top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 10 “Jitayarisheni kwa Ajili ya MFALME Kutawala!”

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa Nabii Hannah kwa sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni


Umeandikwa 27 Januari, 2019

Ujumbe wa Kinabii


(Tulikuwa tunaabudu, halafu nikaona YESHUA Akiingia wakati tulikuwa tunaimba wimbo wa kwanza. Nilisikia upepo 4 zikipuliza …)


Naam, abuduni Uwepo WANGU. NInawatia mafuta, nyinyi nyote! Na mabusu YANGU ya manukato. Ufalme uko tayari. Tayari kutawala. Matayarisho yamefanywa. MFALME wa Wafalme, BWANA wa Mabwana Yuaja Duniani kutawala!!! (Nahisi Mbingu zimehifadhi nguvu nyingi sana)


Usikawie, jitayarishe. Ingia katika Neno LANGU. Chagua siku hii ni MUNGU yupi utatumikia. Na heri uchague Yule MUNGU sawa. Njia ya uhai ni moja, mauti pia ni moja. Tumefanya mengi sana. Kuokoa wanadamu kutoka kwa laana ya milele. Ishafanywa. JINA LAKE ni YESHUA. Nyama iliyokolea, iliyokamilika.


Naam, kaza fikra. Lazima NIje katika hasira YANGU kali! Lazima NIje NIfanye kazi YANGU ambayo NIliahidi YEHOVAH! Si jambo dogo. Wengi hawaelewi na watashangaa. Watoto WANGU, mko katika maji, lakini Niko nanyi. Hamtazama. Fanyeni kazi pamoja kwa Utukufu WANGU.


(Tuliimba wimbo wa kuabudu, ABBA YEHOVAH Azungumza …)

Moto kwenye watu WANGU! Moto! Na zaidi! Na utaenea kama moto wa mwituni! Mbele Utaenda! Eneza! NENO LANGU la moto! Litakuchoma, MIMI tu. Kuna wakati. Wakati huu, kufukiza uvumba. Nyinyi ni uvumba WANGU, bakuli LANGU la uvumba. Teketeeni kwa ajili YANGU! Manukato yote! Nayataka! Inachoma tamaa zenu zote, ikiacha tu MIMI ndani yenu. Hivi ndivyo ilipaswa kuwa. Dunia nzima ilipaswa kuwa hivyo. Lakini wanaitelekeza.


(Naona Serafim wakionekana mahali petu katika maono.)

Marekani! NIlikupa rehema! NIlikupa Donald Trump. Atafanya mapenzi YANGU, lakini unakataa. Atafanya kazi YANGU, kuchoma na kuangamiza minara ya baali. Yeye ni kiongozi wa haki mradi atubu. Anasikia kile anahitaji kuNIfanyia. Yeye ni kifaa CHANGU cha kuwatimizia vitu. Marekani! Kwa sababu bado NInao watu wanaNIlilia! Kwa ajili yao. Kwa ajili yao!

Amsha dunia yote! MFLAME Anakuja! Mko tayari? La, wengi wenu hamko (tayari). Funzeni na mshiriki njia ZANGU. Zinarefusha maisha yenu. Watoto, funzeni wengi. Shirikini kwenye YouTube. Funzeni, dhihirisha huo upendo. Msijali wanachofikiri, maana ni kweli. Dhihirisha njia YANGU, mapenzi YANGU, fikra ZANGU.


KuNIhusu MIMI tu, Takatifu na Adili. Kuweni safi pamoja naMI. NIruhusu NIongee nanyi. NIwakumbatie na NIwafurahie. Watoto WANGU Wachanga, Biarusi WANGU! Furahieni naMI! NImekuwa NIkingojea siku hii kwa muda mrefu sana.


Mapenzi [yaani kudura] yenu si mazuri kabisa. NIpeeni utawala wenu. Acheni MIMI NIwathibiti. Na kuwaletea ukombozi zaidi. NIongeleshe wakati kumenyamaza, sikia mnong’ono WANGU… Mapenzi [kudura] YANGU… Jinsi yalivyo safi … Utukufu wa Dhahabu… Shh… Kuwa katika Uwepo WANGU.



Mwisho wa Neno

4 views

Recent Posts

See All
bottom of page