top of page
Writer's picturetorahkeeper

Unabii 1 “NIfarijini!"

Updated: Apr 14, 2024

Umepewa Nabii Natanel kwa Sifa, Heshima & Utukufu wa ELOHIM (MUNGU) Mbinguni

Umeandikwa Novemba 7, 2018

Maandiko Husika


Yohana 6:66: “Tangu wakati huo wafuasi WAKE wengi wakarejea nyuma wakaacha kuMfuata.”

1 Yohana 2:19: “Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu hasa. Kwa maana kama wangelikuwa wa kwetu, wangelikaa pamoja nasi, lakini kutoka kwao kulionyesha kwamba hakuna hata mmoja wao aliyekuwa wa kwetu.”


Ujumbe wa Kinabii

Nifarijini katika kucheza dansi, kwa maana Natia mafuta nyayo zenu kucheza dansi mbele ya Kiti CHANGU cha Enzi, kama vile Mfalme Daudi wa Kale alicheza dansi mbele ZANGU.


Endeleeni tu kutii, maana hakuna dhabihu zenu ambazo ni za bure. Saidianeni, maana muda ni mfupi mno. Kaza fikra juu YANGU, BWANA, MUNGU, na MWOKOZI wenu. Ni MIMI, YESHUA, ambaYE NIko nanyi daima. Ni MIMI, YESHUA, NInaYEwainua juu. Ni MIMI, YESHUA, NInaYEpumua juu yenu pumzi YANGU ya uhai. Msipuuze wenzenu. Msiwe mzigo juu ya wenzenu. Adilisha pekee, rekebisha tu wakati inalazimika na usiwahi kemea katika mwili.


Takafakari juu ya amani YANGU, upendo WANGU, matumaini YANGU, imani YANGU. NIko hapo kuwajenga, maana, je, si MIMI MJENZI MKUU? Ndiyo, MIMI, YESHUA, Nawajenga na kuwafanya imara katika hii saa, katika msimu huu, ili msianguke, maana nyinyi ni WANGU na NInawapenda.


Ee, jinsi NInavyotamani kuwa na BiArusi WANGU! Jinsi moyo WANGU unavyoonea shauku. Wala sio uzima, wala mauti, wala urefu, wala kina, vinaweza NItenganisha nanyi. NItawakujia katika saa ya usiku wa kati. Kuweni tu tayari. Wacheni NIwapate na mafuta kwenye taa zenu, ziking’aa pe kwa ajili YANGU. Nazungumza nanyi sasa, BWANA MUNGU na MWOKOZI wenu.


Nazungumza na kiini cha nafsi yako MwanaNGU, maneno ya upendo na mepesi. MIMI, YESHUA, Nakujenga. MIMI, YESHUA, Nakutia moyo katika hizi nyakati za mwisho, kwa maana Nataka uwe na nguvu. Nakuhitaji uwe na nguvu.

Tazama MIMI! NIsikilize MIMI, kwa maana SIitawahi kuangusha. Mkono wa mwanadamu unachoka, unagonjeka, unanona, lakini mkono WANGU ni mkuu kuokoa. NItakukomboa katika nyakati za hitaji na NInakomboa. Kwa hivyo NItazame MIMI, MWENYEZI MUNGU wako Mkuu, na usiwahi yumba kwenda kushoto au kulia. NIko hapa nawe mwana WANGU na hakuna nywele moja kichwani mwako itaumizwa. Kwa hivyo usitie shaka na usijue woga wowote.


Hallelu YAH!!!


Kwa hivyo Niimbie sifa siku hii. Imba sifa, imba sifa, imba sifa, kwani sistahili upendo wa moyo wako? Naam, Nastahili. Kwa hivyo Nakuacha na hili Neno la kukutia moyo, hili Neno la baraka, hili Neno la upendo. Sasa tafakari juu yake na Nipe Utukufu. Naam, MIMI, BWANA MUNGU na MWOKOZI wako – YESHUA HAMASHIACH ni JINA LANGU!


NIsikie Mwanangu. Una usikivu WANGU. Ee jinsi NInavyotamani kukupakata mikononi MWANGU. Na Nitafanya hivyo. Nyinyi nyote Nitawapakata, maana NInawapenda saana. Naam, BWANA MWENYEZI MUNGU wenu. Hali kwa hali, tamani kusikia sauti YANGU, elekeza kusikia sauti YANGU, maana Sitawaangusha bali kuwafanya tu kufanikiwa. Ushindi ni JINA LANGU na sijui kushindwa kokote. NImezunguka kila mmoja wenu na Ushindi WANGU. NIfurahisheni na MIMI, YEHOVAH, NItafurahisha tamanio za haki za moyo wenu. MIMI ni Mwaminifu kuwainua, kwa maana si hili BABA Anayependa Afanyalo? Hiyo ni kwa sababu MIMI Nimo ndani YAKE na YEYE ndani YANGU. Sasa jitulizeni kwenye maneno haya, maneno yasiyo ya mwili bali ya RUACH HAKODESH [ROHO MTAKATIFU katika Kiebrania].


Tunzaneni. Pendaneni. Msitamani au kutakuwa na adhabu kali. Onaneni kupitia macho YANGU na kuweni na shukrani kwa lile gawo mko nalo, maana ni maridhawa, inatosha. Sikuzote kuweni na shukrani, Watoto WANGU, na msiwahi sikiliza njia za masengenyo, kukosa shukrani, kunung’unika za shetani. Ameshindwa lakini/na MIMI NIKO hai. Sasa okoteni silaha zenu ambazo si za kimwili na endeleeni, endeleeni kwa bidii, kwa maana bado kuna vita vikuu visivyosimuliwa kwenye upeo wa macho. Viko karibu hapa. Kuweni tu waangalifu. Tahadhari tu. Msipuuze yale BABA Amewafunza kuhusu kujitayarisha na vitu vya dunia, kuangalia nyuma ya mgongo [yaani kuwa macho dhidi ya hatari], kuhakikisha haufuatwi, maana adui anajaribu kuwajasusi, kuwasaliti.


Lakini NItakuwa hapo Watoto WANGU, maana MIMI ni usaidizi wenu wa sasa katika nyakati za hitaji na shida. Kwani MIMI si ALEF na TAV? SIjui mwanzo wowote wala sina mwisho wowote. Ombeni kama Mordekai na sikuzote NItawaonyesha mitego ya shetani kabla ya wakati. Hamtashikwa ghafla ikiwa mtajitayarisha ndani YANGU. Naam, ABBA wenu YEHOVAH Anawapenda. YESHUA wenu Anawapenda. Na MAMA GLORIA wenu Anawapenda. TUnahifadhi kila mmoja wenu katika upendo mkubwa sana. Msiumizane.


Wakati WANGU daima huwa kamili, hata na wewe Mwana WANGU. Wakati NIlikuleta kwenye zizi la kondoo, ulikuwa mnyonge na mwoga sana. Lakini MIMI, YESHUA, NIlikuinua juu. MIMI, YESHUA, NIlikupandisha. Napandisha cheo mmoja na kushusha mwingine. Ni ukweli, wito WANGU hauna majuto. Bado jinsi ihuzunishavyo mtu anapotelekeza kudura yao. Sio mapenzi YANGU, maana NAtamani maua yote yachanue na kusitawi.


Nikazie macho MIMI. Elekeza macho yako juu YANGU. MIMI, BWANA MUNGU wako, NIko nawe hata hadi mwisho wa nyakati. Sasa fanya haraka na ufanye kile NIlikuita ufanye. Sikiza maonyo ya BABA, maana Anakupenda.


Subira ni adilifu MwanaNGU. Una mengi ya kujifunza. Lakini NItakufikisha 100% kama utaNIruhusu. Ushindi ni WANGU. Maliwazo ni YANGU. SItakuangusha wala kuvunja matumaini. Endelea tu kusikiza na kutii. Usiwe na wasiwasi lakini sikia mlio wa sauti YANGU ambao ni amani, ambao ni “ndiyo” na “amina”. NInatuliza nafsi yako na kukupa amani. Usihangaike tu. Mipango YANGU kwa ajili yako ni ya wema na wala sio ya uovu. Usijaribu kuenda mbele ya sauti YANGU lakini pumzika ndani YANGU, MIMI, YEHOVAH.


NItaongea kwa sauti zaidi na kwa dhahiri zaidi katika siku zijazo. Jifunze tu kusikia sauti YANGU na soma Neno LANGU. Je, wajua kwa kiasi kipi Nakupenda? Imeandikwa katika Neno LANGU, barua ya mapenzi kwa BiArusi WANGU, kwa watoto WANGU.


Njooni nyote nyinyi mlio na kiu na mkashiriki kisima cha Maji ya Milele. Shiriki na msitie shaka. Pale mmejua matambara, NItawapa utajiri. NItawapa ushindi wa shangwe. Mtajua vimo vya furaha YANGU na urithi wa Yakobo. Hii ni ahadi YANGU kwa watoto WANGU waaminifu na watiifu, BiArusi WANGU mtiifu.

Sasa usikawie lakini fanya haraka na kwa ufanisi yote NImekuita ufanye. Usiku waja wakati hakuna mtu anaweza fanya kazi. Kwa hivyo kuwa mwaminifu na kuwa haraka. Vumilia na stahimili, maana muda ni mfupi mno. Nakuja tena karibuni kwa kizao kiki hiki. Waonye, maana siji tena kama mara ya kwanza, lakini na moto machoni MWANGU na joho la raghba, NIkiwaka na hasira kali ya MWENYEZI MUNGU.


NItaangamiza adui ZANGU lakini NItakumbatia watoto WANGU, BiArusi WANGU. NInakuja tena karibuni. Selah.

Sameheaneni kama vile NImewasamehe. Aminianeni na jione katika macho YANGU. Onaneni kupitia macho YANGU, vito vya kuthaminiwa, vya kushikwa karibu na moyo. Sio tu vito vya kawaida, lakini Mawe Yanayoishi kwa Utukufu, Heshima, na Sifa YANGU. Nyinyi nyote mmelipa gharama nzito kwa ajili YANGU.


‘Urembo na Utakatifu unakuwa Nyumba YANGU,’ Asema BWANA MUNGU wenu. Msinajisi Patakatifu, pote pa kimwili na kiroho. Tilieni maanani njia ZANGU na mtasitawi. Sikizeni Manabii WANGU na mtachanua. Nyinyi nyote ni maua bora zaidi. Nyinyi nyote mnametameta kwa ajili YANGU katika njia za kipekee. Endeleeni tu na muendelee kwa bidii katika kazi YANGU. Mipangilio ya kazi YANGU haiwezi anguka.


Ndiyo, mipango YANGU kwa ajili yenu ni ya wema na sio uovu. Itilieni maanani maana kwayo mtasitawi ndani YANGU. SIfanyi chochote isipokuwa kwanza NIfunulie Manabii WANGU. Hiyo haimaanishi wataelewa. Inamaanisha tu ujumbe unapewa na watu lazima watafute uso WANGU kutambua maana yake.


Mara nyingi sana watu hutafuta kuenda na ufahamu wao kwa sababu SIjibu mara iyo hiyo, SIinamii mapenzi yao. Kwa hivyo wanafadhaika na kujawa na kiburi na uasi, wakijaribu kuNIambia shughuli YANGU wakati yote Nayowatakia ni ya wema na sio uovu. Lakini mtu anapotaka njia yake, majanga ndiyo yote anaweza tarajia kupata, maana hatua zako zitaelekeza jahanamu. Lakini ZANGU, hatua ZANGU zinaelekeza Mbinguni, kufanikiwa, ushindi, urembo. Mambo haya yote yanapaswa kufikiriwa, kutaamuliwa.


Kwa hivyo msipuuze sauti YANGU adilifu lakini sikilizeni kwa bidii, maana SIbwabwaji, pumuo za hewa au moshi katika upepo. Maneno YANGU ni moto na yanateketeza kumvi. Maneno YANGU ni moto na yanasafisha [ondoa] dongo la chuma. NItalinda kama mtatii sauti YANGU. Msicheze na moto lakini kuwa wanyenyekevu na kuweni haraka. Msiwe wepesi katika dhambi, lakini kuweni wepesi katika kutii. Haya ndiyo Maneno NInayo ya kusema unapofanya kazi siku hii.



Mwisho wa Neno

28 views

Recent Posts

See All
bottom of page