto kwa ajili ya uoshaji wa Neno. NIko nanyi, kweli, lakini mnaNIhitaji zaidi sasa kuliko mbeleni. NIsikizeni na msitelekeze njia za kale. Njia za kale ni zipi? Torah YANGU iliyojaribiwa na kweli. Je siYE YESHUA Njia, Ukweli na Uzima (Yohana 14:6)? Je Hakufuata Torah (Mathayo 5:17)? Basi nini kisingizio chenu cha kutofuata njia ZANGU? Fanyeni kama Alivyofanya na mtasitawi. Msifanye kile ambacho ni sawa machoni mwenu, kwa maana huu ni upumbavu, huu ni wazimu.
Uabudu sanamu ni baa. Msiruhusu shetani kutaabisha maisha yenu. Msiishi katika dhambi (Warumi 6:12-13). Msimu wa neema YANGU unafikia mwisho. Wote watahukumiwa. Na ni kitu cha kuogofya kusimama mbele ZANGU, MUNGU AISHIYE. Jiweke katika utaratibu. Msitandawaini (msilale/msisinzie) mezani. Simameni wima. Ninawatazama, watoto WANGU, na Nahitaji mfano. Ninahitaji mshahidi kuNIshuhudia MIMI, [kushuhudia] UMOJA WANGU. Je, Wayahudi wataamini vipi ila kuwe na nuru kwa mataifa? Na Naanza nanyi, salio LANGU aminifu, lakini Nahitaji utaratibu. Nahitaji sheria; kuweka pamoja kwa vipande kuNIonyesha mnaelewa.
Kila mmoja wenu simameni mbele ZANGU kama ile Menorah yenye matawi saba yanayowakilisha Roho Saba za MUNGU, za ELOHIM. Ng’aeni kwa wangavu kwa ajili YANGU, MIMI, YEHOVAH. Msiwahi acha nuru izime. Msiwahijiweka katika nafasi ya kujisalimisha kwa dhambi. MIMI, YEHOVAH, ni angamizi. MIMI, YEHOVAH, ni Mpaji-uzima, kwa maana NInaua na kufanya hai (Kumbukumbu 32:39).
Chungeni ulimwengu, NInapotuma salio LANGU, wakati NInapotuma METATRON WANGU! Wataenda na kufanya vijasiri! Wataenda na kutwaa na kushinda. Hakuna chochote ambacho hawataweza kutimiza, kwa maana wataenda katika pumzi na ROHO wa ELOHIM wao. Kilio cha midomo yao kitakuwa kitakatifu. Watatangaza JINA la YESHUA kutoka mwisho wa dunia hadi mwingine na hakuna watakaowafukuza.
MSISIMAME mbele yao katika ukaidi! Msisimame mbele zao katika chuki! Wale wanaotafuta kuwadhuru watateketezwa na NENO la mdomo wao na MOTO ulio machoni mwao (Ufunuo 11:5). Ole na iwe kwa ulimwengu katika siku hiyo ya majaliwa! NInaweka msingi. NInaita gharika kuinuka. Mataifa yatainuka na mataifa yataanguka. Mataifa yote ni kama tone katika ndoo na NInatakuwa na hukumu YANGU (Isaya 40:15). NIlitafuta rehema na NIkapata uovu. NIlitafuta ukweli na NIkapata uwongo. Hakuna yule afanyae wema (Zaburi 14:2-3).
Kwa hivyo NIlituma MWANANGU YESHUA HAMASHIACH (Yohana 3:16-21). Kwa hivyo NIlituma MWANANGU kumwaga DAMU YAKE, kupatanishia nafsi za wanadamu. Wote wanaoMpokea, wanaNIpokea MIMI, YEHOVAH. Wote wanaogeuka kutoka kwa njia zao za uovu na kuMtumainia wataokolewa. Endeleeni katika ustahimilivu. Endeleeni katika uvumilivu. Msitelekeze njia za kale, njia ya zama.
NIsikizeni, ee Israeli. NIsikizeni na mtii. Msiwafukuze wale Mashahidi Wawili (Ufunuo 11:1-14). Wanakuja katika njia hamfikirii. Hawaji kulingana na thiolojia yenu. NItafuteni mapema na mtaNIpata (Yeremia 29:13). Tafuteni ufahamu WANGU na hamtapotoka, hamtateketezwa katika kutotii. Tembea naMI naMI NItembee nanyi. NItakuwa na njia YANGU ndani yenu, ee Israeli, hata kama vijito nyikani. Kubalini MWANANGU YESHUA na mtawekwa huru. Mmelemezwa na mizigo ambayo si ya KWANGU. NImekuja kuwaweka huru. Chukueni mzigo WANGU juu yenu. Chukueni nira YANGU (Mathayo 11:28-30). Tembea naMI naMI NItembee nanyi.
Chukueni Tawi LANGU la Mzaituni. NInawapa amani, ee Israeli. Njoni chini ya kivuli, kinga ya METATRON WANGU na mjifunze kuNIhusu, mjifunze kuhusu MASIA. YULE ambaYE Anapaswa kuja ni mkuu na mwenye nguvu. YULE ambaYE Anapaswa kuja ni ALEF na tena Tav. Jifunzeni kuNIhusu. Msiache shetani awashawishi, kuwapenya na uwongo wake, na mwana wake (2 Wathesalonike 2:1-12). MIMI NDIMI MFALME! MIMI NDIMI MASIA na YESHUA ndilo JINA LANGU! Msisikize mwingine. Amkeni, Bi-Arusi wa Israeli alalae (Isaya 52:1-2). Amkeni na mje KWANGU, kwa maana ni MIMI, MTEUAJI wenu, ambaYE yuko hapa! NInawateua kwa uzima, kwa uhuru mnapopatikana ndani YANGU.
Msipuuze Wokovu wenu, hadhi yenu watoto WANGU (Wafilipi 2:12). Msipuuze na jueni kuwa ni MIMI, MIMI NInaYEfunza katika msimu wa usiku. Ni MIMI ambaYE ni Mwaminifu na Mkweli, Mwenye nguvu na wakutafakariwa juu YAKE. MIMI NDIYE, MFALME wa UTUKUFU WOTE. MIMI NDIYE nafsi yenu inatamani sana. MIMI NDIYE NInayeokoa. Shema Yisrael! NIsikieni na mtii. Ninanena mara moja na Mbingu zinatingisika (Yoeli 3:16). Je, ni vipi ziaidi unafaa, ee mwanadamu, unayekaa duniani?! MIMI ni WOKOVU wenu lakini msikanyagie chini DAMU YANGU (Waebrania 10:26-31). Wakati mnapofanya mazoea ya kufanya dhambi, umekuwa mvunjaji sheria. Je, hii imekuwa kazi yenu, watoto WANGU? Mnapaswa kujishughulisha hadi kuja KWANGU lakini sio kutumia neema YANGU kama leseni ya kutenda dambi. Msitende dhambi tena. Tubuni na mtahadhari au miale ya jahanam iwateketeze!
NIngependa kwamba yeyote asiangamie lakini hae[!], SIweziwachagulia (Kumbukumbu 30:19-20). Lazima mgeuke kutoka kwa njia zenu za uovu. Lazima mpendeze BABA. Nawezawaombea lakini SIweziwachagulia (Warumi 8:34). NInaonyesha rehema. Je, hiyo inawatosha?